Edward Ngoyai Lowassa

Ukimwacha Hayati waziri Mkuu Sokoine kiutendaji anaye fuata ni Marehemu Lowasa.
Wawili hawa walikuwa ni majembe kwelikweli.....wafuatiliaji mambo na wabunifu.
Leo hii sukari tu inatutoa jasho!!!!!!!!
 
Ukimwacha Hayati waziri Mkuu Sokoine kiutendaji anaye fuata ni Marehemu Lowasa.
Wawili hawa walikuwa ni majembe kwelikweli.....wafuatiliaji mambo na wabunifu.
Leo hii sukari tu inatutoa jasho!!!!!!!!
Ila mmoja alikuwa mwaminifu sana kwa rasilimali za nchi na madaraka yake ila mwingine alikuwa mwizi mfujaji wa mali za umma na fisadi papa na mlevi wa madaraka
 
MAPIGO 10 YA CCM KWA LOWASSA

Haikuwa Jambo rahisi kwa CCM kumshuhudia Kiongozi mkubwa ngazi (Waziri Mkuu) kukihama CCM na kujiunga na Chama cha upinzani CHADEMA.

Usiwaone leo CCM msibani wanalia na kupishana kutoa maneno mazuri kwa Mzee Lowassa ukajua hadi roho zao ni nzuri, HAPANA.

Ukiondoa vicheko, tabasamu na maneno matamu ya CCM wanapokuwa mbele ya kamera huwa wanaupande wa pili wa sura zao na roho zao.

Lowassa alishawahi kuziona sura halisi za CCM, tena waliokuwa Viongozi wenzie, marafiki,'family friends' na aliokuwa anakula na kuywa nao kila siku. Baada ya kugusa maslahi yao kwa kuihama CCM

Walimpiga mapigo haya

1. Pigo la kwanza,ilikuwa marafiki aliokuwa nao katika kambi yake ya CCM (safari ya matumaini) na waliomshawishi 'amwage mboga' kwa kuihama CCM.Baada ya Lowassa kutii ushauri wao.marafiki hao hawakuhama,wakabakia CCM.

2. Baada ya uchaguzi 2015, Serikali ya CCM ikamuondoa mtoto wa kike wa Lowassa ( Pamela ) aliyekuwa anafanya kazi BOT Makao makuu Dar es Salaam na kumpeleka BoT tawi la Arusha tena bila kupangiwa kazi yoyote.

3. Apiri 16,2016 Mkwe wa Edward Ngoyai Lowassa (Sioi Sumari) akafunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha $6M akakaa gerezani miaka

4. Haikutosha,Shamba la kufugia na kukuzia mifugo la Mzee Edward Ngoyai Lowassa lililopo Mkoani Tanga,Handeni likataka kuporwa na serikali lote,Waziri mmoja kutoka Baraza la mawaziri la Magufuli akashauri walimege nusu tu,badala ya kupora lote. Wakalichukua nusu.

4. Shamba lingine la Mzee Lowassa lilipo mkoani Tanga ,Loshoto likiwa linasafishwa na Bulldozer, Serikali wakazuia zoezi lisiendelee. wakampelekea Mzee Lowassa bill ya billion 10,kama malimbilizo ya kodi ya ardhi ya shamba lile.Mzee akalitema,Serikali wakalibeba.

5. Serikali ya CCM,pia wakamfuata Fred Lowassa (mtoto wa Kiume wa kwanza wa Mzee Lowassa) wakamlima kodi kupitia TRA kiasi cha zaidi ya Tsh billioni 5,katika biashara zake,wakazifunga akaunti zake binafsi na za biashara mpaka atakapolipa kodi zote.

6. Mzee Lowassa alikuwa anatibiwa na kuhudumiwa na Serikalini,kama Waziri Mkuu Mstaafu,ambapo alikuwa anaenda katika klinic ya matibabu nje ya nchi kila mwaka.

Lakini baada ya kuhamia CHADEMA wakafuta huduma hiyo Mzee Lowassa akawa anajihudumia mwenyewe kwa fedha zake ktk matibabu.

7. Mzee Lowassa alikuwa anaishi Dodoma maeneo ya Area D,katika nyumba za Serikali (TBA) Kama mpangaji na Mtanzania mwingine

(Ile nyumba ambayo alipokuwa CCM watu mbalimbali walikuwa wanaenda kumuomba agombee urais)

aliporwa ile nyumba na serikali ya CCM,kwa sasa nyumba ile amepewa Rais Hussein Mwinyi anaitumia kama makazi yake anapokuwa Dodoma.

8. Pigo jingine,mlinzi wa muda mrefu wa Mzee Lowassa Bw. Tendewa ambaye alikuwa siyo Mlmlinzi tu bali mtu wa karibu kwa miaka mingi sana.

alisimamishwa kazi punde baada ya Mzee Lowassa kuhamia CHADEMA tu akiwa amebakisha miezi 6 kustaafu utumishi wake, na akapoteza mafao yake yote.

9. Wafanyabiashara na marafiki wa Mzee Lowassa Dar na Arusha wakafilisiwa,wengine kutishwa mashitaka au kufuatiliwa na TISS kama bado wanamawasiliano na Lowassa (wakataka afe njaa)

10. MONDULI-Siku moja Serikali ilienda Mkoani Arusha,Monduli katika shamba la Mwekezaji (Mzungu) wakiamini ni Shamba la Mzee Lowassa wakalitaifisha na kisha wakaligawa kwa Wanakijiji kumkomoa Mzee Lowassa.
lakini halikuwa shamba lake bali la Mwekezaji wa miaka mingi

Wakahakikisha pale Monduli wanaondoa heshima ya Mzee Lowassa kwa kuweka DC atakayekuwa anamdhalilisha Mzee Lowassa, wakahamisha Mbunge na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli kutoka CHADEMA kuhamia CCM ilikufuta kabisa legacy ya Mzee Lowassa.

