Kikapuu
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 1,122
- 1,629
Utangulizi.
Elimu kwa maana pana ni tendo au uzoefu wenye athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine (Wikipedia). Elimu Bora ni ile itolewayo kwa jamii ili kukidhi mahitaji yao kulingana na rasilimali zinazowazunguka, mwanafunzi huandalia ili aweze kukabiliana na mazingira husika.
Chanzo : Effermit
Baadhi ya nchi zenye elimu Bora.
Kwa kuanza na dunia kwa ujumla baadhi ya nchi hizo ni Kama vile Canada, Marekani, Israel, China na Urusi. Kwa kuangazia bara la Afrika ni Kama vile shelidheli, Afrika kusini, Tunisia pamoja na Mauritius, hii ni kwa mujibu wa NewsNowGh. Utoaji wa elimu katika nchi hizi ni ule wa kuandaa wataalamu kulingana na rasilimali zilizopo eneo husika na ufundishaji kwa njia ya vitendo zaidi kuliko nadharia.
Namna Bora ya kuwa na elimu Bora.
1. Uwepo wa lugha moja ya kufundishia. Mwanafunzi na mwalimu anapaswa kutumia lugha moja kwa ufasaha ili mawasiliano baina ya mwanafunzi na mwalimu yaeleweke. Jamii au serikali inapaswa kuchagua lugha moja kwa ngazi zote za ufundishaji.
Chanzo : Kutoka mtandaoni
2. Uwepo wa utawala bora kuanzia chini hadi juu. Kila mmoja anapaswa kutoa mchango wa kuhakikisha elimu inatolewa kwa uweledi wa hali ya juu. Uwajibikaji unapaswa uanzia kwa mtu mwenyewe, familia, jamii, hadi serikali.
3. Ushirikiano wa taasisi mbalimbali na shule husika. Elimu bora ni ile ambayo shule hushirikiana ipasavyo na mashirika au taasisi kwa mfano maktaba kuhakikisha wanafunzi wanasoma na kupanua maarifa kulingana na mahitaji yake.
Chanzo : twitter
4. Mtaala bora unaoendana na rasilimali zilizopo. Shule inatakiwa itoe elimu kwa kuzingatia rasilimali za eneo husika mfano eneo lenye hifadhi za taifa inapaswa kuwe na elimu inayohusu masuala ya hifadhi. Hi itasaidia kujifunza kwa uhalisia na kuibua wajuzi wa masuala hayo kuliko kufundisha elimu isiyoendana na eneo husika.
5. Uwepo wa mbinu bora za ufundishaji. Mafunzo kwa njia ya vitendo ni muhimu kuliko nadharia, mwanafunzi ataweza kueleza zaidi kuhusu somo husika bila wasiwasi na itajenga tabia ya udadisi kwa mwanafunzi kwani rasilimali zitakuwa karibu nae. Pia matumizi ya tehama ili kuokoa mda wa kuandika na kueleza dhana katika somo husika.
Chanzo : yanablogepotcom
6. Uzalishaji bora wa wataalamu kupitia ujuzi kuliko ufaulu. Ili mwanafunzi awe mbobevu inapaswa iwepo timu ya kuchunguza kipaji chake kwa ngazi za chini za elimu. Hi itasaidia kukuza wataalamu mahiri, endapo mwanafunzi uhalisia wake wa ujuzi hauendani na rasilimali zilizopo inapaswa kuhamishwa mapema na kupelekwa eneo husika.
7. Uwepo wa muundo bora wa elimu ikiwa ni elimu ya awali, elimu ya upili, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Muundo huu utasaidia kupunguza mda mwingi wa kukaa shuleni na kuwapa mda wa kutosha kusoma fani husika na kwa mda unaohitajika.
Chanzo : kutoka mtandaoni
8. Kujenga mazingira bora ya utoaji wa elimu. Kwa kuzingatia miundombinu na afya kwa watoa huduma ya elimu na wanafunzi. Majengo na zahanati vinapaswa kuwa bora na utoshelezi wa vifaa kwa kila sehemu husika.
9. Kupunguza idadi ya masomo na kuyapa kipaumbele masomo husika yamfaayo mwanafunzi. Kufikia elimu ya upili mwanafunzi anapaswa kujikita kwenye fani husika bila kupoteza mda. Afya ya akili kwa mwanafunzi itakuwa bora zaidi kuliko mwanafunzi mwenye masomo mengi yasiyo na tija kwa maendeleo ya jamii imuzungukayo.
Chanzo : Africaparent
10. Mgawanyo bora wa shule. Utoaji wa elimu shuleni unapaswa ufate rasilimali zilizopo eneo hilo. Itapunguza uhitaji wa vifaa kwa vitendo na kusaidia utumiaji bora wa pesa kwa nyanja ya elimu. Mseneo yenye madini inapaswa kusepo shule za ufundi na maeneo ya kilimo napo elimu kuhusu kilimo inapaswa itolewe na sio elimu ya kilimo itolewe sehemu ambapo hata kilimo hskuna.
Wajibu wa kuboresha elimu ni wa kila mwanajamii
Katika dunia kila kinaishi kwa utegemezi wa kitu kingine. Hivyo jukumu la uwepo wa elimu bora ni kwa kila mtu si serikali, si jamii, si mwalimu na wala si mzazi au mwanafunzi. Hivyo wanajamii wanapaswa kujitoa ili kuhakikisha huduma ya elimu inatolewa kwa ufasaha.
Serikali Inapaswa kuaandaa mifumo bora wa utoaji elimu, utoaji bora wa vifaa vya utoaji elimu pamoja na uongozi bora kwa kuhakikisha kila mtu anawajibika kulingana na majukumu yake. Kuunda taasisi zitakazoshughulika na masuala ya rasilimali, vipaji pamoja na mahitaji ya eneo husika hadi ngazi ya kitaifa.
Jamii kuhakikisha huduma ya elimu inatolewa ndani ya jamii kwa kutoa mchango mbalimbali kama ujenzi wa miundombinu ya shule, ushirikiano bora na watoa huduma wa shule ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.
Chanzo : madukamedia
Mzazi, mlezi na wanafunzi uongozi bora unaanzia chini kabisa hivyo mzazi anapaswa kufatilia maendeleo ya mwanafunzi kwa kuhakikisha anapata elimu bora. Kuhakikisha mwanafunzi ana nidhamu ya kutosha na hulka ya kujisomea na kudadisi vitu mbalimbali vilivyopo eneo husika. Pia, mwanafunzi anapaswa kutoa ushirikiano kwa mzazi, mwalimu na hata mshauri wake kwenye fani husika.
Chanzo : udakusoeccially
Mwisho, upatikanaji wa elimu bora unahitaji mchango mkubwa kupitia rasilimali zilizopo katika eneo hili ikiwemo rasilimali watu. Elimu bora inahitaji uwekezaji mkubwa wa fedha na muda, kupitia vitu hivi tunaweza kupata matunda bora zaidi. Uaandaji wa wataalamu wa baadae utakuwa Bora na wenye tija kwa jamii husika. Pia, uwepo wa utawala bora na mfumo bora kwa nchi husika itarahisisha upatikanaji na utoaji bora wa elimu nchini.

Upvote
1