IoT
JF-Expert Member
- Apr 21, 2014
- 1,057
- 1,402
Leo hii Report ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali 2019/2020 imewasilishwa Bungeni. Kinachoshika headline kwa sasa ni juu ya ubadhirifu/ufisadi, pamoja na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi.
Tukiangazia kwa mapana, tutagundua kuwa hata report za ukaguzi kwa miaka ya nyuma zimekuwa zikifunua ufisadi mwingi unaofanywa na Taasisi na viongozi tuliowapa dhamana ya kutumika kwa maslahi ya Taifa letu.
Pamoja na hayo yote, hakuna hatua za dhati zimechukuliwa kuondosha huo ufisadi—kwa kuwachukulia hatua hao wabadhirifu wa fedha zetu.
Wananchi pia tumekuwa tukijadili kuonyesha masikitiko yetu, baadaye tunasahau kwa muda na kukumbushwa machungu kwa mwaka unaofuata.
Ikiwa tuna nia ya dhati ya kukomesha ufisadi, pendekezo langu ni kudai Katiba mpya kwa nguvu zote au kufanya maandamano ya kuishinikiza Serikali kuchukua hatua juu ya ufisadi huu. Vinginevyo, tutaendelea kushuhudia ufisadi usio na kikomo, na kila Rais akituhumu Tawala zilizopita kwa ufisadi, lkn baada ya muda nao hutuhumiwa kwa ufisadi—a vicious cycle.
Mwisho, tusitegemee maajabu sana kwa Rais mpya.