Egypt

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
351
Reaction score
887

Na, Comred Mbwana Allyamtu.

Sunday 10/9/2017.
Misri (Kwa Kiarabu: مصر, Masr) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki ikiwa na eneo la Rasi ya Sinai kwenye bara la Asia pia. Ni nchi yenye wakazi milioni 90 na mji mkuu Kairo ni kati ya miji mikubwa zaidi duniani. Ni kati ya nchi za dunia zenye historia ndefu inayojulikana.

Asili la jina MISIR nikutokana na maana ya jina lenyewe kimsingi Jina la Misri kwa Kiswahili linafanana na jina rasmi la kiarabu (مصر Miṣr katika lugha ya Kiarabu.) kwa mantiki hiyo Misir Ni jina la Kale jinsi inavyoonekana katika Biblia ya Kiebrania ambako huku huonekana ilikuwa ikiitwa “Mitzrayim’’ (מִצְרַיִם, dola ya Misri humaanisha Misri ya Juu na Misri ya Chini). Maana ya jina hili ni "nchi".

Katika enzi ya Misri ya Kale nchi hiyo iliitwa na wenyeji Km.t (Kemet) inayomaaniosha "nchi nyeusi" kwa kutaja ardhi "nyeusi" (=yenye rutuba) ya bonde la Naili ambayo watu weusi walikuwa wakiishi, tofauti na ardhi nyekundu ya jangwa, na kwa mantiki hii ndio maana wanahistoria huamini kuwa dola ya Misir ilikuwa ikikaliwa na watu weusi toka miaka 8000 BC huko nyuma na kuifanya misiri kuwa ni moja ya maeneo ya kale kabisa duniani kustaarabika…..( hilo tutaliona huko mbele katika uchambuzi wangu wa kile kinachoitwa “chimbuko la ustaarabu duniani ni Afrika”. Majina ya Kizungu ya "Egypt" (ing.), "Egypte" (Far.), "Ägypten" (Jer.) yanatokana na jina la Kigiriki Αίγυπτος (aigyptos). Hakuna hakika juu ya maana asilia ya neno. Wengine huamini neno limetokana na jina la hekalu muhimu mjini Memphis. Neno hili pia kwa asili ya jina "Wakopti" ambao pia ni sehemu ya wenyeji wa Misri walivyojiita wakati wa utawala wa Dola la Roma

JIOGRAPHIA YA MISIRI
Misri imepakana na Bahari ya Mediteranea kwa kaskazini, Israel na Eneo la mamlaka ya Palestina kwa kaskazini mashaliki, ghuba ya Suez, ghuba ya Aqaba, Bahari ya Shamu kwa mashaliki, Sudan kwa kusini na Libya kwa magaharibi. Umbo la nchi ya Misir hufanana na trapeza. Tabia nchi ni yabisi sana na maeneo makubwa ni jangwa, pamoja na oasisi na maeneo ya savana ya miiba. Karibu asilimia 79 ya wananchi wote huishi ndani ya ukanda mwembamba wa bonde la mto Naili. Bonde hili linavuka nchi kuanzia mpakani na Sudani katika kusini kuelekea kaskazini hadi mdomo wa mto (Derta) kwenye Bahari ya Mediteranea. Ardhi pande zote mbili za mto inamwagiliwa na kulimwa. Kwatika umbali mdogo kutoka mto jangwa inaanza na kutapakaa karibu seheemu kubwa ya nchi.

Takriban kilomita 250 kabla ya mdomo Naili inagawanyika katika mikono mbalimbali na kuunda delta ya mto. Kanda hili ni mbichi si zaidi ya asilimia 5 za eneo lote la nchi, ila 98% za wananchi wote huishi humo. Kwa hiyo na kwa msingi huu Naili huitwa "Baba wa Misri", kwa maana bila mto huo pasingekuwepo taifa hili. Mji mkuu wake ni Kairo (Cairo) uko mwanzoni mwa eneo la delta.

