Elimu ilikuwa mkombozi wa Wanawake na Vijana maskini lakini janga la ajira limewarudisha kulekule kwenye utumwa

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
ELIMU ÍLIKUWA MKOMBOZI WA WANAWAKE NA VIJANA MASKINI LAKINI JANGA LA AJIRA LIMEWARUDISHA KULEKULE KWENYE UTUMWA

Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli

Elimu ñdio ilikuwa ukombozi wakutegemewa na Wanawake waliowèngi na vijana kutoka familia maskini.

Wanawake wengi hasa wale waliokuwa wanafanya vizuri shuleni waliona nuru ya matumaini katika maisha yao.

Tayari walikuwa na mifano dhahiri ya wanawake waliosoma na walioajiriwa pamoja na baadhi ya viongozi wa kike kitaifa.

Hii iliongeza kujiamini kwao kwamba watakaposoma na kupata elimu angalau ya stashahada au shahada moja wataweza kujitegemea na kujinasua katika makucha ya utumwa wa mwanaume.

Lakini kama ilivyosemwa ng'ombe wa maskini hazai. Wanawake wengi wamesoma lakini wamejikuta wamesoma katika kipindi ambacho tayari kuna wasomi wengi na uhitaji wao umekuwa mdogo.

Hofu imetamalaki. Kiburi cha kuona wangeweza kujitegemea kinayeyuka. Ukweli ni kuwa kwenye suala la uchumi na uzalishaji Mwanamke hana pumzi ya kutosha kukusànya utajiri nje ya kuajiriwa

Ni wanawake wachache sana ambao wana uwezo wa kuvumilia na ku-sustain kwenye mapambano ya maisha pasipo kuhitaji msaada wa mwanaume

Wengi huanza kwa mbwembwe lakini hawafiki mbali wanajikuta wakikata tamaa. Tunasema ngoma ya watoto haikeshi. Amesoma ndio lakini kama asipoajiriwa kwenye uchumi atakuwa sawa na yule asiyesoma.

Biashara ndogondogo zisizokua ambazo zinakabiliwa na pepo na tufani za changamoto huwafanya wanawake wasomi kuweka mpira kwapani au kurudisha mpira huo kwa kipa.

Bado ndoa itaendelea kuwa sehemu ya kitega uchumi kwa wanawake Duniani. Sio Afrika ni duniani hata hizo nchi zinazoitwa zimeendelea.

Wakati huo wanaume nao upataji wa elimu utachangia kwa kiasi kikubwa kuona hakuna umuhimu wa ndoa yaani kuajiri Mwanamke huku wakiona ni biashara au kuendesha kampuni isiyo na faida zaidi ya kunyonywa.

Zaidi tabia ya watoto wengi wakikua kuwapendelea Mama zao ni sababu nyingine ya vijana wa Gen Z kupinga kuishi kwenye ndoa.

Suluhu kwa wanawake itakuwa kuwageuza watoto kuwa vitega uchumi vyao baada ya Taasisi ya ndoa kudondoka na wanaume kukataa kuishi hata kinyumba na wanawake. Huku wanaume nao suluhu yao ikiwa ni kutoa child support tuu na kuwafanya wanawake wawe Watu wa kulalamika kutokana na ugumu wa maisha.

Changamoto itakuwa kwa wale wenye ndoa na wanaume wanaohudumia familia zao vizuri.
Wanawake wengi watajigonga na kupigania kuingia kama sio kuvunja kabisa ndoa hizo. Vijana watakuwa na pesa lakini hawatataka kuoa baada ya kugundua kuwa wanawake wengi huvizia pesa zao.

Na kitendo cha wanawake kutowataka wanaume wakati huo Wakiwa hawana pesa na baadaye kuwashobokea Wakiwa na pesa, kitakuwa ni red alert Kwa Vijana hao waliofanikiwa. Wengi watataka kuwa na watoto tuu.

Kauli ya tafuta pesa imelenga zaidi kuweka upendo na utu pembeni huku vita ya kuonyeshana uwezo wa kiutafutaji baina ya Mwanamke na mwanaume ikiwa Dhahiri.

Ingawaje mwisho wa pambano wanawake wataangukia pua na wachache kati yao watapatemo chochote kitu. Kifuatacho ni msemo kuwa Mwanamke ni chombo cha starehe kitarejeshwa na zama zitajirudia.

Watanunuliwa kimafungu kwa ukahaba. Watanunuliwa kimafungu na kuolewa Mitala kama zamani.
Kwa sababu upendo na utu hautakuwa kipaombele tena bali matokeo ya tafuta pesa yatajirudia ambapo zamani ni mwanaume lazima uwe na mali.

Mwisho wa siku Mwanamke atabaki kuwa Mwanamke na tegemezi daima dawamu. Na maskini ataendelea kuwa maskini daima dawamu. Ingawaje wapo Exceptional ambao ni wachache sana ambao wataweza kuvunja hiyo kanuni. Na msemo wa maji hufuata mkondo utaendelea kudumu.

Ijumaa Kareem

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
nini kifanyike ili tusikatae ndoa mkuu?
 
Upendo na utu utañgulizwe.

Mbaya zaidi kwa wanawake wengi, njaa haikai pamoja na MAPENZI.

So acha mambo yaende hivihivi. Yatajiseti yenyewe mbele kwa mbele
Mkuu mda mwingne vijana hawakatai ndoa eti kwa sababu wana njaa ,mimi tena naona vijana wengi wanaojitafuta bado ni wanaoa kwa kasi na kuishia njiani.
 
Kwa wanawake wengi, Njaa haikai pamoja na Mapenzi.

