BUMIJA
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 5,950
- 11,295
Wasalaam.Kumekua na tabia siku hizi hasa kwa wale waliofanikiwa kimaisha kwa njia tofauti na kisomo kuwabeza waliosoma kwamba si chochote.
Mfano kuna mtu anaitwa Dotto Magari na Mbunge Msukuma.
Hawa wanaponda sana watu walio na Elimu kwamba haina faida.
Najiuliza wakienda Hospitali hao madaktari wanaowatibu si wanatumia Elimu zao?
Ni mfano tu wa hao ila mitandaoni kumeibuka wimbi kubwa la watu wakinanga na kuonyesha elimu haina manufaa.
Watoto wa maskini wanamezeshwa hizo Perspective huku watoto wa viongozi wakiendelea kupata Elimu nzuri zaidi na huenda tukatawaliwa na vizazi vile vile miaka ijayo.
Tumejengewa mifumo na misingi kwamba manufaa ya elimu ni kuajiriwa.
Dhana ya kuajiriwa inaturudisha nyuma wengi.
Lakini pamoja na ajira za kuajiriwa kupungua haimaanishi thamani ya Elimu isiwepo.
BUMIJA Tutor.
Arusha, Tanzania