Mwisho
Mapigo yote haya hayakumfanya Mzee Lowassa Kupiga magoti kwa serikali ya CCM au kurudi CCM.

kwa muda wa miaka 4,kuanzia 28-07-2015 alipohamia CHADEMA hadi tarehe 28 -02- 2019 alikuwa ni mtu mwenye msimamo mkali sana usiotetereka.

01/03/2019 Lowassa alirudi CCM ili kumnusuru rafiki yake kipenzi ROSTAM AZIZI ambaye alipigwa mapigo mawili tu na serikali ya CCM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Siku ya Ijumaa ndiyo itakuwa rasmi kwa waombolezaji wote kutoa heshima zao za mwisho na kuiacha siku ya Jumamosi kwa ajili ya familia na viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Rais @SuluhuSamia , viongozi wa kimila watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho siku hiyo, ibada takatifu ya mazishi itaongozwa na KKKT na kwa kuzingatia kuwa haya ni mazishi yenye hadhi ya kiserikali JWTZ ndilo linaloshughulikia taratibu za mazishi yenye heshima ya kijeshi ikiwemo kupiga mizinga 17 wakati mwili ukiteremshwa kaburini," - Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi

#RIPLowassa
#EastAfricaRadio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
___
Edward Ngoyai Lowasa ameondoka. Yuko mahali salama pasipo na mgao wa umeme wala usanii wa treni za umeme. Amepumzika baada ya kazi ngumu. Anapokufa mtu mzito kama Lowassa, kuna makundi matatu hujitokeza;
1. Wanaolia
2. Wanaofurahia
3. Wasiojua kama walie au wafurahie.

Makundi yote matatu tunayo katika kifo cha Edward Lowasa. Mimi sijui nipo kundi gani lakini niseme mambo manne ninayokumbuka:

1. Dola yetu ina mihimili mitatu: Bunge, serikali na mahakama. Lakini Lowassa alisababisha kuzaliwa kwa mihimili mitatu ndani ya mhimili wa bunge:
  • Wa kwanza ni Spika Samwel Sitta
  • Wa pili ni Wabunge mitume wakiongozwa na Mwakyembe
  • Mhimili wa 3 ulikua Edward Lowasa mwenyewe.
Hakika Bunge la 9 halitasahaulika kwa WEMA na UBAYA wake.

2. Alikuwa mtetezi asiye na mtetezi. Alikitetea chama chake, kikamtelekeza. Alimtetea Rais wake akamsaliti. Aliitetea nchi lakini nchi ikawatetea watesi wake.

3. Aliwapenda Wamasai, lakini Watesi wake wakamchonganisha na Wamasai. Wakahoji umasai wake na kudai Lowassa ni Mmeru. Lakini upendo wake kwa Wamasai ukawa na nguvu kuliko fitina za watesi wake. Akiwa hai na akiwa maiti Edward amebaki kuwa Mmasai.

4. Alisalitiwa na wengi aliowasaidia. Baada ya kumtumia kwa maslahi yao na kumtelekeza alibaki na Regina. Tujifunze kujali familia zetu. Mwisho wa yote, mzigo unabebwa na familia. Mambo ya “Pengo halitazibika” ni ulaghai mtupu. Kufa uone watakavyoziba pengo hata kabla ya mazishi.

LOWASSA KATIKA UBINADAMU WAKE:
A. Aliwaamini watu kuliko walivyomuamini.

B. Aliuchukia umaskini kwa vitendo. Watesi wake wakatumia hoja hii kumchonganisha na wananchi maskini. Wakasahau kuwa hata maskini wanauchukia umaskini wao na wanatamani kutoka.

C. Aliamini uzalendo si umaskini. Unaweza kuwa tajiri na ukawa mzalendo.

D. Alitumikia vyama 2 vikubwa. Vikamchafua na kumsafisha. Vikambeza na kumtukuza. Ameondoka akiwa mshindi kwa vyama vyote viwili.

E. Ameishi duniani miaka 70. Lakini Historia yake ni ndefu kuliko miaka yake. Ni mfupi wa umri lakini mrefu wa historia. Nenda Edward. Pole kwa Mama Regina, Watoto na wajukuu.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back to Big Edo,
Nimesoma andiko la familia. Kijana aliyeandika ameandika kwa utulivu sana na weledi wa hali ya juu. Amejua kuchagua maneno ya kutumia, zaidi sana ametunia maneno mepesi kwa weledi.
Ktk picha, nimeona kumbukumbu ya Big Edo na viongozi wengi wakiwemo marais wa Tz: Mwalimu, Rukhsa, Ben, Jiwe na mama…kwa bahati…sijaona mzee wa Msoga. Kama na nyie mmeona kama mimi, naamin huo nao ni ujumbe.
Kuhusu rambirambi bila shaka aliyecompile alifanya sampling, napenda kuamini kuwa alitumia random sampling…otherwise ninaona tena bwana yule wa Msoga zake hazipo pale. Hata hivyo ni wengi walitoa salam zisingeweza kuandikwa zote[emoji848]
Rambirambi za Bashe, Rostam na Mwandosya na kaka Haikaeli nadhani ziko ‘natural’ sana.
Binafsi kutoka kwa Big Edo nachukua mambo 2:
1. Maamuzi magumu…
2. ⁠Uzalendo si umasikini…
 
ni mwanasiasa fisadi na mwizi ambae hajawahi kutokea katika Tanzania. Alitawaliwa na uchu wa madaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…