Elimu bila nidhamu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Kwahiyo elimu ni mafunzo yahusianayo na nguvu za kiakili, yaani kuendeleza akili na maadili, kwa kusoma na nidhamu, ili kumfanya binadamu kutenda katika usahihi. Elimu hii ni lazima iunganishwe na maarifa ya kazi bila hivyo elimu yetu itakuwa haijakamilika.
Kwahiyo mtu aliye elimika tutampima katika matendo yake. Ina niwia vigumu kuamini na kutia akilini mtu asiye kuwa mwaminifu na mwizi kuwa ameelimika.

Tutamuona mtu aliyeelimika anavyoendesha familia yake na anavyoishi na jamii inayomzunguka. Tutampima katika nidhamu yake. Elimu bila nidhamu ni maarifa tu. Haina faida yeyote. Haiwezi kujenga kitu chochote endelevu.
Elimu bila nidhamu ni sawa sawa na mto bila kingo. Mto bila kingo hukosa mwelekeo na huleta uharibifu. Ni jinsi gani fundi seremala mwenye maarifa ya kazi na asiye na nidhamu anaweza kulifaidisha taifa? Ikiwa watu watampelekea mbao awachongee thamani kisha kuwatapeli? Mtu huyu atakuwa na faida gani kwa jamii?


Ni jinsi gani mkandarasi tuliyemfundisha maarifa ya kazi ili ajenge nyumba zetu na madaraja yetu katika ubora atalifaidisha taifa?, ikiwa akipewa kazi anachakachua? Tutapataje mwelekeo kama taifa tukiwa na watu kama hawa? Hawa watu ni sawasawa na mto bila kingo. Je sisi kama taifa tutapigaje hatua kama tutaendelea kuzalisha watu kama hawa wanaotuibia na kujiita wasomi? Kwanini tunafundisha watu wetu stadi za kazi? Je ni kwa manufaa binafsi au kwa faida ya taifa kwa ujumla?

Huu ndio umuhimu wa nidhamu katika elimu yetu. Hatutaweza kujenga kitu chochote bila nidhamu hii. Taifa letu halitoendelea bila nidhamu kwa watu wetu. Hatutaweza kulinda na kuendeleza taasisi zetu bila nidhamu hii.
Bila nidhamu hii, watu wetu wataendelea kuyaibia mashirika na taasisi zetu ambazo ziko kwa faida ya watu wenyewe, katika misingi hii taifa letu halitoweza kupiga hatua kimaendeleo.


Note from the Book KIU YA UZALENDO.
 
Vyema Mkuu! Binafsi ninaamini kuwa Elimu ni maarifa, lakini si maarifa yoyote tu bali ni yale yaliyo sadifu na mahususi kwa eneo husika, maarifa haya mtu hujifunza! Hivyo nidhamu ya Maarifa haya tuyaitayo Elimu ni KUHALISIKA kwake kwa eneo yatolewapo! Hata wizi ni maarifa, na hufunzwa pia, lakini je, unasadifu nini kwetu? (hapa tulipaswa kurudi katika msingi wetu mkuu kama Taifa na tungepata jibu) Hata hivyo tunaweza jibu hivi, kuwa kwa ujumla tamaduni, siasa na uchumi wetu unakataza wizi(Afican Based systems) Basi wizi ni maarifa tu, lakini kwa vile si sadifu kwetu ndio maana hatuwezi kuita ni elimu kwetu. ELIMU NI MAARIFA YANAYOSADIFU MAZINGIRA NA NYAKATI ZA ENEO HUSIKA. a4afrika
Mungu wetu yu tayari kutupigania vitani. Anaita sasa!
 


Wizi ni maarifa gani? Destructive knowledge in faida gani kwetu? je nini chanzo cha elimu je ni maendeleo ya watu wetu au ni kuwaangamiza? Wizi ni ukosefu wa maarifa na ni ujinga kwa kuwa mtu afanye hivyo hupata madhara, Tunategermea elimu kuwa yenye faida kwetu na sio madhara. Wizi ukoi katika category ya ujinga kwasababu ya madhara apatayo mwizi kwa nafsi yake.

Nimezungumza kuwa elimu bila nidhamu ni maarifa tu kwakuwa ni lazima elimu ilekezwe katika mkondo fulani ambao ni productive kwa jamii na nikatoa mifano wa jinsi elimu yetu ilivyozaa mafisadi je ni sahihi kuwa na elimu ya namna hiyo? Je ni sahihi kuwafundisha watoto wetu maarifa ya wizi na kila ''art of evil?'' Je kwa mtazamo huo tutajenga jamii bora na endelevu? Hatutakuwa na jamii inayopigana yenyewe kwa wenyewe? Mimi naamini mwelekeo wetu ni lazima iwe kujenga jamii bora kadiri navyowezekana sehemu ambayo haki italindwa na kuendelezwa kwa vizazi vyote. Na kwa hali na mali ni lazima tuondoe uovu wa kila aina katika jamii zetu ili kujenga jamii bora.

