Vigezo vya mwenye uwezo ni kuelewa matatizo na kutupa plan inayotekelezeka ya kuyakabili, sijaliona hili bado.
Naona wagombea ubunge sample space hapa wanakuja na kutuambia "ubunge si kitu cha ajabu, mtu yeyote anaweza kuwa mbunge".
Umesema karibu na kweli kwamba kila mtu anajiona ana uwezo wa kuwatumikia wananchi (ingawa wengine wanajua wazi kwamba hawana uwezo wala nia ya kutumikia wananchi, bali wanataka zaidi kutumikia matumbo yao) lakini hata kama "wanajiona" wana uwezo, je ni kweli wana uwezo ?
Hata wala madawa haramu ya kulevya nao wana uwezo ? Watoa rushwa wakubwa nao wana uwezo ? Waliao ovyo kila wanapobanwa kwa kuwa hawana mkakati madhubuti nao wana uwezo ? Of course ukiwauliza watakwambia wana uwezo katika namna ya "mwamba ngoma huvutia kwake", lakini je wanaelewa matatizo ya nchi yetu kiundani na wana utatuzi wayo ?