Elimu biashara: Nzi akiacha ujinga

sonofobia

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
1,171
Reaction score
4,295
Baada ya Kukosa kazi nikawa nawaza. Unga kllo 50 kwa mwezi tsh 65,000/=, kwa mwaka 780,000/=. Maharage kilo tsh 2,000, kwa siku @265 530,000/=, nyama kilo 6500, kwa siku 100 650,000 (jumla siku 365), mkaa 3000 kwa mwaka 1,095,000/=, mboga za majani 300, kwa mwaka 109,500, dada wa kazi 50,000/= kwa mwaka 300,000/=, Kodi unalipa 100,000/= (chumba na sebule) kwa mwaka 1,200,000/=, mafuta (kula na taa) 15,000/=, kwa mwaka 180,000/=, viungo kwa mwezi 24,000,kwa mwaka 288,000. Jumla 5,132,500/=. .
.
Kujenga hicho hicho chumba na sebule Kule Chanika ambapo Kimario anauza Viwanja Milioni moja kunaweza kusikugharimu hata 7m. Ntatolea na Mchanganuo wa hesabu, Tofali 900 @1000, 900,000/=, mchanga malori 2 @150,000, 300,000/=, Kokoto gari ndogo 150,000/=, maji 50,000/=, Cement mifuko 60 @12,000, 720,000 (mpaka sakafu ya rafu I.e rough floor), bati piece 30 @24,000, 720,000, Mbao Jumla (2x2 na 4x2) 1,400,000/= gharama ya ufundi 1,400,000/= (chini mpaka kupaua), madirisha 5 ya mbao, 450,000/=, plasta mifuko 30 na ufundi 560,000/=.Hapa unahamia wako ukisubiria kumalizia mdogo mdogo, unakua umebakiza Umeme, hizo gypsum na tiles si wengine tumekua hazipo mpaka leo, ila weka ruksa. Jumla 6,650,000/=(ramani ya nyumba nimeweka)
Hapa Tunachukulia Mfano wa Maisha ya kawaida tu. Achana na wale wanaowaza kukaa Goba wakat hata uwezo wa kununua Kiwanja Kinyamwezi Hawana, ambao ukiwapa takwimu watakupinga bila data au na data ambazo hawana, hawajawah hata zunguka Kerege wakaona watu wanavyojenga kwa mtaji wa Bagia. Sisemi Msile ili msijenge Hapana. Wala sisemi Kujenga ni bora zaidi ya kula Hapana. Wala sifananishi kula na Kujenga Hapana. Ila nasema tu, Nzi akiacha Ujinga anaweza Tengeneza Asali. Tuacheni Ujinga
By Albert Man Dea

C&P
 
Umetoa alternative nzr ya pesa ya kodi 1,200,000/= per year ni kujenga nyumba ya 7mil. How about hzo gharama nyngn?
 
Dhima yahii nyuzi ni kuuza kiwanja.
When you go places, go in style, nimeamini hahha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…