Elewa kitendo cha Kulia na Faida zake Kiafya

Elewa kitendo cha Kulia na Faida zake Kiafya

Jiwa Hassan

New Member
Joined
Aug 20, 2024
Posts
3
Reaction score
3
Kimsingi kulia ni jambo linalofungamanishwa na HISIA. Na mara zote si LAZIMA iwe ni huzuni tu hata katika Furaha ya dhati huwa tunatokwa na machozi. Na hii utaiona Kwa wanyama wote kwani wao pia wana HISIA na matamanio ndiyo maana unaweza kumuona Tembo anatokwa machozi na anamuokoa MTOTO wake shimoni.

Kulia ni NAMNA Bora ya kupunguza shinikizo la HISIA hasi NDANI yetu pia kwani ni moja ya njia za kutokusanya majeraha ya HISIA. Hii husaidia kemikali za msongo kupunguzwa (stress chemicals) na zikaletwa zile za Furaha (endorphins). Hapa sasa mapigo ya moyo yatakuwa sawa na Ari ya kutenda inarejea.

Pia soma: Leo ndio nimegundua kuwa kulia ni tiba kubwa sana

Kutokwa machozi huleta u-sumaku wa HISIA endapo wapendanao wakikumbatiana Kwa Furaha ya dhati nadhani unaweza kuiona Kwa mama na MWANAYE.

Hivyo Kwa ujumla wacheni tuyaruhusu machozi kutoka. Usiikusanye HISIA NDANI YAKO. Kama ni huzuni achilia nishati hasi hii itoke na kama ni Furaha iruhusu nishati hii chanya itawale Lakini usikithirishe kwani lolote likizidi ni ishara ya changamoto za afya ya AKILI

Jina langu: Jiwa, Othman Hassan. (Mkurugenzi: THE BETTER YOU LTD) Mshauri Afya ya Jamii na Kujimudu
 
Back
Top Bottom