TAIFA HILO LIMEGAWANYWA KATIKA KANDA ZIFUATAZO:
Oasisi ya mto Naili: - Mto umechimba bonde kama mfereji katika mwamba asilia ya nchi. Ndani ya bonde hili jembamba lenye upana hadi kilomita 25 kuna kanda la ardhi yenye rutuba kuanzia Ziwa Nasser hadi Kairo.
Delta ya Naili:- Upande wa kaskazini wa Kairo Naili inajigawa katika mikono miwili mikuu na kati ya mikono hiyo miwili kuna eneo la delta yenye km² 23,000 kwa umbo la pembetatu. Inajaa ardhi ya rutuba kutokana na matope ya Naili iliyopelekwa huko na mafuriko katika muda wa miaka elfu kadhaa. Eneo hili linalimwa kote na kumwagiliwa likiwa na mikono midogo ya kando ya Naili.

Jangwa la Magharibi: - Ni eneo kubwa upande wa magharibi wa Naili lisilo na milima mikubwa. Kaskazini mwake kuna tambarare ya Lybia iliyo takriban mita 240 juu ya uwiano wa bahari. Kusini mwake linainama eneo la mbonyeo wa Qatara hadi mita 133 chini ya UB, halafu jangwa linapanda tena juu kuelekea kusini magharibi. Ndani ya eneo hili kubwa kuna beseni kadhaa pamoja na oasisi za Siwa, Bahariyya, Farafra, Dakhla na Charga. Kilomita 100 upande wa kusini-magharibi wa Kairo kuna oasisi kubwa ya Fayyum pamoja na ziwa la Warun lenye eneo la km² 230.

Jangwa la Mashariki:- Ni eneo upande wa mashariki wa mto Naili. Huko kuna milima inayopanda juu ya mita 2,000 pamoja na wadi yaani bonde kali. Jangwa linatelemka hadi mfereji wa Bahari ya Shamu ambao ni sehemu ya Bonde la Ufa linaloanza Palestina na kuendelea hadi Ziwa Nyasa.

Rasi ya Sinai: - Ni eneo la jangwa na milima inayofikia hadi mita 2637 (Jabal Katharina).

HISTORIA YA MISIR/EGYPT (KEMETI)
Nchi hiyo ni kati ya vitovu vya ustaarabu wa binadamu, na kwa sababu hiyo inavutia watalii wengi. Historia ya awali ya taifa hilo ni Katika kipindi cha historia ya awali tangu takriban miaka 6000 BC wakazi wa Misri walikuwa na kilimo cha nafaka. Walikuwa na teknolojia ya Zama za Mawe. Wakati ule Jangwa la Sahara lilipanuka na kuwalazimisha watu kukaa karibu zaidi kwenye mto Nile na kwenye oasisi kama Faiyum. Katika mazingira ya jangwa bonde la Nile liliwavuta watu kutokana na rutuba kubwa ya ardhi iliyoongezwa kila mwaka upya kwa njia ya mafuriko yaliyotandaza matope kutoka nyanda za juu kwenye ardhi.

Utafiti wa akiolojia umegundua ya kwamba wakazi hao wa bonde walianzisha tamaduni mbalimbali zilizokuwa tofauti kati yao lakini zilizowasiliana kibiashara. Mifano ya kwanza ya mwandiko wa hiroglifi imepatikana kwenye vyungu vilivyofinyangwa mnamo 3200 BC.

Misri ya Kale Katika karne zilizofuata, mnamo 3000 BC yalitokea muungano wa sehemu mbalimbali wa Misri chini ya wafalme wenye nguvu wanaotajwa kwa cheo cha Farao. Katika historia iliyotungwa na waandishi Wagiriki wa Kale ni kwa Kwamba Farao Menes (Meniphis/Niamer) anayetajwa kuwa mtawala wa kwanza na mwasisi wa dola hiyo kubwa kabisa aliyeunganisha Misri ya Kaskazini na Misri ya Kusini kuwa milki moja na mpaka kufikia kuwa himaya kubwa sana duniani. Lakini hata hivyo inajulikana kuna wafalme waliomtangulia waliokuwa tayari na milki kubwa katika zile zilizo kuwa Misir ya kusini na kaskazini. Hata hivyo Pharaoh Menes (meniphis) alianzisha utawala wa nasaba mbalimbali zilizofuatana, pamoja na vipindi vya kati ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe na mafarakano katika nasaba ziliweza kugawa nchi tena kwa muda.

