EgyptAir Yamzawadia Kichanga Aliyezaliwa Ndani ya Ndege Ikiwa Safarini Tiketi ya Kusafiria Maisha yake yote (Life-time Travel Ticket)

EgyptAir Yamzawadia Kichanga Aliyezaliwa Ndani ya Ndege Ikiwa Safarini Tiketi ya Kusafiria Maisha yake yote (Life-time Travel Ticket)

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Shirika la Ndege la Egypt,yaani EgyptAir limemzawadia Kichanga aliyezaliwa ndani ya ndege wakati ndege hiyo ikiwa Safarini Tiketi ya maisha.

Mwanamke wa Yemen alishikwa na uChungu ndani ya ndege na kujikuta akijifungua Kwa kusaidiwa na daktari ambae Kwa bahati nzuri alikuwa abiria.

Baada ya wahudumu kupata taarifa hiyo ,rubani alijaribu kushuka Kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Munich Ili kumsaidia mwanamke huyo lakini kabla ndege haijafika Ardhini Mwanamke huyo alijifungua Kichanga hicho humo humo ndani ya ndege.

Screenshot_20240907-195056.jpg

My Take: Tulishafundishwa kwamba sio vizuri kusafiri siku zikikaribia maana purukushani za safari zinaweza kupelekea pre mature birth.

Hongera Kichanga Kwa kupata Tiketi ya maisha kusafiri popote na EgyptAir.
 
Ndio maana mashirika mengi ya ndege hayataki upande ndege kama mimba yako ni kubwa. Ili kuepusha dharura kama hizi.
 
Back
Top Bottom