Naomba unijibu swali nililouliza kutoka kwenye mifano ya fundi seremala na mkandarasi je watu hao watakuwa na faida kwa umma? Je elimu yetu itakuwa ni yenye mantiki kwa kuzalisha watu kama hao? Tunahitaji kutengeneza the best people as we can katika taifa hili lakini bila kuzingatia nidhamu zao tutawezaje?

Nafikiri huu ni mwanzo wa taifa letu kuendelea kama tutazingatia masuala haya ya msingi.
 
Note ''Kuendeleza akili na maadili'' ''kusoma na nidhamu'' kutenda katika ''usahihi'' na maarifa ya kazi.

Kuendeleza akili ni kumfanya aweze kufikiri mwenyewe na maadili ni kumjengea tabia yake. Kusoma ni kumpatia maarifa through books na mafundisho nk. Nidhamu ni kuelekeza mkondo wa akili za kijana katika mwelekeo fulani ambao utakuwa productive kwa jamii, ni kuangalia ''code of conduct'' . The whole process is the training of the mind na sio kumuingizia maarifa tu mtu bila kuangalia nidhamu yake.
Kitu tunachohitaji ni kujenga nidhamu ya jamii na hatutaweza bila Elimu iliyobora kama definition inavyosema hapo juu. Tunahitaji kujenga jamii yenye nidhamu na inayofikiri ....Inayooongozwa na fikra.
 

Tuko pamoja Mkuu! Sijapingana na post yako ya kwanza, labda sijaeleza vizuri kuweza kueleweka! Nilichomaanisha ni hiki, Elimu ni Maarifa lakini si kila Maarifa ni Elimu, Elimu ni Maarifa/Ujuzi unaosadifu Mazingira na Nyakati za eneo husika! Wizi ni Maarifa lakini si Elimu kwasababu unakinzana na nyakati zetu (tamaduni-vile mahusiano yapo)
Kwa maana hiyo kusema kwamba Kuna Elimu mbaya, ni makosa pia! Elimu/maarifa haya watu hujifunza, kinachoweza kuwa kibaya ni Mafunzo kama mchakato wa kufikia elimu, matokeo ya mafunzo yoyote yale ni maarifa sadifu (Elimu) ama yasiyosadifu (Upuuzi). Niliwah kutoa mfano huwa wa kumfundisha mtu aishie jangwani namna ya kuvua samaki, hata akiweza hatuwezi kuita ni Elimu, Elimu ni Ufunguo wa Maisha(hawakukosea), aje uvuvi utamsaidia jangwani? Ni Bure! Lakini maarifa hayo yapopatikana pwani, ni sahihi kuita Elimu maana yanahalisika!
Elimu ni Ujuzi na Maarifa HALISIKA! Relevant Knowledge & Skills! Ni wajibu wetu leo kupima mafunzo yetu leo (formal na informal) kwa kiwango gani yako-designed kufikia Elimu!
Mungu wetu anaita sasa!
 

Mkuu,

Ninakubaliana na ulichokiandika, Katika hali ya kawaida, elimu inatarajiwa kufundisha mambo matatu, nayo ni,

1) Ufahamu
2)Maarifa na
3)Itikadi

Katika hali yeyote ile, elimu inampa mtu ufahamu wa mambo, akishafahamu mambo kwa maana ya kujua hiki ni nini na maana yake nini then anajifunza maarifa.

Maarifa ni ile hali ya kuweza kutumia ufahamu wake katika mazingira yanayomzunguka, na inaweza ikawa kwa manufaa binafsi au ya jamii nzima, na pia inaweza ikawa kwa hasara binafsi au ya jamii nzima, hapa tuelewe pia kuwa manufaa binafsi yanaweza kuleta hasara kwa jamii na hali kadhalika hasara binafsi inaweza nayo kuleta hasara kwa jamii pia. kwa mantiki hii, nakubaliana na wewe kwamba wizi nao ni elimu kwa maana ya maarifa lakini elimu hii bado haijakamilika.

Kukamilika kwake mpaka elimu ile iwe na ITIKADI. Hapa kwenye itikadi ndipo hasa kwenye tatizo hususani katika nchi yetu,
Wasomi wetu wanaposaini mikataba mibovu, ni kwa sababu ya kukosa itikadi,
Wanaposhindwa kutatua matatizo ya jamii pamoja na usomi wao inaweza kuchangiwa na kukosa itikadi pia,

Miiko na ahadi za mwana TANU kwa mfano, zilikuwa ni itikadi zenye manufaa sana kwa taifa letu,
'kupoteana' tunakokuona hivi sasa, ni moja ya matokeo ya kupuuza itikadi hizo.
 


Tutampimaje mtu aliyeelimika labda niulize swali hapa? Je mnachukuliaje suala la nidhamu katika elimu yetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…