Eeehh Mwenyezi Mungu niepushe na Mali Nyingi!!!!

chiko

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2010
Posts
590
Reaction score
271
Ndugu wanajamvi, napenda kuwashindikiza kwenye wikiendi na maombi ninayo oomba kila kuchao!!!!"Ewe Mwenyezi Mungu niepushe na Mali nyingi", kwanini nasema hivi, kwa sasa kipato changu nashkuru si cha juu na sio chini, napata mahitaji yangu na familia, lakini kwa muelekeo ni navyoona kwenye maisha ya kileo, mali ndo ina poromosha maisha mengi ya Binadamu haswa waume kwa familia zao. Visa ni vingi sana, kina Tiger Woods, Michael Jordan, hivi karibuni Swarzenneger na wengine wengi ambao kama wangekuwa watu wa kawaida hawangepata shida nyingi.

Nina maanisha, Kipato kikiwa kingi, mtu hujisahau, na hata kumdhihaki maulana, ndio humwambia shemegi yenu pia aniombee sana niendelee na hivi nilivyo, kwani nikitajirika, majaribio ni mengi na kujificha itakua vigumu!!!!

JIM BACKUS " Many a man owes his success to his First wife, His second Wife to his Success", Weekend Njema Jamani!!!!!!
 
Safi ujumbe mzuri na weekend njema kwako pia.
 
mhh lakini pesa hazibadilishi tabia ya mtu bali zinamagnify tabia zake...., kwahiyo ukiwa mtu wa tabia fulani hata ukiwa masikini utakuwa na hizo tabia tu...., ni kwamba haujapata opportunity...., naona bora ubadilishe sara ili upate pesa ili uweze kubadilisha maisha ya watu kwa kuwasaidia na kutoa misaada..... au unasemaje?
 

mkuu umeingia cha kike...Hivi ni nani wanaocheat zaidi ya maskini? nani wana wake wengi zaidi ya mskini kwetu Tanzania? hao mselebu kila kona wanamulikwa ndo maana unaona hivyo eti kazaa katoto kamoja tu nje hilo ndo unaogopa? babu yako alikuwa na watoto wa ngapi wa nje? Jibu unallo mwenyewe then think twice...
 
Tatizo sio pesa tatizo ni watu!
 
duuuhhh
sawa mkuu
mimi niko kinyuma kabisa na maneno yako
 

Magulumangu kaongea..
and I'm out...
 
Aisee mungu akujalie maombi yako.....ila miye namwomba anilimbikizie mali ya kufa mtu
 
sawa mkuu yote maisha cha msingi omba furaha amani hekima na busara katika maisha na hizo ndo silaha za kuyakabili maisha.
 
Aisee mungu akujalie maombi yako.....ila miye namwomba anilimbikizie mali ya kufa mtu

AMINA, Dr. mie nakuombea pia ujazo wa mali ya kufa mtu, isije ukawakimbia watakavyo kufuata kwa malundo, alafu mungu akichukua chake, watoto waonyeshwa watu....mtoto wa DR huyu...!!!!
 

Magulumangu; Mimi nilikuwa namaanisha karne ya sasa hivi, Ukiwa maskini, hata kutongoza utakataliwa, lakini ukiwa nacho, wewe hutongozi, bali utakuwa wawinjwa hasa, kila kona ukipita watu wataka mbegu zakoooo!!!!!!!!!
 
mimi naomba nipate mali nyingi maana Suleimani alikuwa tajiri lakini alitii Mungu na Ayubu alikuwa tajili alimpendeza Mungu ila kubwa zaidi omba HEKIMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…