ELIMU BILA MATENDO IMEKUFA
Imani bila matendo imekufa!
Haya unaweza kuyaona kupitia(Kwa nini imani bila matendo imekufa?). Haya ni maneno yanayopatikana katika biblia. Ni maneno yanayo tutaka tuweke katika matendo kile tulichofundishwa na kuaminishwa. Haya pia tunayapata katika Quruan ambapotunaambiwa kuwa matendo na elimu huenda sambamba (htt://firqatunnajia.com/16-elimu-na-matendo-ni-mambo-mawili-yenye-kwenda-sambamba). Vitabu vyote viwili vinaonesha kuwa kunaulazima kuonesha katika matendo kile tunacho kifahamu au kuamini. Utamjuaje mtu aliyeelimika? Jibu ni rahisi tutamjua kwa matendo yake katika jamii. Elimu inatakiwa tuione katika shughuli zetu tunazozifanya, mawazo yetu tunayoyatoa na mienendo yetu ya kila siku. Kujua kitu halafu hukifanyii kazi hiyo ndiyo elimu iliyokufa.
Elimu haipatikani shuleni peke yake, bali ni kutoka katika jamii yetu kwa ujumla. Ili tupate maendeleo katika kila sekta lazima kizazi kipate elimu bora. Ubora tutauona katika utendaji wa wahitimu katika jamii na si matokeo yanayobandikwa kwenye mbao. Kama wanachofundishwa watoto hawakifanyii kazi baada ya masomo, hicho kitu kimekufa kwa maana kwamba watoto walichokuwa wanafanya ni kuhudhuria shule. Hivyo tuweke nguvu kuwa kinachofundishwa shuleni kinawekwa katika matendo. Tusiendelee kuwashuhudia bachelor holders wakirandaranda tu mitaani na bahasha za kaki kuomba ajira, kama ajira haipatikani waweze kujiajiri.
Tatizo la ajira ni kubwa sana yaani wanaoajiriwa ni wachache ukilinganisha na wanaohitimu masomo (Tatizo la uhaba wa ajira ni kubwa kiasi gani Tanzania? - BBC News Swahili). Tunashuhudia baadhi ya watu ambao hawakupata bahati ya kupata elimu rasimi ya shule wakijimdu kimaisha huku kuna baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu wakiwa ni masikini wa kutupwa.
Twende pamoja usichoke, wakati tunabeba mabegi kwenda shule huku tukiwacheka waliokosa nafasi ya kuendelea na masomo ya juu. Tulichekelea kana kwamba tumepata kombe la dunia. Hawa waliobaki waliumiza vichwa na kuamua kuweka kile kidogo walichonacho katika matendo, wakati tunahitimu vyuo wao tayari wanamiliki biashara, bustani, mifugo n.k. Tukazidi kupotea zaidi kwa kutumia muda wote kutafta kazi katika ofisi mbalimbali. Kwanini ofisi? ni elimu na imani au sumu mbaya tulizomezeshwa kwamba tukifaulu vizuri tutaajiriwa katika ofisi za viyoyozi. Tusipopata ajira huko tujue ni mgawanyo tu wa majukumu. Hatuwezi wote kuajiriwa kwenye ofisi hizi.
Lazima kila mtu aangalie ni wapi anaweza kuweka katika matendo kile anachokijua. Kwanini matajiri wakubwa nchi hii si maprofesa kutoka pale mlimani? wala wachimbaji wakubwa wa madini kama Laizer si Phd holders? Maswali ni mengi lakini jibu ni moja hawa watu waliweka katika matendo kile kidogo wanachokifahamu. Na sisi tuanze kidogo kidogo kabla ya makubwa. Watu watatuuliza mlifikaje huko juu? Tuamke leo kama jamii mdogo kwa mkubwa, raia wa kawaida kwa kiongozi. Tuthubutu kama taifa tusije tukaendelea katika kundi la walioshindwa.
Hivi kwa nini kila mmoja anatakiwa kuwajibika kuhakikisha elimu tuliyonayo inakuwa dhahiri?Mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya taifa tujifunge kibwebwe ili kile tunachokijua tukione. Maono hutokana na elimu mtu aliyonayo.Hii inamaana kuwa ili uwe na maono halisi lazima uwe na elimu bora.Maono halisi lazima yawe na mikakati ya kutimiza hayo maono. Lazima tujue baada ya kuhitimu masomo lazima tujue inatakiwa tufanye nini ili kiletulichopata kichipue (Indeed.Com - Career advice; finding a job/what to do after college).
