Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
EID EL FITR: ''BLUE HAWAII'' ELVIS PRESLEY EMPIRE CINEMA 1964
Kuna ndugu yangu hapa kaangalia video ya watoto wa mtaani kwangu Magomeni Mapipa leo asubuhi baada ya sala wamekuja kunipa mkono wa Eid na wakanisomea Qur'an kunifurahisha.
Ndugu yangu huyu akaweka ''comment'' akasema hawa vijana wamenikumbusha Saigon Club.
Nimemjibu kuwa Saigon Club wakati huo ilikuwa bado nikamweleza kuwa hawa masheikh waliokuja kunisalimu hawanikumbusha Saigon Club.
Kwa umri ule walionao wamenikumbusha utoto nina miaka 12.
Hakuna binadamu naamini ambae hatazami nyuma na kuacha kujuta.
Kwa nini haikuwa hivi kwa nini ilikuwa vile?
Ilikuwa siku ya Eid Fitr 1964 asubuhi baada ya chai nimepita theatre zote maarufu kwa michezo tuliyokuwa tunaipenda kuangalia - Cameo, Odeon, Avalon, Chox na Empire.
Kulikuwa na senema za Kirumi wakionyesha filamu za ''Hercules,'' ''Land of Cyclops,'' ''The Colossus of Rhodes,'' picha za ''Cowboy'' kama tulivyopenda kuziita ''Westerns,'' tukimpenda sana Alan Ladd aliyecheza ''Shane'' na tukimuusudu sana John Wayne aliyecheza, ''North to Alaska.''
Huyu Alan Ladd alipata umaarufu kama mwigizaji kwa kuwa alipigania Vita Vya Pili Vya Dunia.
Alan Ladd alicheza picha na Sidney Poitier, ''All The Yong Men,'' kuhusu vita hivyo.
Siku moja nazungumza na Juma Mwapachu ilikuwa siku chache baada ya kifo cha Kleist Sykes mwaka wa 2017.
Siku ile ya maziko ya Kleist nilimuona Juma Mwapachu kanyanyuka kwenda kupokea jeneza la Kleist likitolewa nyumbani kwake Kawe Beach akiwa katika majonzi makubwa.
Juma Mwapachu akaniambia, ''Nakumkumbuka Kleist mwaka wa 1957 nimekuja likizo Dar es Salaam na nimefikia nyumbani kwao. Kleist akanichukua kwenda Amana Cinema Ilala kumwangalia Alan Ladd katika ''Shane.'' Kleist alikuwa mdogo kwangu lakini ndiye alikuwa akinivusha barabara ya Kitchwele tunakwenda kupanda basi la gorofa kwenda Ilala.''
1957 Kleist alikuwa mtoto wa miaka saba.
Siku ya sikukuu wenye majumba ya senema walikuwa wanajua waweke filamu gani wajaze watu hasa sisi watoto.
Kufika Empire Cinema nikakuta nje limewekwa bango kubwa la Elvis Presely kashika guitar jina la mchezo, ''Blue Hawaii.''
Naimba lyrics hizi za ''Blue Hawaii.''
''Night and you
And blue Hawaii
The night is heavenly
And you are heaven to me...''
Mtoto mdogo katika ''teens'' ana mengi ya kuhifadhi yenye faida kwa dunia na akhera yake lakini nyakati zile zilikuwa ngumu sana.
Hakuna katika sisi aliyekuwa hamjua Elvis Presley.
Elvis alikuwa star mkubwa wa Rock and Roll.
Mwaka wa 1964 tukikaa Mtaa wa Aggrey mwisho karibu unapokutana na Mtaa wa Nkrumah na kwa miaka ile sisi ndiyo tulikuwa Waafrika pekee tuliokuwa tumepanga sehemu ile majirani zetu wengi walikuwa Magoa.
Nalikumbuka duka nililokuwa nikitumwa kununua mikate maziwa na vitu vingine lilikuwa duka la Singa Singa nyumba ya pili kutoka kwa Gateways nyuma ya tajiri mkubwa Muhindi, Habib Punja.
Nilisoma na mjukuu wa Habib Punja St. Josephs, yeye akiletwa shule na Mercedes Benz.
Baba akinituma mara nyingi dukani hapo kununua Swiss Cakes alizokuwa akipenda kunywea chai ya jioni.
Jirani na nyumba yetu ilikuwa International Hotel hoteli yenye hadhi kubwa miaka ile na mkabala na kulikuwa na Annex yake.
Katika Annex hii Peter Colmore alikuwa na makazi ya kudumu ingawa mwenyewe akiishi Nairobi na akija Dar es Salaam kwa ajili ya shughui zake za biashara na Ally Sykes.
