SoC01 Elimu bila ya adhabu kali na vitendo vya unyanyasaji inawezekana Tanzania

SoC01 Elimu bila ya adhabu kali na vitendo vya unyanyasaji inawezekana Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Adhabu na vitendo vya ukatili katika elimu vinaathiri maendeleo ya watoto wa shule katika harakati za kujipatia elimu , vitendo hivyo vinapingana pia na sera ya elimu ya Tanzania ya mwaka 2014 inayomtaka kila mtoto kupata elimu bora kuanzia shule za msingi, sekondari mpaka elimu ya chuo
Ni kawaida watoto wetu hutumia muda mwingi katika maisha yao kuwepo katika mazingira ya shule kwa kuenda asubuhi na kurudi majumbani kwao mchana au jioni na wengine huishi huko huko katika shule za bweni.

Shule nyingi hapa Tanzania zimekuwa zikitoa adhabu kali na vitendo vya kikatili dhidi ya watoto wawapo shule hasa pale wanapokuwa wameenda kinyume na sheria za shule

Adhabu kali na vitendo hivyo dhidi ya watoto ni kama yafuatayo

* Kuchapwa fimbo za kutosha, hii haikubaliki na iko kinyume na haki za binadamu.
Shule zote za serikali na baadhi ya shule za private hapa nchini zimekuwa zikitoa adhabu ya vikoboko kwa watoto kitu ambacho kinaathiri maendeleo ya watoto kitaaluma. watoto wamekuwa wakipigwa fimbo hazina idadi kwa makosa ya kawaida tu wawapo shuleni, mbaya zaidi siku hizi hata viongozi wenye dhamana na elimu nchini wanasisitiza walimu kutumia viboko kuadhibu watoto badala ya kukemea vitendo hivi

* Watoto wamekuwa wakiambiwa maneno makali na walimu wakiwa shuleni.
watoto wengi wamekuwa wakipewa maneno makali yakuvunja moyo na matusu pale tu wanapofanya vibaya kitaaluma huko shuleni, hii inawaathiri watoto wengi kisaikilojia na kupelekea kukosa kujiamini

* Watoto wengi hususani wakike wanapia manyanyaso ya kijinsia wawapo mashuleni, wengi wanabakwa na walimu na kujazwa mimba, hali hii ni kikwazo katika kufanikisha elimu kwa watoto wa kike katika shule za msingi na sekondari hapa nchini

Hivyo basi zinahitajika nguvu za ziada ikiwa ni pamoja na serikali kwa kushirikiana na wanajamii wote kuamua kupinga na kucondemn wazi wazi adhabu za viboko, ukatiri na unyanyasaji wa watoto shuleni. Pia kutoa adhabu kali kwa wale wote wanaoendelea kutenda vitendo hivyo katika shule zetu
Elimu bila viboko na unyanyasaji wa watoto shuleni inawezekana
 
Upvote 8
Kuna point katika bandiko lako ila haliko kwenye mtiririko unaoeleweka.

Kila paragraph ni kama ina taarifa tofauti lakini inayozungumzia kitu hicho hicho.

Ila hongera kwa kujitosa...kila la heri.
 
Kuna point katika bandiko lako ila haliko kwenye mtiririko unaoeleweka.

Kila paragraph ni kama ina taarifa tofauti lakini inayozungumzia kitu hicho hicho.

Ila hongera kwa kujitosa...kila la heri.
asante sana mkuu, awali nilikuwa sijui kama ninaweza kuedit
now nimejaribu kurekebisha typing errors na kuipanga upya kwa kiasi chake

naomba kura yako mkuu
 
Back
Top Bottom