Tunashuhudia vijana wengi ambao hawana hata ajira wakipata pesa inayoweza kuanzisha mradi mdogo, wanaishia kwenda kwa Mr. Matelephone na kununua smartphone ambayo atalazimika kuihudumia bila kumpa faida yoyote. Sisemi simu ni mbaya la hasha tuitumie kutunufaisha kama kutangaza biashara na kujiendeleza kupata ujuzi utakaotusaidia kuendelea mbele kidogo. Tutumie simu kuitangazia dunia mbuzi, kuku, matunda, culture, nguo na biashara nyingine. Tukiuza tutakuwa tumeihudumia dunia na sisi tutakuwa tumepata chochote kitu. Elimu yetu vyovyote ilivyo iwe duni au bora tuitumie kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.
Ni lini elimu yetu inakufa? Jibu ni rahisi kabisa kujibu swali hili, elimu yetu inakufa na kuzikwa tu pale tu tunapofikiri kusoma ni kupata vyeti na ofisi zenye viti vya kuzunguka na viyoyozi. Elimu ni kujua kuwa katika jamii kuna mgawanyo wa majukumu. Sehemu itakayokufaa zaidi ni kuanzisha shughuli zako mwenyewe kwani huku utastaafu ukiamua mwenyewe. Tupambane kuweka elimu yetu katika matendo kwa kujiajiri na mambo mengine. Ni maneno mazuri lakini huku ni sehemu pekee utatumia maarifa ya darasani na yale ambayo hujawi kufundishwa. Lakini kwa vyovyote iwavyo changamoto ni sehemu ya kuonesha uhalali wa vyeti ulivyonavyo. Je, kwako elimu ni silaha au ni kamba ya kukunyonga? (Education: The Most powerful weapon or changing the world | USAID Impact).
Elimu tunayowapa vijana wetu ni lazima iwape uwezo wa kuona kiu ya kusimama wenyewe kuliko elimu inayowapa ndoto za mchana wakiwa ofisi za UN pale New York. Idadi kubwa inaenda kusoma ili kupata kazi za mishahara mikubwa ni wachache wanaenda shule ili baadae waweze kujiajiri na kuendeleza vipaji vyao. Mambo yakienda tofauti vijana hawa huishiakujiingiza katika vitendo viovu kama ujambazi, umalaya, utapeli, madawa ya kulevya.
Watoto tuwafundishe kwa vitendo. Bora tuwafundishe kidogo ambacho wanaweza kukifanyia kazi kuliko kuwapa rundo la nadharia. Kuwafundisha kwa vitendo si darasani tu bali kwenye jamii yetu kwa ujumla. Viongozi wetu wa kisiasa wawe mfano wa kuigwa. Watu wetu mashuhuri wasipige tu picha sehemu nzuri tu, wawe tayari kupiga picha wakipanda mpunga au kusafisha zizi (Corrupt youth are product of our leadership and society). Ukisoma ripoti hiyo utaona ni kwa namna gani viongozi wala rushwa wanaharibu kizazi kjacho.
Mikakati iwekwe ili kila kijana afikiwe mahali popote alipo. Kulingana na REPOA inaonesha wanaohitimu masomo ngazi mbalimbali ni vijana takribani milioni moja na wanaopata ajira serikalini na taasisi nyingine ni 250,000 tu (BBC Article) . Vijana ni nguvu kazi ya leo. Juhudi zaidi ya hizi zinatakiwa kuongezwa. (Kazi.go.tz: Mh. katambi abainisha mikakati, sifa, fursa za ajira kwa vijana).
Licha ya ukweli kwamba serikali inajitahidi kuweka mikakati ya kuinua vijana ukweli ni kwamba serikali haitoweza kwa sasa kumfikia kila mmoja hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kutafta suluhu ya mapema kabla ya serikali kukufikia. Tuone juhudi zaidi za kumuinua kijana badala ya serikali kuwa kizingiti kwa vijana. Kuandaa vituo atamizi ni mbinu nzuri zaidi ambayo itawasaidia vijana kukuza elimu ya vitendo. Changamoto kubwa ya vijana si mtaji tu maana ukiwapa vijana mtaji wataishia wote kuanzisha biashara za mtaani zinazofanana na kugombaniana wateja wa mtaani. Biashara za aina hii huishia kufa.
Kwa kuhitimsha tunashuhudia ripoti zinaonesha kuwa nchi zilizoendelea zimeruhusu elimu kuwekwa katika matendo. Ukiangalia nchi kama Marekani, Ujerumani,Uingereza zinaongoza kuwa na mazingira mazuri ya kuwekeza (kutoka Gotquestions.com). Sekita pekee inayoweza kubeba kila mtu kiajira ni sekita binafsi. Kila mtu baada ya miaka 60 ya kustaafu, atarudi kuwa mkulima, mfanyabiashara, mfugaji, mvuvi au mjasiriamali. Kwa kuangalia ukweli huo ni lazima tuwekeze nguvu zetu huko tukiwa bado vijana. Ajira za serikali au katika taasisi nyingine zinaukomo. Hatuna budi kuanza mapema kabla hatujachelewa.
Na: Dony (0715675933)

Upvote
0