Corticopontine
JF-Expert Member
- Sep 20, 2019
- 666
- 1,277
Bunge la Ulaya na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano ya kutoa passport ya kielektroniki (cheti cha Covid19) itayoruhusu Mtu kusafiri katika Nchi 27 za Umoja wa Ulaya ikionesha hali yake ya chanjo, majibu ya Covid19 au uzima wa afya yake.
Cheti hiki kinasemekana kitazuia hasara ambayo huenda ingepatikana msimu huu wa majira ya joto Ulaya ambapo Watu wengi husafiri katika Nchi tofauti kwa ajili ya utalii wakisisitiza kwamba hii ni kwa ajili ya kuaminiana tena, sio tu kwa Wanachama wa Umoja wa Ulaya lakini pia Raia wa Ulaya ili wafurahie haki yao ya kusafiri bila vizuizi.