Mafarao wa Misri ya Kale walifaulu mara kadhaa kupanua mamlaka yao hadi ndani ya Sudani ya leo, na pia juu ya sehemu za Palestina na Syria ya leo. Mara kadhaa wavamizi kutoka nje walifaulu kushika utawala juu ya Misri kama vile Wahyksos kutoka Palestina / Kanaan, Wakushi kutoka Nubia au watu kutoka Lybia (Libya na Tunisia ya leo). Wavamizi hao walitumia pia cheo cha Farao wakijaribu kuendeleza tabia nyingi za milki za awali. Hatimaye wote walipinduliwa tena na viongozi wazalendo walioanzisha nasaba mpya. Hata hivyo Mwaka 525 BC mfalme wa Uajemi aliteka Misri wakati amabpo Uajemi ilipo kuwa himaya kubwa katika dunia. Kwa kipindi kifupi Wamisri waliweza kuwaondoa tena na kuendelea chini ya watawala wazalendo. Hata hivyo baadae ilivamiwa na kuwa chini ya Rome amabayo wakati huo ilifahamika kama Misri ya “Ptolemi (Wagiriki)” na chini ya Roma


MISIR /EGYPT (KEMETI) YA PTOLEMY (WAGILIKI) NA CHINI YA ROMA
Uvamizi wa Aleksander Mkuu mwaka 332 BC ulianzisha kipindi cha Misri ya Kigiriki. Mji mpya wa Aleksandria ulikuwa mji mkuu mpya. Jemadari wa Wagiriki walitumia pia cheo cha Farao na kutawala kama nasaba ya Ptolemi, lakini tabaka ya watawala ilikuwa na utamaduni tofauti sana na wananchi wakulima wa kawaida. Wakati wafalme Wagiriki waliendelea kutawala milki mpya ilienea kutoka magharibi ya Mediteranea iliyokuwa Dola Ya Roma. Malkia wa mwisho wa Misri alikuwa Kleopatra. Baada ya kifo chake Misri ilikuwa jimbo la Dola la Roma (hicho ni kipindi cha himaya ya Roma).

Utawala wa Kiroma uliendelea kwa karne 6. Katika muda huu Ukristo ulianza kuenea katika Misri. Nchi ilikuwa haraka kitovu muhimu cha imani mpya ya Ukristo wa Kikopti (Coptic) uliendelea kwa kasi na mapokeo ya pekee na kupeleka mfumo huu wa Ukristo wa kikopti kufika hadi Sudani na Ethiopia. Lakini hali ilikuwa ngumu baada ya magavana wa Roma na baadaye wa Bizanti kujaribu kuwalazimisha Wakopti kufuata misingi na mafundisho ya Kanisa rasmi yaani Kanisa la Kiorthodoksi.

UVAMIZI WA DOLA LA KIARABU NCHINI MISIR NA KUINGIA KWA DINI YA UISLAM MISIR
Kwenye mwaka 639 AD jeshi la Waarabu Waislamu lilivamia Misri na kuteka nchi yote katika muda wa miaka 3. Wenyeji wengi waliokuwa Wakristo Wakopti hawakuwapinga kwa sababu walipendelea Waislamu kuliko Wakristo Waorthodoksi waliowahi kuwakandamiza vikali katika miaka iliyotangulia. Kwa karne kadhaa idadi kubwa bado walikuwa Wakristo lakini kuanzia karne ya 12 idadi ya Waislamu ilikuwa kubwa zaidi kwa sababu Wakristo walipaswa kulipa kodi zaidi na vipindi kadhaa vya mateso vilitokea na yote ilisababisha kuhamia kwa wananchi kwenda dini mpya. Watawala wapya hawakutumia Mji wa Aleksandria kuwa mji mkuu bali walianzisha mji mpya wa Fustat karibu na Babylon ya Misri pale ambako mto Nile unajigawa na kuanzisha delta yake.

