Gautten Potten
JF-Expert Member
- Aug 22, 2022
- 1,642
- 3,426
Ronaldo Luis Nazario Délima mzaliwa was Rio Dejaneiro mnamo 1976 September 18 ni Moja kiumbe hatari na gwiji la kihistoria katika Mchezo wa soka ndani na nje ya Brazil kuwahi kutokea.
Kati ya Miaka ya 1994 na 1999, Ronaldo Nazário alifunga mabao 115 katika michezo 134 kabla ya jeraha lake la kwanza la goti lililomkuta akiwa Internationale Milan.
Psv Eindhoven
Mechi 57, Goli 54, Assist 7.
Fc Barcelona
Mechi 49,Goli 47, Assist 13.
Unaweza Kuona Conversion rate yake ilivyokuwa hatari.
Alifanya matukio ya kutisha kwa mabeki na makipa akiwa na 17 Hadi 22 katika ardhi ya Spain hata Italy.
Ndiye Mchezaji pekee aliyeweza kufunga mara 88 kwa kulamba vyenga magolikipa, kuaakalisha-kuwazunguka na Kisha kufunga.
Zifuatazo ni baadhi ya kadhia walizokutana nazo makipa :
Brazil vs Ghana 2006
Kingson vs Ronaldo na ndio Goli lake la mwisho katika World Cup.
Akifunga Mabao 15 katika Michezo 19.
Mtu anapandishwa viazi na kuacha Goli wazi Serie A.
Shughuli hii ya kuwarubuni na kuwalaghai Makipa aliianza mapema Sana na katika umri mdogo mno.
Mabeki kama Paolo Maldini, Fernando Hierro, Franco Baresi, Desailly, Cafu, Roberto Carlos, Costacurta, Nesta, Cannavaro, Thuram na wengineo. Generation ya vyuma hiyo hakuna mzembe,Kolo wala kilisha hapo.
"Ni ngumu kummaki hata umpake rangi kichwani
kwa miguso yake.
Mguso wa kwanza tu ashakuacha, wa pili anakuvuruga, kisha wa tatu anakudhalilisha vibaya sana. Alikuwa kama mgeni kila nikikutana naye" - Cannavaro.
"Ulikuwa ndio wakati pekee nilipomuona Maldini akiwa na wasiwasi kibaruani kwake.
Akaniambia 'Marcel, inabidi ukae karibu yangu. Nahitaji msaada wako hapa, lazima tumuongezee Lindo huyu mtu sio wa kawaida ni
mchawi." - Marcel Deasilly
Ronaldo ni mchezaji pekee kuwahi kumtisha Paolo Maldini! na kuivuruga Safu yake ya ulinzi Hadi kupewa Jina la Elphenomenon.
Maldini - "Nilikuwa na bahati ya kutosha kucheza dhidi ya Ronaldo. Alikuwa mtu wa ajabu na hatari Sana na mpinzani mgumu kuliko kuwahi kukumbana naye baada ya Maradona, R9 ndiye mchezaji mkubwa zaidi ambaye nimewahi kumfesi."
Pichani Maldini na Kipa wake walishaungwa tela, Billa mbinu chafu R9 alishamaliza Kazi.
Bila mbinu Chafu Paolo hakufua dafu kwa Délima.
Ni mwamba aliyepotea kwa miaka miwili baada ya kuumia goti na kurudi kuupiga Timu ya Taifa akiwa na goti Moja na kutwaa Ubingwa wa Dunia.
⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀⠀
Happy Birthday El Magnifico.
Ametimiza miaka 47.
Asante kwa kukonga Nyoyo zetu wakati wote uliokuwa uwanjani.
🥇🥇🥇🥇.