Edward Snowden – Mwanateknolojia aliyevujisha siri za usalama wa Marekani na kuwa mhifadhiwa wa Urusi

Edward Snowden – Mwanateknolojia aliyevujisha siri za usalama wa Marekani na kuwa mhifadhiwa wa Urusi

Mamlukii

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
1,063
Reaction score
2,387
Unaweza kufikiria mtu mmoja aliwezaje kufichua siri kubwa za kijasusi za serikali yenye nguvu zaidi duniani?

Huyu ni Edward Snowden alithubutu na aliweka maisha yake rehani ili kufichua mpango wa siri wa ufuatiliaji wa kimataifa unaotishia faragha ya watu wote.

Aligeukaje kutoka kwa mfanyakazi wa NSA hadi kuwa mhalifu wa kimataifa aliyepewa hifadhi nchini Urusi
Edward Snowden alizaliwa Juni 21, 1983, North Carolina.

Alikua na kipaji kikubwa cha teknolojia, na hatimaye akajiunga na mashirika ya kijasusi ya CIA na NSA kama mtaalamu wa usalama wa mitandao.

Snowden alihusika kwenye miradi ya siri ya kijasusi. Akiwa NSA, aligundua programu ya PRISM, mpango wa serikali wa kufuatilia mawasiliano ya raia bila idhini.
Serikali ya Marekani kupitia PRISM ilikuwa ikikusanya taarifa binafsi za raia kama simu, barua pepe, na ujumbe wa maandishi kupitia makampuni kama Google na Facebook, kinyume na haki za faragha za watu.

Snowden aliona ni muhimu kuanika ukweli huu, akiamini serikali ilikuwa inavunja haki za msingi za faragha za watu. Mwaka 2013, alivujisha nyaraka za siri kwa vyombo vya habari.

The Guardian na The Washington Post walichapisha taarifa hizo, zikisababisha mlipuko wa kimataifa. Siri za kijasusi za Marekani na Uingereza zilifichuliwa, ikiwemo ufuatiliaji wa viongozi kama Kansela Angela Merkel.
. Mara tu baada ya kuvujisha taarifa hizo, Snowden alikimbilia Hong Kong, akijua kuwa Marekani ingejaribu kumkamata mara moja.

Baada ya kufika Hong Kong na kufichua taarifa hizo kwa vyombo vya habari, Edward Snowden alijikuta akiwa kwenye hatari kubwa ya kukamatwa na kurejeshwa Marekani.

Serikali ya Marekani ilitoa waranti ya kukamatwa kwake kwa makosa ya ujasusi, wizi wa nyaraka za serikali, na kufichua taarifa za siri.

Hii ilifanya maisha ya Snowden huko Hong Kong kuwa magumu zaidi, na alihitaji kutafuta njia ya kujificha zaidi. Akiwa Hong Kong, Snowden alianza kuwasiliana na mawakili na mashirika ya haki za binadamu ili kuomba msaada.

Aliomba hifadhi kwa nchi kadhaa, ikiwa ni pamoja na Ecuador, Iceland, na Bolivia, lakini hakuna nchi iliyokuwa tayari kumtoa ulinzi wa moja kwa moja kwa haraka

Mnamo Juni 23, 2013, Snowden alifanikiwa kuondoka Hong Kong kuelekea Moscow, Urusi, kwa ndege ya Aeroflot, akiwa na msaada wa timu ya Wikileaks.

Sababu ya kuondoka Hong Kong ilikuwa kwa sababu serikali ya Hong Kong ilikuwa inakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa Marekani kumkamata Snowden.

Ilisemekana kwamba serikali ya Hong Kong ilichelewesha mchakato wa kumkamata ili kumpa muda wa kuondoka
Urusi ilicheza kwa uangalifu kwenye suala hili. Rais Putin alisema wazi kuwa, ili Snowden apewe hifadhi ya muda nchini Urusi, ni lazima aache kufichua taarifa za siri zinazoweza kuathiri masuala ya usalama wa kimataifa, hasa yale yanayohusu Marekani.

Snowden alikubaliana na masharti haya, na mnamo Agosti 1, 2013, serikali ya Urusi ilimpa hifadhi ya muda wa mwaka mmoja.

Hifadhi hii ilimwezesha kuishi Urusi kihalali bila hofu ya kukamatwa au kuhamishwa.

Baadae URUSI iliamua kumpa Uraia
Marekani ilimfungulia mashtaka ya ujasusi na usaliti. Snowden alitajwa kama msaliti na mhalifu wa usalama wa taifa, huku wengine wakiamini yeye ni shujaa wa uhuru na faragha.

Kitendo chake kilianzisha mjadala mkubwa kuhusu usalama wa taifa vs faragha ya watu binafsi, huku sheria mpya zikipitishwa kudhibiti jinsi serikali zinavyokusanya na kutumia taarifa za raia.

Snowden, hadi sasa, anaishi uhamishoni nchini Urusi, akiendelea kuzungumza juu ya haki za kidijitali, huku serikali ya Marekani ikimwona kama mhalifu hatari.
IMG_2810.jpeg
IMG_2811.jpeg
IMG_2812.jpeg

IMG_2807.jpeg
IMG_2809.jpeg
 
Kwa hiyo Russia ina enjoy kuwepo kwake huko.
Ina maana siri ya US ziko nje nje kwa Russia.
 
Kuna biography yake kaigiza joseph gordon levitt iko poa sana.
 
Back
Top Bottom