Acheni ujinga. Hana lolote na Kiingereza chake cha kimasaai. Bandwidth inasumbua nimeshindwa kuangalia clip nzima lakini hapo mwanzoni tu kachapia kwa kusema "rest you assured" badala ya "rest assured." Kiingereza anajua cha kawaida tu, huwezi kumfananisha na Benjamin Mkapa, Iddi Simba au Juma Mwapachu.
Kwanza hata Edward Lowassa angekuwa anajua Kiingereza, so what? Ufisadi wake unabaki pale pale. Ondoeni upuuzi wenu hapa kujaribu kujipanga kumpa sifa za kijinga. Huyu ni fisadi, ana utajiri mkubwa ambao vyanzo vyake havielezeki. Hafai kuwa kiongozi wa ngazi yoyote hapa Tanzania! Ukweli ndio huo...