Hadi mwaka 969 AD Misri ilitawaliwa na watawala wa Waislamu Wasunni waliokuwa kwa majina ya magavana na wawakilishi wa makhalifa huko Dameski au Baghdad, lakini zaidi watawala hao walikuwa wakijitegemea katika hali halisi. Mwaka 969 AD Wafatimi (sehemu ya dhehebu la Shia) kutoka sehemu za Tunisia ya leo walivamia na kuteka nchi wakianzisha ukhalifa wao. Wafatimi walikuwa Waismaili, wakati ule mwelekeo wa kimapinduzi ya kiShia. Walianzisha makao makuu yao nje ya Fustat na Babylon wakaiita "Al-Qahira", yaani (mwenye ushindi,) na hii ndio ilikuwa chanzo cha Kairo ya leo. Wakati wa vita za misalaba ( cross War) Wafatimi walishindwa na askari wa Kisunni waliendelea kuunda nasaba ya utawala wa masultani wa Mamluki wa Misri.

KUPANUKA KWA MILIKI YA OTHUMANI (HIMAYA YA OSMANI) NA MISIR KUWA JIMBO LA OSMANI
Hatimaye misir ilikangukia katika Jimbo la Milki ya Osmani Mnamo mwaka 1517 AD, Waosmani walivamia na kuteka Misri. Hadi karne ya 19 Misri ikaendelea kama jimbo la Milki ya Osmani, kisheria hata hadi hapo Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ilipoanza. Hali halisi nchi ilikuwa na kipindi kifupi kama milki ya kujitegemea wakati wa karne ya 19, hadi kusimamiwa na Uingereza hasa kwa shabaha ya kutawala mfereji wa Suez na minajili ya nchi kulindwa. Mwaka 1914 ilitangazwa kuwa nchi lindwa chini ya Uingereza; tangazo la uhuru la mwaka 1922 lilomuweka mfarme Faud madalakani bado halikubadili hali ya mambo na lakini liliacha athira kubwa Kwa Uingereza. Hatimaye mwaka 1952 uhuru kamili ulipatikana na Tangu mwaka 1952 Misri imepata uhuru kamili, na tangu hapo ilitawala pia mfereji wa Suez.

UHURU 1922 NA MAPINDUZI YA KIZALENDO YA MWAKA 1952
Uingereza ilitangaza kuipatia uhuru mwaka 1922 ikiwa ni pamoja na kumuweka mfarme Faud madalakanihuku Saad Zaghul akiwa wazili mkuu wa taifa hilo huru, kimsingi uhuru huo ulitambulika kama uhuru bandia na kupelekea kuibuka vuguvugu la mapinduzi jeshini

Fikra za makamanda wa kijeshi walimuondosha madalakani mfarime farouk aliyeitawala misir kwa mkono wa chuma baada ya kulithi kiti cha ufalme kutoka kwa baba yake alifariki na kulithi kiti hicho. mwanamapinduzi Gamal Abdel Nasser ndie aliye endesha mapambano ya mapinduzi ya halakati ya kumuondoa madalakani mfarme Farouk na kufanikisha harakati hizo za mapinduzi mwaka 1952 kundi hili liloongoza mapinduzi lili itwa Cadeti 3 ambalo liliwajumuisha maofisa vijana. Vijana hao ambao tayali walikuwa tayali wameanza kuvutiwa na vuguvugu la kisiasa la afrika pamoja kwamba vijana hao walikuwa wameshibana na madola ya kiarabu lakini walijisogeza zaidi na mitazamo ya kiafrika iliyoangazia siasa za afrika( Pan Africanism).

Lieutenant General muhamad Naguib ambaye aliteuliwa kuwa raisi na kuwa kiongozi wa taifa jipya la misir huku Gamal Abdel Nasser kuwa makamu wake na Saadat kupewa wizara muhimu. Hata hivyo Naguib baadae serekali yake ilikabiliwa na mawibi na kashikashi za kisiasa yeye mweneyewe aliamua kuachi ngazi na nafasi yake kuchukuliwa na Gamal. Hata hivyo utawala wa Gamal ulikabiliwa na mapingamizi mengi kutoka nchi za maghalibi ambazo ziliitumia taifa la Israel kuidhofisha misir Gamal mwenyewe alitaka kupinduliwa katika jaribio lilotaka kumuua ambalo jalibio hilo lililatibiwa na kikundi cha MUSLIM BROTHERHOOD (undugu wa kiislam) hatua iliopelekea serekali yake kuifuta na kukipiga marufuku kikundi hicho na kumuweka kizuizini raisi wa kwanza wa taifa hilo Mohamad Nguib.

