Eee Mungu......

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2011
Posts
3,988
Reaction score
1,308
Rabbi uloumba mbingu, Ukaumba na dunia
Nasi kwetu walimwengu, Dini ukatushushia
Nini letu fungu, Sisi ulotuwekea



Kutwa kucha twakuasi, Maovi kuyavamia
Tena bila ya kuasi, Mengi tunakusudia
Mola haiwi basi, Waja kwako twarejea



Muombozi wetu nani, Kwayo tunokutendea
Ya Illahi ya Manani, Wapi tutakimbilia
Tutaingia motoni, Kama hujatupokea



Twakuomba Rahmani, Waja wako twatubia
Tunataka samahani, Kila tulokutendea
Sisi sote duniani, Na waliyotangulia
 
Ndiye weye peke yako, Mwengine hapatikani
Twataka shifaa yako, Akhera na duniani.
Kama si rehema zako, sisi sote mashakani.
 
sisi sote mashakani, bila ya rehema yako
hatokei duniani, wa juu zaidi yako
wote insi na majini, wote ni viumbe wako
tusamehe waumini, tuipate pepo yako

tuipate pepo yako, tusamehe waumini
tupe na rehema zako, akhera na duniani
na kila lo zuri kwako, kwetu wala situkhini
sisi sote waja wako, tusamehe ya Mannani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…