Nafikiri hujanielewa
 
Msomi anatengeneza ajira sio kutegemea kuajiriwa.

Usomi wa shuleni haupo kufundishwa kutengeneza ajira bali kuwa mfanyakazi bora au kutumikishwa.

Ndio maana mfumo wa elimu wetu mwanafunzi hujengewa hofu ya kumwogopa mwalimu.

Uliona wapi mtu mwenye hofu akatengeneza ajira.

Kujiajiri inahitaji uthubutu
 
ELIMU ÍLIKUWA MKOMBOZI WA WANAWAKE NA VIJANA MASKINI LAKINI JANGA LA AJIRA LIMEWARUDISHA KULEKULE KWENYE UTUMWA

Anaandika, Robért Heriel
Mtibeli

Elimu ñdio ilikuwa ukombozi wakutegemewa na Wanawake waliowèngi na vijana kutoka familia maskini.

Wanawake wengi hasa wale waliokuwa wanafanya vizuri shuleni waliona nuru ya matumaini katika maisha yao.

Tayari walikuwa na mifano dhahiri ya wanawake waliosoma na walioajiriwa pamoja na baadhi ya viongozi wa kike kitaifa.

Hii iliongeza kujiamini kwao kwamba watakaposoma na kupata elimu angalau ya stashahada au shahada moja wataweza kujitegemea na kujinasua katika makucha ya utumwa wa mwanaume.

Lakini kama ilivyosemwa ng'ombe wa maskini hazai. Wanawake wengi wamesoma lakini wamejikuta wamesoma katika kipindi ambacho tayari kuna wasomi wengi na uhitaji wao umekuwa mdogo.

Hofu imetamalaki. Kiburi cha kuona wangeweza kujitegemea kinayeyuka. Ukweli ni kuwa kwenye suala la uchumi na uzalishaji Mwanamke hana pumzi ya kutosha kukusànya utajiri nje ya kuajiriwa

Ni wanawake wachache sana ambao wana uwezo wa kuvumilia na ku-sustain kwenye mapambano ya maisha pasipo kuhitaji msaada wa mwanaume

Wengi huanza kwa mbwembwe lakini hawafiki mbali wanajikuta wakikata tamaa. Tunasema ngoma ya watoto haikeshi. Amesoma ndio lakini kama asipoajiriwa kwenye uchumi atakuwa sawa na yule asiyesoma.

Biashara ndogondogo zisizokua ambazo zinakabiliwa na pepo na tufani za changamoto huwafanya wanawake wasomi kuweka mpira kwapani au kurudisha mpira huo kwa kipa.

Bado ndoa itaendelea kuwa sehemu ya kitega uchumi kwa wanawake Duniani. Sio Afrika ni duniani hata hizo nchi zinazoitwa zimeendelea.

Wakati huo wanaume nao upataji wa elimu utachangia kwa kiasi kikubwa kuona hakuna umuhimu wa ndoa yaani kuajiri Mwanamke huku wakiona ni biashara au kuendesha kampuni isiyo na faida zaidi ya kunyonywa.

Zaidi tabia ya watoto wengi wakikua kuwapendelea Mama zao ni sababu nyingine ya vijana wa Gen Z kupinga kuishi kwenye ndoa.

Suluhu kwa wanawake itakuwa kuwageuza watoto kuwa vitega uchumi vyao baada ya Taasisi ya ndoa kudondoka na wanaume kukataa kuishi hata kinyumba na wanawake. Huku wanaume nao suluhu yao ikiwa ni kutoa child support tuu na kuwafanya wanawake wawe Watu wa kulalamika kutokana na ugumu wa maisha.

Changamoto itakuwa kwa wale wenye ndoa na wanaume wanaohudumia familia zao vizuri.
Wanawake wengi watajigonga na kupigania kuingia kama sio kuvunja kabisa ndoa hizo. Vijana watakuwa na pesa lakini hawatataka kuoa baada ya kugundua kuwa wanawake wengi huvizia pesa zao.

Na kitendo cha wanawake kutowataka wanaume wakati huo Wakiwa hawana pesa na baadaye kuwashobokea Wakiwa na pesa, kitakuwa ni red alert Kwa Vijana hao waliofanikiwa. Wengi watataka kuwa na watoto tuu.

Kauli ya tafuta pesa imelenga zaidi kuweka upendo na utu pembeni huku vita ya kuonyeshana uwezo wa kiutafutaji baina ya Mwanamke na mwanaume ikiwa Dhahiri.

Ingawaje mwisho wa pambano wanawake wataangukia pua na wachache kati yao watapatemo chochote kitu. Kifuatacho ni msemo kuwa Mwanamke ni chombo cha starehe kitarejeshwa na zama zitajirudia.

Watanunuliwa kimafungu kwa ukahaba. Watanunuliwa kimafungu na kuolewa Mitala kama zamani.
Kwa sababu upendo na utu hautakuwa kipaombele tena bali matokeo ya tafuta pesa yatajirudia ambapo zamani ni mwanaume lazima uwe na mali.

Mwisho wa siku Mwanamke atabaki kuwa Mwanamke na tegemezi daima dawamu. Na maskini ataendelea kuwa maskini daima dawamu. Ingawaje wapo Exceptional ambao ni wachache sana ambao wataweza kuvunja hiyo kanuni. Na msemo wa maji hufuata mkondo utaendelea kudumu.

Ijumaa Kareem

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kuna haja kubwa ya kukaa chini na kutangaza hali ya hatari kuhusu mabadiliko ya maisha na elimu itolewayo ni kama vile maisha yapo kasi zaidi kuliko elimu ndio maana kwa sasa elimu haitatui changamoto za kimaisha
 
Back
Top Bottom