SoC02 Elimu bora kwa matunda ya taifa la kesho

SoC02 Elimu bora kwa matunda ya taifa la kesho

Stories of Change - 2022 Competition

Mzaliwaa

New Member
Joined
Sep 13, 2022
Posts
2
Reaction score
1
Elimu ni ujuzi ambao mtu au mlengwa hupatiwa kwa lengo la kumtoa kutoka katika umasikini wa fikra kwenda katika ubunifu na uzalishaji wa mawazo ulio bora katika kuleta maendeleo baina yake na jamii inayomzunguka. Elimu inayotolewa nchini ni bora lakini sio bora zaidi kwa sababu ina mapungufu mengi kuliko faida na imezua maswali mengi kutoka kwa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu wakiuliza maswali kadha ya kadha kuhusiana na kile wanachokipata na kile watakachokizalisha.

Maswali ni kama vile;

1. Je elimu inakuza uelewa kwa mlengwa au ni kwa ajili ya kumtoa na kufanikisha amevuka kutoka katika ngazi au daraja moja la kielimu kwenda katika lingine?.

2. Je elimu itolewayo inaleta ufanisi katika nyanja mbalimbali, mfano katika teknolojia, utunzaji wa miundombinu na mazingira, inachochea kuanzishwa kwa fursa mbalimbali au ni mpaka watu wapate tena darasa baada ya kuhitimu ngazi zao za masomo ili kupata uelewa na muongozo wa nini wafanye katika kujikwamua kutoka katika sehemu moja kwenda katika sehemu ingine?.

3. Je elimu na mitaala itolewayo nchini ni kwa ajili ya kukuza walengwa ili kuleta maendeleo ya ndani kwa wakati huu au ni kwa ajili ya kujaza walengwa kwa fikra na vitu vya mataifa ya nje ili tuige yale yaliyofanywa kwa vipindi vilivyopita?.

4. Je elimu inayotolewa nchini ni kwa ajili ya kukuza kweli vipaji na kuviendeleza (mfano elimu zitolewazo kwa watu wenye vipaji maalumu) au ni kwa ajili ya kuhakikisha watu wamemaliza masomo yao kwa nyanja mbalimbali?.


Mfano elimu za vyuo vikuu zinasaidia watu baada ya kumaliza vyuo katika kujiajiri na kujiendeleza au ni mpaka kusubiri ajira?.

Imezoeleka katika vyuo mbalimbali kwamba wanafunzi husubiria semina mbalimbali kutoka kwa watu wa nje kama vile wafanyabiashara wakubwa au watu maarufu kama vile wanamuziki waliofanikiwa kibiashara ili kupata mawazo mbalimbali ya wapi kuanza na nini cha kufanya. Je kabla ya hapo wanafunzi hupata semina nyingi za ndani kupitia walimu wao na pia kutengenezeka kwa vikundi vya kutosha na venye tija ambavyo vitawasabibishia watumie ujuzi waliopata ndani ya mwaka huo wa masomo katika kuchanganua tatizo au jambo fulani ambalo limejitokeza kwa muda huo ili kukuza uelewa wao na kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kujitoa kutoka katika ngazi moja kwenda katika ngazi ingine kikamilifu na kujenga watu ambao wakishahitimu basi si watu wa kwenda kubweteka bali ni watu wa kutengeneza fursa sanifu katika nchi.

Pia suala la elimu inayotambulika kwa jina la vipaji maalumu, je ni kweli ni kwa ajili ya kuvitengeneza hivyo vipaji maalumu vilivyopo au tu inaitwa hivyo lakini haioneshi utofauti na elimu zingine zitolewazo. Na kama vipaji maalumu vinatengenezwa je ni kwa ajili ya maslai ya nchi au kuvitoa kwenda katika mataifa mengine ambapo vitaendelezwa na kukuzwa huko na kuchochea mafanikio katika hayo mataifa ya nje?.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom