Elia Mpanzu ni rasmi kuitumikia Simba kwenye michuano ya kimataifa, kuanza na CS Sfaxien Jumapili hii

Elia Mpanzu ni rasmi kuitumikia Simba kwenye michuano ya kimataifa, kuanza na CS Sfaxien Jumapili hii

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Klabu ya Simba SC imefanikiwa kumuingiza winga wake mpya, Elie Mpanzu, kwenye mfumo wa usajili wa CAF, hatua inayomruhusu kuichezea timu hiyo katika mechi za Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup).
IMG_2186.jpeg

Kwa mujibu wa taarifa, Simba SC imepata leseni ya Mpanzu baada ya kumjumuisha kwenye usajili wa CAF jana, Januari 01, dirisha hilo lilipofunguliwa.
photo-output.png

Mpanzu ataanza kutumika Jumapili, Januari 5, katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia utakaochezwa saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Taïeb Mhiri, iwapo kocha Fadlu Davids atampanga.

Pia, Soma: Klabu ya Simba yalaani vurugu zilozofanywa na Klabu ya CS Sfaxien jijini Dar

Mashabiki wa Simba wanatarajia kumuona nyota huyo akitoa mchango mkubwa katika michuano hiyo muhimu.
 
Back
Top Bottom