JOSPIDE MAJABA
Member
- Mar 15, 2013
- 24
- 9
Nianze kwa kumpongeza mh.Pinda waziri mkuu wa Tanzania kwa kuunda Tume ya kuchunguza matokea mabaya ya kidato cha nne 2012 ili serikali iweze kujiridhisha wakati inapanga mikakati ya kuboresha elimu hapa nchini.Hata hivyo binafsi mbali na pongezi hizo sikuona umuhimu wa dhati wa kuunda tume ile tofauti na kutumia raslimali za umma tu maana sababu hasa zilizopelekea matokeo kuwa vile ziko wazi kabisa.
Wanafunzi hawa kushindwa kwao kuliandaliwa tangu chini kabisa wakiwa shule za msingina sio sekondari kama watu wanavyodhani.
Mtaala wa elimu ya msingi unaonesha masomo mengi mtoto wa darasa la kwanza anayotakiwa kusoma yakiwemo ya hesabu, kiingereza, kiswahili, sayansi, stadi za kazi, haiba na michezo nk. Wakati wanafunzi hawa ndo wanajifunza kujua kusoma, kuhesaabu na kuandika kwa wakati huo anafundishwa mambo ya sayansi na mengine yanayomtaka aandike wakati hajajua kusoma na kuandika.
Wanafunzi hawa walikuwa wakifika darasa la nne wanafanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne kwa ajili ya kuwapima ili waingie darasa la tano LAKINI cha kushangaza wataalamu walifuta kigezo cha kupandisha wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la nne kuingia la tano badala yake hata waliosindwa mtihani huo huruhusiwa kuendelea na darasa la tano.Kimsingi baadhi ya wanafunzi huingia darasa la tano bila kujua kusoma na kuandika.
Wanafunzi hawa huendelea hivyo mpaka darasa la saba ambapo hufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na wanaofaulu huchaguliwa kuingia kidato cha kwanza kwa elimu ya sekondari LAKINI alama za ufaulu kwa darasa la saba zimekuwa zikishushwa kila kukicha ili kuwafanya wanafunzi wengi waingie sekondari, matokeo yake wameingia sekondari wengi wakiwa na uwezo mdogo.Hili pia huchangiwa na mifumo ya mitihani inayobadilika kila wakati hadi sasa kutuletea mitihani ya kuchagua herufi za majibu ya sahihi hata hisabati, hili halikubaliki hata kidogo.
Wanafunzi walipofika kidato cha pili walifanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili licha ya kwamba shule nyingi zilikuwa na matatizo ya kimiundo mbinu ya shule hata hivyo lengo la mtihani wa kidato cha pili huwa ni kupima uelewa wa wanafunzi na kupata wanaoendele na kidato cha tatu ili hatimaye waingie wanafunzi safi kidato cha nne LAKINI wanafunzi wote hata waliofeli waliruhusiwa kuendelea na kidato cha tatu hadi cha nne na hatimaye tumeshuhudia madudu ya matokeo.
Katika ngazi zote amnazo wanafunzi hawa wamepitia wamekumbana na matatizo mbalimbali makubwa ambayo yamepelekea wavune mabua katika mitihani kwa mazingira waliyotengenezewa. Baadhi ya vikwazo ni pamoja na:
1. Uhaba mkubwa wa walimu kwa ujumla.
2. Uwepo wa walimu waliokata tamaa na mazingira ya kazi na kutoridhishwa na kipato cha kazi wanayoifanya kwa kupewa maslahi duni na kuwa na madai mengi ambayo wanaona yameshindikana.Walimu wengi wanaishi maisha ya kukopa unga, mchele, sukari katika vibanda vya wafanyabiashara jambo ambalo huwashushia hadhi na heshima zao katika jamii.Wengi wao hawana morari ya kufundisha kwa weledi na vilevile walimu wengi huonewa na kunyanyaswa na maofisa wao bila sababu za msingi.
3.Uhaba wa vyumba vya madarasa.Shule nyingi hazina madarasa ya kutosha kulingana na idadi ya ongezeko la wanafunzi kwenye shule jambo ambalo limewafanya wanafunzi wakose mahali pazuri pa kusomea.
