Ilikuwa mwaka 1984, majira ya asubuhi nilimshuhudia mwalimu wetu katika shule ya sekondari ya bweni iliyoko kijijini kwenye baridi na huku akiwa amekumbatia redio yake ya mkononi, ukali wake aliuweka kando akifuatilia kwa karibu taarifa redioni. Nasi wanafunzi tukajongea alikosimama, tusidadisi kulikoni redioni? Ndipo tukasikia sauti ya Rais Nyerere, akitangaza taarifa ya kifo hicho.
Sisi tukaingia kwenye huzuni na mijadala ya mino’ngono, hali kadhalika walimu na ndicho kilikamata taifa zima kwa wakati huo, kila mahali kukazizima. Ni ishara tosha kwamba alikuwa kipenzi wa wakubwa na wadogo, isipokuwa mashabiki wa wizi, dhuluma na maovu.
Ni msiba uliompata Mwalimu Nyerere kwa kumgusa mtendaji wake mkuu serikalini, uliomuumiza kisaikolojia, huku ikimkatisha bashasha ya maandalizi ya saa 24 mbele, kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake kijijini Butiama,.
Kwanini nchi ilizizima kwa kifo hicho? Sokoine ana sifa nyingi. Inajumuisha uzalendo, uchapakazi, makini na mtu anayedai matokeo ya kweli katika utendaji wake, kwa maana ya kufanya ufuatiliaji wa kila alichokitekeleza au kuahidiwa.
Hata kifo chake, alikuwa safarini akitokea akiwa kwenye safari ya gari eneo la Dakawa Morogoro, akitokea Bungeni Dodoma kuelekea Dar es Salaam. Sababu kuu ya kutumia barabara, ilikuwa haja ya kukagua ustawi wa mazao shambani, lakini bahati mbaya uwanda wa mauti ukampata.
Dhana ya ubora wa utendaji na umahiri wa kufuatilia mambo, nilibahatika kupata ushuhuda kwa marehemu Mzee Geofrey Mhagama, ambaye ana simulizi kubwa ya uchapakazi wa Sokoine, binafsi akajifunza muundo mpya wa utendaji serikalini.
Anasema, akiwa naibu waziri katika wizara mpya iliyoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1970, Sokoine alimfunza kufanya kazi kwa mipango, udhibiti na ufuatiliaji makini.
Kwa mujibu wa Mzee Mhagama, alijikuta anaingia katika tabia na utaratibu wa kuandika kila jambo la kikazi, ikiwamo ahadi wanazopewa kazini na namna ya kufuatilia matokeo yake, ili asiponyokwe na ‘umakini’ na ‘ufuatiliaji.’
Anasema, kuna wakati alishangazwa alipoitwa na bosi wake, Waziri Sokoine, aliyemuuliza matokeo aliyopata kutokana na ahadi walizopewa kote walikopita, ikiwamo zile alizodhani ni ‘blabla’za ziarani, jambo lililomfanya anyanyuke ofisini mara moja, kwenda kufuatilia majibu ya ahadi hizo.
Mbali na nafasi katika Baraza la Waziri, Mhagama alikuwa mbunge wa Songea na baadaye alikuwa mkuu wa wilaya katika maeneo tofauti nchini na katika maisha yake ya ustaafu, alihitimshia na uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa Ruvuma, kabla ya umauti wake wastani wa muongo mmoja sasa.
Ikirejewa hata katika vita dhidi ya uhujumu uchumi, ufisadi na rushwa, ilityofungiliwa mahakama yake maalum ya uhujumu uchumi, msukumo unaoendeshwa na serikali iliyoko madarakani sasa, ina wasifu wote wa kupokea kijiti cha kazi nzuri iliyoanzia ngazi ya awamu ya kwanza na kupitia awamu nyinginezo.
Miongoni, inajumuisha hatua ya maboresho ya kisheria; huduma za kipolisi kuhamia Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takuru), iliyoboreshwa zaidi kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Vivyo hivyo, huduma hiyo ya polisi ilisafiri hadi kuanzishwa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, iliyopitia hatua sasa kuwa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Mambo hayo yote na yale ambayo leo hii yana ubatizo wa ‘ufisadi’ huko nyuma yalibeba jina la asili la ‘uchumu uchumi’ katika hilo, Waziri Mkuu Sokoine, anakumbukwa sana alivyopambana katika nafasi ya utendaji mkuu wa serikali.
Bado kumbukumbu imebaki, kwamba mwanzoni mwa miaka 1980, anakumbukwa ukamanda wake kupitia kioo cha ‘Vita ya Uhujumu Uchumi’ ambayo hadi leo imebaki mfano wa kuigwa na kwa kiasi kikubwa, kinachofanyika sasa katika vita hivyo, kinashabiliana na matendo ya zama za Sokoine.
Historia yake
Sokoine, alizaliwa Agosti Mosi ya mwaka 1938, huko Monduli mkoani Arusha, Ilipofika mwaka 1948 alianza elimu ya Msingi kwao Monduli na baadaye akafaulu darasa la nane, akachaguliwa kuendelea katika Shule ya Sekondari Umbwe, iliyoko Moshi, alikohitimu mwaka 1958.
Mwaka 1961, ambao nchi ilipata uhuru, ikiwa ni miaka mitatu baada ya kumaliza shule na alijiunga na chama cha TANU na mwaka mmoja baadaye, alipata fursa ya kwenda mafunzoni nchini Ujerumani, alikohitimu mafunzo ya miaka miwili mwaka 1963.
Baada ya kurudi masomoni, aliteuliwa kuwa Ofisa Mtendaji wa Wilaya ya Masasi na ndipo akagombea na kupitishwa ubunge kwao. Hapo ndipo neema ilimfungukia, akiteuliwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Usafirishaji na Kazi.
Mwaka 1970, alipandishshwa, akishika nafasi ya uwaziri wa nchi na miaka miwili, 1972, baadaye aliteuliwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, alikoendelea kudumu hata katika baraza lingine la mawaziri, baada ya uchaguzi wa mwaka 1975.
Pia, wakati huo mwaka 1977, ikiwa imeanzishwa CCM, aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, huku akipanda zaidi kuwa Waziri Mkuu, alikodumu hadi mwaka 1981 na kisha akateuliwa tena katika nafasi hiyo, mwaka 1983, hadi kifo chake, siku kama ya leo miaka 34 iliyopita.
Wasifu huo wa maisha ya marehemu Sokoine, haishangazi kuona leo hii ni Siku ya Taifa, mahali alikofia kunajengwa mnara maalum wa kumbukumbu na Chuo Kikuu cha Kilimo Mrogoro, kilichoanzia kuwa kitivo cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sasa ni Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), sekta ‘iliyomkosha’ marehemu Sokoine, hata kifo chake kilikuwa katika mazingira ya kukagua maendeleo ya kilimo nchini.