Edward Teach (Blackbeard), Mwamba aliyekua anaokoa watumwa baharini ili wafanye kazi za wizi wa Meli (Pirates)

Arnold Kalikawe

Senior Member
Joined
Sep 28, 2016
Posts
152
Reaction score
374
Baharini kuna mali nyingi sana sema tu inakuwa ngumu sana kuzifikia. Kuna stori ya jamaa mmoja aitwaye Edward Teach ama Blackbeard kama alivyokuwa akijulikana.

Mchizi huyu alizaliwa mwaka 1680 na kufariki 1718. Kwa miaka hiyo huyu jamaa ndiye aliyekuwa akiongoza kwa kufanya wizi mkubwa humo baharini. Alikuwa ni haramia aliyekuwa na meli yake, yaani kazi yake kubwa ilikuwa ni kuja na kufanya wizi kwenye meli yenu na kuondoka na mali zenu.

Jamaa alisumbua kwa kipindi kirefu, alitafutwa kila kona, kumpata halikuwa jambo la kawaida kwani naye alikuwa mjanja na mwenye mbinu nyingi za kupambana na polisi.

Huyu ndiye pirate maarufu kuliko wote duniani mpaka sasa hivi. Meli yake ilikuwa na dhababu, almasi nyingi kuliko hata meli nyingine. Mchizi alifanya biashara kubwa iliyomuingizia pesa nzuri tu.

Wakati nyie mnakamata watumwa kwenda kuwatumikisha, mchizi alikuwa anateka meli zenu, akawaokoa watumwa na kuanza kufanya nao kazi za wizi baharini jambo lililowakasirisha watu wengi na kuanza kumtafuta.

Kuhusu kifo chake ni kwamba alikuwa akipigana na Waingereza wakiongozwa na Maynard huko Ocracoke. Vita vilikwenda vizuri mpaka wakaona sasa walishinda. Wakateremka na kwenda kwenye hiyo meli, hawakujua kama kulikuwa na wengine waliokuwa wamejificha, wakawahiwa na kuuawa, yeye alipigwa risasi tano na kufariki dunia.

Meli yake ikapotea na kwenda kuzama ikiwa na mzigo mkubwa wa dhahabu na almasi. Watu waliitafuta na kuitafuta lakini hawakufanikiwa kuiona. Mpaka leo hii, kila mtu anatamani kuipata meli hiyo, wanajua ina mali nyingi, tatizo ni moja tu, ilizamia mahali gani? Ugumu unaanzia hapo.

Ukitazama muvi za Pirate of Carribeans utamuona.

Screenshot_20240526-173155_1.jpg
 
View attachment 3000083
Sawa
 
Nilijua tu mwisho wa stor watasema meli ilizama na mali na wahijulikani ilipozama
 
Back
Top Bottom