EFD Machines: Ndg Wananchi.... sina hakika kama kweli sisi ndiyo wenyenchi!

EFD Machines: Ndg Wananchi.... sina hakika kama kweli sisi ndiyo wenyenchi!

josam

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Posts
2,252
Reaction score
1,041
Hakuna kitu kinaniuma kama kupata kwa jasho kali (Serikali kukamua walipa kodi) na kisha kutumia kwa DEZO?????????!!!!!!!! Mfanyakazi wa sekta binafsi na umma hususani mwalimu na baadhi ya idara serikalini, anatokwa na jasho kupata huo mkate na kodi inasombwa kwa manufaa ya KIFISADI!!!?? Hivi tukiachilia mbali watumishi wa TRA au vigogo, Sheria ya Kodi kw maana ya PAYE ina-apply kwa Mshahara wa Mbunge??!!!!! Mapato yake yote ikiwa ni pamoja na mshahara, posho, mafuta, chochote ambacho ni stahiki ya mbunge kama ilivyo kwa mfanyakazi wa sekta binafsi au Umma, kinakatwa kodi????????!!! Je, kwa vile Mbunge anapata mapato makubwa kuliko hata machinga anayetakiwa kufungiwa machine, Serikali haioni umuhimu mkubwa sana kwa Mbunge kufungiwa machine hii/ kutoa malupu lupu ya Mbunge yasiyokatwa kodi au kuingizwa kwenye fomula ya PAYE?!!? Assume: Total income Tshs.12, 000, 000/=Deductions: NSSF?? = 1,200,000 PAYE: 3,129,700Take home: 7,670,300 Waheshimiwa, hiki ndicho kiasi mnacho chukua???!


Hapa kuna Issue zaidi ya mbili hivi


  1. Elimu kwa umma - hiki siyo kigezo sana japo elimu haikutolewa ipasavyo isipokuwa kama ilivyo kawaida serikali kutopenda kushirikisha wadau kwa mapana. Serikali inapenda sana usiri. Mambo mengine hayahitaji usiri kiasi kile serikalini kwa umma na ndiyo maana issue nyingi zinagomewa na wananchi kwa madai kwamba hawakushirikishwa na serikali haijifunzi wala siyo sikivu kwani haya yanatokea kila mara na hakuna mabadiliko. Mambo yanawahusu wananchi na ni kwa masilahi yao, kwa nini wafichwe?
  2. Gharama ya kufungiwa machine hii ya kukusanya taarifa za mlipa kodi, hapa ndipo kuna tatizo kubwa na maswali mengi yanayopelekea kile kinachoitwa USIRI SERIKALINI!
Sina wala sioni tatizo kwa kila mfanyabiashara kulipa KODI, LAKINI?


    1. Kati ya Serikali na Mfanyabiashara nani anapata hasara zaidi kwa kutokungwa kifaa hiki? Jibu lahisi litakuwa SERIKALI. Kama hivyo ndivyo, swali la pili linakuwa….
    2. Kwa nini mfanyabiashara alipie gharama za manunuzi / kufunga ifaa hicho? Kwa nini gharama hizi zisigharimiwe na serikali?

USHAURI:

    1. Serikali inunue na ifunge kifaa hiki kwa kila mwenye anwani na lesseni ya kufanya biashara. Ikifanya hivyo nina imani 100% Serikali itajua lengo halisi la (lililo nyuma ya) kulalamikiwa mashine hizi.
    2. Serikali iweke ulazima wa kila mfanyabiashara kutumia mashine hizo katika kila mauzo yanayofanyika kila siku.
    3. Serikali iweke adhabu kali na ifuatilie (kwa uwazi kuepuka vishoka wapenda mitelemko/rushwa) kila mfanyabiashara kufanya maingizo / manunuzi kupitia mashine hiyo.

Nini tafsiri juu ya Serikali isipo ingia gharama za kununua mashine hizi?


  1. Serikali haitajua lengo mahususi la wananchi kupinga kununua na kufunga mashine hizi
  2. Wananchi wataendelea kuamini (kwani wanahisi hivyo) kuwa eidha serikali yenyewe inataka kujinufaisha kupitia mgogo wa mashine hizi kwa kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara na manunuzi ya mashine hizi. Mpango wa wenye meno serikalini na wafanyabiashara/watengenezaji wa mashine hizo.
  3. Serikali siyo sikivu na siyo shirikishi kwani huu ni uonevu kuliko hata wa kikoloni. Hakuna usawa na haki.
  4. Itaacha maswali mengi yasiyo na majibu kwamba ni rahisi n si ghari kifaa hiki kinunuliwe na mwananchi/ machinga kuliko serikali? Kwamba serikali haina uwezo wa kununua kifaa hiki kwa kila mfanya biashara? Je, serikali inakusanya fedha kiasi kidogo (yaani chini ya gharama ya kununua kifaa hicho) kutoka kwa hao wafanya biashara hivyo ikimnunulia kifaa hicho itakuwa imepata hasara? Kwamba serikali ikinunua itakuwa imetumia vibaya fedha ya mkulima mlipa kodi?,nk…nk..nk…nk?

Ikumbukwe kuwa kupunguza gharama za kununua na kufunga kifaa hiki hakutasaidia au kupunguza kero za kurupushani za matumizi ya mashine husika, kifaa hiki kinapalilia RUSHWA kwa watumishi wa serikali (ni wote sikusahau kusema wasio waaminifu) na wafanyabiashara hivyo malengo ya serikali hayatafanikiwa kama ilivyokusudiwa (kama kweli serikali itakuwa wazi bila udanganyifu wa kupika takwimu kama BRN). Ukwepaji wa kulipa kodi utakuwa pale pale na utazidi lakini kubwa zaidi ni kupanuka kwa mirija ya kuomba rushwa kwa maafisa wa TRA au Vs.
Serikali Tafakari na Fanya Maamuzi Magumu, serikali isipende mteremko kwa kila jambo!
 
Naona unaipigia debe NSSF waombe wakulipe... kwenye mada kama hizi dokezea tu mfuko wa mafao na sio kutaja shirika yapo mashirika zaidi na ni hiari ya mtu kuchagua mfuko wa kulipia
 
18pecent walipe wananchi lakini wawekezaji walipe 3pecent, hii ni serikali ya aina gani?na kwa hesabu ya haraka sasa kodi zinavokua kubwa kila mahali kwa siku kila mtu ambaye anatumia wastan wa sh.5000 kwa siku serikal inachukua kod ya 1200
 
Back
Top Bottom