4.Ukosefu wa maabara. Kwa wanafunzi wanaopenda sayansi wamejikuta katika wakati mgumu wa kukosa maabara kwa ajili ya masomo yao ya sayansi jambo lililopelekea wasome masomo ambayo siyo chaguo lao hadi kupelekea kuwa na matokeo mabaya lakini hata shule zilizojikakamua kwa upande wa serikali kuwa na maabara zimejikuta hazina walimu na vifaa kwa ajili ya maabara.
5.Ukosefu wa HOSTELI.Wanafunzi wengi wanasoma aidha wanatoka nyumbani ama wanatoka nyumani kwao moja kwa moja.Wanafunzi wa bweni sio wengi kama kulinganisha na wa .Wengi wao wamejihusisha na mambo yasiyofaa hadi kupelekea kutozingatia masomo hasa kufanya walimu washindwe kuwadhibiti vizuri wanafunzi hawa maana ili mwanafunzi aweze kufanya vizuri katika masomo yake ni lazima asimamiwe na mwalimu, sasa hawa wanafunzi wanatoka nyumbani kwa kiasi kikubwa,nini matokeo?
6. Wazazi kutowajibika. Kwa kiasi kikubwa katika suala la elimu wazazi wamejiweka pembeni na kuwaacha walimu kushughulikia suala hilo wakati linahitaji nguvu ya pamoja.Wazazi wengi hudhani akishatoa mchango shuleni basi amemaliza kumbe anapaswa kufuatilia maendeleo ya mtoto wake na kudhibiti nidhamu yake pindi awapo nyumbani.Wazai hawafanyi hivyo na badala yake wapo wazazi ambao huendesha harakati za kuwashambulia walimu bila sababu yoyote na kuwavunja nia ya kuendelea kufundisha.
7. Walimu waliovamia fani. Kimsingi wapo baadhi ya watu ambao wamejiunga na kozi za ualimu si kwa sababu wana mawiwa ila tu kujipatia ajira na kuendelea na mambo yao tofauti na ya kufundisha.Kwa mfano wapo watu wanaosoma ualimu vyuo vikuu lakini eti kwa sababu ya kigezo cha kupata mkopo.Watu wa aina hii ndio huenda shuleni kuchakachua na siyo kufundisha.
8. WANAFUNZI KUTOJISOMEA.Ni ukweli usiopingika kwamba wanafunzi wa sasa hivi kwa kweli ni janga, yaani wana areji na vitabu, hawapendi kuisomea hata wale wanaobahatika kuwa na baadhi ya walimu ari zao za kujisomea ni ndogo sana inahitajika mikakati madhubuti kusaidia wanafunzi hawa kurudisha moyo wa kupenda kusoma.
9. Ukaguzi wa shule. Wakaguzi wa shule hawajawezeshwa vya kutosha ili kufuatilia masuala ya ufundishai wa walimu.Wakaguzi ndiyo macho ya kusaidia kuwaweka walimu kwenye mstari kama wamepotoka mahali fulani katika ufundishaji na kama hawawezeshwi nini kinaendelea? LAKINI pia hata waliopo baadhi yao hawana uwezo wa kuwakagua walimu.Unategema mkaguzi mwenye diploma anamkagua mwalimu mwenye digrii ana lipi la kumuongezea kama siyo kujaza fomu na kuondoka na mwalimu kuendeleza mambo yake?
10.Walimu hawashirikishwi.Kuna mambo mengi yanafayika kuhusu walimu bila wao kushirikishwa, mfano mabadiliko ya mitaala ya elimu, walimu huona wanaletewa mitaala kuitekeleza bila kuwa na semina na mafunzo ya kutosha jambo linalopelekea walimu kufanya kazi kwa uzoefu na sio weledi wa kimatini.
11.Wanasisa. Wanasiasa kwa kiasi kikubwa wameathiri elimu ya hapa nchi kwa kuingilia kazi za kitaaluma zaidi badala ya kufanya siasa zenye manufaa kwa jamii.Wanasisa wamewaaingilia walimu hadi wengine kufikia hatua ya kuingia madarasani kuwakagua kama wakaguzi.Jambo hili limewafanya walimu kuwa katika hali ya sintofahamu kuhusu wasimamizi wao.
