Elias Maguri achana na Simba na Yanga

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Napenda kumuasa mchezaji huyu kuachana kabisa na mawazo ya kujiunga na Simba, Yanga na hata Azam kwa maendeleo yake ya kucheza soka. Badala yake ajikite kutafuta timu yoyote nje ya nchi hii hata Zambia kama walivofanya akina Samata na Ulimwengu. Asiwe na tamaa ya kufanikiwa kwa haraka kwani hata hao akina Samata na Ulimwengu walianza taratibu mpaka sasa wapo katika kiwango cha Kimataifa. Alikuwa Simba lakini wakamuona wa nini sasa wameanza kumvuruga mawazo ili aiache timu yake ya Stand United. Kuchezea timu ya taifa si lazima uwe timu za Simba na Yanga na sasa Azam!
 
Mimi binafsi ni yanga lakini simshauri aje huku, maana najua atakapoishia
 
Tatizo wachezaji wetu hawajielewi. Akishatangaziwa gari na millioni 50 huyo utamsikia mbio simba/yanga. Baada ya hapo benchi halafu anatolewa kwa mkopo anasahau kuwa sasa hivi anafunga sana kwa sababu anapangwa kila mechi dakika zote 90. Huyo maguli aachane na timu za bongo atafute timu nje. Ajiulize sasa hivi samata na ulimwengu wanalipwa kiasi gani. Na kama wangeendela kucheza hapa bongo sana sana wangekuwa wameshatemwa na simba na yanga labda kidogo mwadui ya julio ndio ingekuwa imewasajili maana julio ndio anajua vipaji vilivyotelekezwa..
 
Unaweza kumpa ushauri huo, lakini atakuwa muhimu sana kama hatakuwa na umri mkubwa. vinginevyo apige hela kibongo bongo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…