Elimu Haina Mwisho; 'mchongo' adhimu kwa mtoto wa kike

Bigmaaan

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2023
Posts
306
Reaction score
699
Habari za Jioni wakuu?

Leo nimeona niwashirikishe juu ya mchongo huu. Ni kuwa, hii ni Program maalamu ya kuwawezesha mabinti ambao hawakumaliza elimu ya Sekondari kwa sababu yoyote kujiendeleza kielimu na kifani. Elimu hii wanaipataje na kwa gharama gani?

1. Elimu hii inapatikana kwenye vyuo vyote vya Maendeleo ya wananchi (FDC) zilizopo nchi hii.
2. Kama hakumaliza Form 2, atasoma Form 1 & 2 Mwaka mmoja kisha atafanya mtihani wa Taifa. Akifaulu ataendelea Form 3 hapo hapo chuoni.
3. Kama aliishia Form 3 au Form 4[hakufanya Mtihani wa Taifa] basi atasoma Form 3 & 4 mwaka Mmoja kisha atafanya mtihani wa taifa.
4. Akiwa anasoma masomo hayo, atachagua na FANI MOJA ya itayokuwepo chuoni hapo, Mathalani Chuo cha FDC Urambo au Mbeya wanatoa fani za Umeme wa Majumbani, Ushonaji nguo, Ufundi wa Magari, Uselemala au TEHAMA atachagua moja katia ya fani hizo
5. GHARAMA ZA MASOMO. Hatolipa Ada, Chakula wala hostel [ni sharti aishi hostel za chuo], yeye atagharamika sh 54,000 kukata bima yake ya NHIF [ikiwa hana] na atalipia Uniform yake tu.

Faida kubwa ya Kozi hii ni kutafuta Cheti cha sekondari huku ukipata cheti cha fani ambacho utamuzesha kusaka michongo mingine au hata kujiajiri mwenyewe.

So, kibongo bongo tunao mabinti wenye uhitaji huu. Hebu tuwapeleke kwenye fursa hii.
 
ni kweli mleta maada mchongo huo niliupata ,na kuufanyia kazi, vijana wangu wawili watoto wa ndugu wamepitia hapo na alangau cheti cha four 4 wamepata na fani wameambulia leaving certificates wamegoma kusapua ,pia baada ya pasaka kuna mwingine tunapeleka huko kasulu fdc ni mpango upo pw.
 
Uwahi, tar 31 mwisho wa udahili march.
 
Kuna dada yangu anaitwa Lamomy ela anazo ila kaishia darasa la pili ngoja nimsogezee mchongo huu kuna namna inatakiwa aongeze kaelimu

Hivyo vyuo vya FDC Da'slam vinapatikana?
 
Kuna dada yangu anaitwa Lamomy ela anazo ila kaishia darasa la pili ngoja nimsogezee mchongo huu kuna namna inatakiwa aongeze kaelimu

Hivyo vyuo vya FDC Da'slam vinapatikana?
Au sio? 😹😹
Haya lipa school fees nianze kupigwa pindi na malekachaa wa FDC 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…