Elimu bado ni janga kwa wana michezo wetu, je ni Nini kifanyike kuondoa tatizo?

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
2,912
Reaction score
12,904
Karim Mandonga, mchezaji wa masumbwi aliyejizolea umaarufu mwaka wa 2022,huku akizidi kujipatia mashabiki kupitia tambo zake, yaani namna anavyojiamini na kutoa maneno ya vitisho kama hujawahi kumfahamu kabla waweza usije ulingoni ukiogopa kifo.

Kwasasa Karim Mandonga yupo nchini Kenya, huku mashabiki na wadau mbalimbali wa mchezo wa masumbwi wakisubiri kuona Nini kitatokea.

Tukirudi kwenye msingi wa swali langu, nimemsikia kwenye Clip moja anaseme anamshukuru Rais wa Kenya 'Anthony Ruto', na anamuahidi atafanya vizuri mbele yake ili kuendelea kupush mchezo wa boxing.

Je, Ina maana kweli Mandonga na ujanja wake wote anashindwa kujua jina la Rais wa Kenya?

Hakuna mwanadamu anaweza kujua Kila kitu, lakini Mandonga kanishangaza zaidi.
 
Mandonga kutojua jina kamili la Rais wa Kenya si ajabu na si vibaya maana ye anajua kupigana ngumi jiwe tu na anawajua mabondia wakubwa kina Mike Tyson na Mohamed Ali! Sidhani kama mtu kazi kafika form four!!

Nadhani "peleso peleso" ni staili nzuri ya ngumi za Mtu kazi Mandonga maana yake anakufuata na ngumi jiwe za mfululizo hadi unakata moto!hata ukimkandika makonde mazito ye anakuja tu na kurusha masumbwi non stop mpaka unakaa chini na kusalimu amri basi mtu kazi anaanza kucheza kwa kunema kama drunken master na kuruka ruka ulingoni kama Mohamed Ali inapendeza sana.

Hizi ngumi zake mpya za "Sugunyoo" toka Ukraine sijaziona ubora wake japo naamini zitakuwa vitasa vya maana! Mtu kazi si mchezo!

Ile Ngumi nzito sana ya Ndoige ilikuwa moto wa kuotea mbali, ukienda kushoto unakutana nayo kulia pia imo! Bondia wa Kenya akipona kwa Sugunyoo atapigwa kwa Ndoige na akichomoa Ndoige itakuja peleso peleso hatotoka akiwa hai!

Nimeona Mtu kazi Mandonga amei prove sana siku hizi anaanza kuwa bondia kamili taratibu ana ngumi nzito na anaficha uso si kama mwanzo ilikuwa Sanaa tupu!

Wadhamini hawatoshi Mandonga ameiva kwasasa anahitaji mapambano makubwa na mabondia wa Marekani!

Kwasasa hata Mayweather, Mwakinyo, Twaha Kiduku na Dula Mbabe sijui Mfaume wote wanakaa tu kwa Mandonga mtu kazi!

Hili balaa jipya la mtu kazi Mandonga la kupiga watu ngumi jiwe za tumboni si dogo naona wazi kabisa lengo lake mtu kazi ni kuwastaafisha masumbwi wote watakaokutana nae!
 
Maywether akikosea kusemaDr. Samia Suluhu tungesema ni bahati mbaya au dharau na si ujinga
 
Duh! anapigana lini nizione hizo peleso peleso za huyu kijana wetu,kipenzi cha watanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…