Katika umri ule wa miaka 12 sikujua kuwa iko siku watu hawa wawili nitasuhubiananao sana na nitaandika historia zao.
Nyuma ya hoteli yenyewe International Peter Colmore alikuwa na nyumba ya gorofa moja juu makazi chini ofisi ya High Fidelity Production makao yake makuu Government Road, Nairobi.
Hii ni ofisi aliyekuwa akitumia Peter Colmore na mshirika wake wa biashara Ally Sykes.
Turudi kwa Elvis Presley.
Nilikuwa sijapata kuona filamu yoyote ya Elvis kabla.
Kengele inagongwa...ngriiiii!
Niko katika kiti changu Empire Cinema.
Taa zinazimwa ukumbi mzima kiza kitupu.
Inasikika sauti ya Elvis anaimba nyimbo yenyewe ''Blue Hawaii.''
Elvis Presley alipotokea tu.
Kelele tulizopiga na miruzi hazisemeki.
Siku zote ninapoisikia nyimbo hii huwa inanirudisha udogoni na hupata hisia ''nostalgia,'' kutaka kama nirudi tena utoto na nitembee katika mitaa na barabara zilezile nilizopita nikiwa na umri wa miaka 12.
Blue Hawaii ilinichukua sana na nikampenda mno Elvis.
Ubongo wangu ukawa unanasa nyimbo zake kama sumaku inavyokamata chuma.
Nimehifadhi nyimbo zote kichwani.
Kichwa Cha mtoto chepesi kuhifadhi vitu hata kama ni vya kipuuzi.
Hela zangu za shule zikienda kwenye kununua rekodi, comics na kula ice cream Mainsfield Street.
Duka hili la ice cream liko hadi leo na lilikuja baadae kununuliwa na rafiki yangu marehemu Yusuf Zialor na akiliendesha mkewe Shama kwa miaka mingi hadi aipofariki hivi karibuni.
Siku ya Eid tukiruhusiwa watoto kuchelewa kurudi nyumbani.
Nakumbuka niliporudi nyumbani baba alikuwa keshaingia chumbani kwake kulala.
Asubuhi tukinywa chai ikawa kazi ya baba kunisikiliza kuhusu Elvis na muziki wake.
Baba akaniambia kuwa wao walipokuwa watoto wakimpenda Bing Crosby.
Balozi Abbas Sykes amepata kunihadithia kuhusu safari alizokuwa akifanya na baba yangu wakitoka Mtaa wa Kipata kwenda Avalon Cinema kuangalia senema za Bing Crosby, Loius Armastrong na wanamuziki wengine maarufu wa nyakati zao.
Hakika huwa na hamu ya kurejea utoto lakini kama ningerudishwa udogoni kuna mambo mengi ningefanya juhudi kubwa kuyabadili.
Leo asubuhi nilipokuwa nimetembelewa na hawa masheikh zangu hakika walinikumbusha mbali lakini nilifurahi na kumshukuru Allah kuwa hawa vijana wanapita njia nyingine kabisa.
Ningependa kuhitimisha kwa kueleza siku nilipokaribishwa na Prof. James Giblin kusomesha darasa la ''undergraduates,'' University of Iowa, Marekani.
Prof. Giblin aliniambia kuwa wanafunzi wangu ni vijana wadogo na wangependa kujua ujana wangu ulikuwaje huko Tanzania.
Niliposimama mbele ya darasa langu niliweka kwenye ''projector,'' picha ya bango la ''Blue Hawaii,'' hapo chini.
Nikawaambia kuwa ilikuwa baada ya kuangalia movie hiyo Blue Hawaii 964 ndipo niliponyanyua guitar na kujifunza kupiga.
Huwezi kuamini jinsi hawa vijana walivyohamasika na kwa kuwamaliza kabisa niliwawekea picha yangu nikiwa na umri wa miaka 17 kwenye Variety Show shuleni kwetu St. Joseph's Convent.
Miaka mingi imepita lakini naona kama vile ilikuwa jana.
PICHA:
Picha ya pili hiyo nyumba nyeupe ndiyo ilikuwa ofisi ya Peter Colmore na Ally Sykes katika miaka ya 1960 wakati mimi nakua.
Hayo majengo mengine hayakuwapo wala hilo banda mbele ya nyumba hiyo.
Nyumba hiyo ilikuwa imesimama hapo peke yake na ikipendeza sana ikiteNganishwa na "open space," kati yake na International Hotel.
Nilipofika hapa hivi karibuni baada ya miaka zaidi ya 50 ilinichukua muda mrefu kuitambua nyumba hii.
Nyumba ambayo baba yangu alipanga imevunjwa imejengwa gorofa ndefu.
Picha ya tatu nikiwa na Prof. James Giblin University of Iowa.