Hatua ya Israel kuvamia eneo la Sinai liliongeza misiguano kati ya mataifa hayo mawili na hatimaye kuzuka vita ya mwaka 1967 na hatimaye kufungua njia ya kifo chake mwaka 1970 baada ya kukumbwa na shambulio la moyo….hata hivyo raisi wa awamu ya tatu Anwar E-lsaadat alitiana saini na taifa la Israel katika makubaliano ya amani jambo lilopokelewa vibaya na mataifa ya kiarabu hali iliyopelekea misiri kufutwa uanachama wa jumuia ya Arab legue.

Hata hivyo jambo hilo la mkataba wa amani baina ya misir na Israel haukuwafurahisha pia waislamu wa ndani ya nchi hasa wale wenye msimamo mkali… hivyo hilo lilifanikisha mauaji dhidi yake mwaka 1981 pale ambapo tarehe 6/10/1981 alipo kuwa anakagua gwaride alipo uwawa kwa kupigwa risasi mara baada ya kifo chake Housi Mubarack alichukua nchi ikumbukwe kuwa Mubaraka ambaye alikuwa makamu wake pamoja na mambo mengine utawala wake Mubaraka ulilalamikiwa kuwa wa kiimla na hatimaye pakaibuka vuguvugu la kialabu liloanza nchini Algeria na kutamatisha utawala wake mara baada ya maanadamano ya umma kutamahalaki pale katika viwanja vya Tahrir Squre yaliyo tamatisha utawala wake Housen Mubalak tarehe ya 18 januari mwaka 2011.

Uchaguzi wa baadae wa juni 2012 ulikipa ushindi chama cha undugu wa kislamu (muslim Brotherhood) na kukilejesha tena katika dira za kisiasa hata hivyo Mohammed Morsi alishinda uchaguzi huo Alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo mwaka 2012,

Mohamed Morsi ni mwanasiasa wa Misri na rais wa tano wa taifa hilo kuanzia Juni/ 30 /2012 hadi Julai/ 3 /2013, alipopinduliwa na mkuu wa majeshi Abdel-Fatah al-Sisi, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. Morsi alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia katika historia ya taifa la Misri. Morsi ni msomi aliefikia ngazi ya PhD na alikuwa mwanachama mwandamizi wa kundi la Udugu wa Kiislamu, akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa tawi la kisiasa la kundi – Chama cha Haki na Uhuru FJP, kilichoundwa na Udugu wa Kiislamu baada ya mapinduzi ya mwaka 2012, baada ya Morsi na wengine kutoroka gerezani. Mursi aligombea urais na kushinda katika kinyanganyiro hicho katika duru ya pili iliyompabanisha na Ahmed Shafik, waziri mkuu wa mwisho wa rais Hosni Mubarak.

lakini aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi dhidi ya utawala wake kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika nchini humo kuupinga utawala wake. Kwa nyakati tofauti Morsi alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ugaidi na bado anakabiliwa na mashitaka mengine pamoja mahakama nchini humo kumfutia adhabu ya kifo.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
.....
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu.

[emoji767] copy rights reseved
[emoji768]written by Comred Mbwana Allyamtu
Sent using Jamii Forums mobile app

Mpendwa nashukuru kwa historia hii. Ila tu nashangaa kwa nini uliandika chini yake madai kuwa wewe uliandika na wewe una hatimiliki juu ya matini hii.

Maana nisipokosei ulisambaza hapa matini inayopatikana katika makala "Misri" ya Wikipedia ya Kiswahili. Ulinakili karibu makala yote neno kwa neno.
Misri - Wikipedia, kamusi elezo huru
Hii si kosa maana kama makala ni nzuri inafaa kusambazwa! Isipokuwa ni kawaida kuonyesha ni wapi tuliponakili.
Ila tu sielewi kwa nini uliweka chini yake "written by Comred Mbwana Allyamtu" ???
 
Wamisri wa zamani walikua wagikiliki sio watu weusi, weusi walikua ethiopia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…