Kimsingi yapo mambo mengi lakini machache nimeyaorodhesa. Sasa ni nini madhara ya kuwa na elimu mbovu kwa Taifa.
Kwanza, Taifa halitopata wataalamu wa fani mbalimbali mfano; madaktari, wanasheria, walimu, mainjinia, wanasiasa na wtaalamu wengineo wengi.Baadhi yao hawa watakaopatika watakuwa ni wale wanaopindisha mambo yaani daktari anapasua kichwa cha mgonjwa badala ya mguu, injinia anajenga daraja akipita binadamu tu na siyo gari daraja linabomoka, atapatikana mwalimu wa kufundisha 1 + 1= 11.Hivyo mwelekeo wa Taifa utakuwa ni kiza kinene.
Pili, shule nyingi za kidato cha tano zitafungwa kwa kukosa wanafunzi wenye sifa kujiunga hivyo ajira za watu wengi zitapotea.
Tatu, Taifa litakuwa limejitenga na dunia nzima kwa kuwa na watu mbumbumbu.
NINI KIFANYIKE SASA?
Binafsi napendekeza hatua za makusudi na za haraka zichukukuliwe na serikali maana ndiyo ina mkataba wa kuwaletea maendeleo wananchi wake:
1.Serikali ilinganishe mishahara ya walimu sawa na watumishi wengine kama Kenya walivyo fanya ili kuondoa malalamiko kwa walimu kwamba wanaonewa na kudhulumiwa kwa kulipwa vibaya hivyo kukosa ari na tija ya kufanya kazi vizuri.
2. Mazingira ya kufundishiaa na kujifunzia yaboreshwe; madarasa, vitabu, umeme na nyenzo nyingine muhimu zitolewe na serikali iitoe muhanga kwa hili
3.Sheria za kuwathibiti wanafunzi ziwekwe wazi na ziwaruhusu walimu kutumia mamlaka kuwashughulikia wanafunzi kwa ufasaha tofauti na sasa hivi mwalimu lazima apate kibali cha mkuu wa shule kumwadhibu mwanafunzi jambo linalopelekea utovu wa nidhamu kwa wanafunzi kuwa mkubwa hadi wamefikiaa kutoa matusi kwenye mitihani ya Kitaifa! aibu gani hii?
4. Waajiriwe wakaguzi wengi wa shule na kupewa vifaa vya kutosha ili waweze kufanya kazi zao vizuri.
5.Walimu washirikishwe katika mambo yote yanayoihusu elimu hususani mabadiliko ya mitaala sambamba na kupewa mafunzo na semina za kutosha kwa walimu wote kuhusu mabadiliko hayo tofauti na sasa wizara inaleta mabadiliko kwa walimu watekeleze bila kuelimishwa.
6.Walimu waruhusiwe kujiendeleza kielimu na wadhaminiwe wanapotoka masomoni badala ya kukatishwa tamaa.
7.Wazazi na wadau wengine wote wa elimu washikamane kwa dhati na walimu wao ili kuweza kupata elimu iliyo bora na wanasiasa waache kuwafuatilia walimu kwa njia zisizo halali, wawatengenezee mazingira safi na ulinzi dhabiti.
8. Baraza la mitihani litunge mitihani yenye ubora na kuhakikisha usahihishaji wake ni wa makini na sio wa ubabaishaji kw kupeleka walimu wenye uwezo mzuri kusahihisha, sasa hivi mambo haya yanafanywa kama dili na sio kuzingatia weledi.
9. Kwa kila ngazi ya elimu suala la kurudia kwa wanafunzi wanaofanya vibaya lirudishwe yaani kila darasa kuwekwe alama za kupanda darasa jingine kuanzia elimu ya msingi kwenye mzizi maana huko ndiko ubovu wa watoto unakoanzia.kama mwalimu wa sekondari napokea mwanafunzi asiyejua kusoma na kuandika unatarjia amsaidiaje?
Yapo mengi ya kueleza hapa maana nina uchungu sana baada ya wadongo zangu lukuki kuambulia sifuri katika matokeo ya kidato cha nne 2012.
KWA PAMOJA TUJENGE TAIFA LETU TANZANIA.
AHSANTENI.