Elisha Chuma
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 282
- 275
Katika mfumo wetu wa elimu kuna elimu muhimu inayokosekana na hakuna sehemu ya kuipata hadi uzinduke mwenyewe ambapo elimu hiyo ni elimu ya kujitambua,asilimia kubwa ya watu wanafeli katika,biashara,mahusiano,ujasiriamali na vingine vingi sababu kuu ni kutokujitambua,na bahati mbaya zaidi hufundishwi shuleni kujitambua unafundishwa kutambua hivyo unajikuta unatambua vingi ila wewe mwenyewe hujitambui.
Tatizo lililopo katika elimu yetu ni kwamba tunasoma kwa kufuata taratibu za watu fulani, mfumo wa elimu tunaotumia Ni wa mzungu , ili ujikomboe unatakiwa ujitambue, mzungu alileta elimu lakini haikuwa elimu ya kutufanya tujitegemee moja moja ilikuwa ni ili kuwasaidia kwanza katika shughuli zao wawepo wenye uelewa kidogo wa kuwasiliana na baadhi ya shughuli, Elimu tunayoipata kwenye shule zetu kuanzia ngazi ya chekechea hadi ngazi ya sekondari ni elimu ya lugha na kusoma,kuhesabu na kuandika, kama ni hivyo kwa nini basi tuendelee kupoteza muda wingi kusumbukia kuhesabu, kusoma na kuandika?
Wanafunzi wanachukua hadi masomo 14 yote ayafanyie mtihani na anatakiwa kufaulu ni uwezo wa hali ya juu unaotumika kwa wanafunzi wanaofaulu, na hicho hakikuwa kizazi cha dot.com ambacho kila kitu wanafunzi wanatumia Mbadala wa google kutafuta.hata kufeli sana kwa wanafunzi wetu kumesababishwa na mabadiliko ya hali ya utandawazi Nchini zamani ilikuwa ili ufaulu unajitahidi kujisomea sana na kujisomea kwenyewe ni kwa makatasi ya mitihani iliyopita na vitabu lakini sasa hivi hali ni tofauti hadi wanafunzi wa shule za msingi wameshakuwa watumwa wa kompyuta kila kitu wanajua kinawezekana hata wanaoshindwa wanajua google itawasaidia lakini. Waliofanya na kusoma kabla ya google walifaulu vipi?
Serikali imekazania sana masomo ya sayansi na hakuna sayansi wanayoisoma tofauti na historia ya sayansi, maabara zenyewe sio za kutosha lakini katika mtihani unatakiwa ufanye nadhalia na vitendo ni jambo gumu kwa wanafunzi wetu na katika hilo bado serikali inataka mtu ajitegemee atajitegemea kwa kitu gani iwapo mmeshamfanya awe tegemezi wa elimu ya kutegemea.
Mfano: Mwanafunzi akiwa msingi kapata elimu ya kusoma na kuandika hadi akamliza huku somo moja tu ndio anafundishiwa lugha ya kigeni, kaingia sekondari lugha inabadilika sasa ni somo moja tu ambalo anafundishiwa lugha ya nyumbani ( hapo tayari umeshamchanganya ni sawa na umemrudisha kuanza msingi wakati yuko sekondari) tena anachukua masomo 14 masomo yote hayo anatakiwa ayaweke kichwani mwake aidha yanamsaidia au hayamsaidii katika maisha ( wakati maana ya kusoma ni kupata elimu amabayo itakuja kukusaidia mbeleni katika maisha yako, kuna umuhimu gani kusoma masomo yasiyo kusaidia ).bila kumuandaa au kumpa machaguzi kulingana na atakachosoma
( mfano: CBG,PCB - Haya kwa upande wa sekta ya afya ,hkl,hgl - haya kwa upande wa lugha ) mwanafunzi anaanza kujichagulia bila kuwa na uchaguzi hivyo uchaguzi wake utafuata ashauri wa marafiki au kundi fulani , atachukua.
Hayo masomo na ataendelea nayo hadi chuo , lakini kutokana na kuwa hayakuwa katika mipangilio yake ya maisha ya baadae ndio unakuta mtu anadegree ya sheria ila anaomba kazi ya kuwa administrator.
Mitaala yetu haiwaandai sana wanafunzi kutambua tofauti iliyopo pale ambapo mtu akiwa shule, akiwa chuo, akiajiriwa na anapo jiajiri mwenyewe, hakuna elimu hiyo lakini baada ya kuona vijana wengi wanapotea sasa hivi vijana wanashauriwa wajiajiri watajiajiri vipi wakati hawana hata hiyo elimu ya ujasiriamali?
Inatakiwa watu wajitambue ilhali wakiwa bado wanauwezo wa kukunjika sio tayari wameshanyongorota ndio mnaanza kuwaambia wajinyooshe, elimu ya kujitambua inatakiwe itambulike kwa kila mtu kuanzia mtoto hadi mtu mzima ikiwa unajitambua hauwezi kukaa mtaani miaka nenda rudi bila kupata kitu cha kufanya kutokana na elimu uliyoipata lakini kwa sababu hajafundishwa kujitambua, muda wa yeye kujitambua anakuwa tayari anamajukumu mengine tayari hilo ni tatizo jingine,tunakimbilia sana kuwalaumu vijana vijiweni bila kutafuta kwanini kijiwe kimepata wanachama.
Ushauri wangu.
Yafaa serikali kuanzisha masomo au kuwe na vipindi maalum katika mtaala wa elimu kufundisha elimu ya biashara na ujasiriamali kwa wanafunzi wetu ili kujenga uwezo wa kujitambua hata wanapohitimu tayari wanakuwa wameshajitambua wako upande gani. Pia ushauri wangu serikali ipunguze masomo yasiyokuwa na umuhimu kwa mwanafunzi anapoteza muda mwingi kufanya yasiyo na manufaa katika maisha yake.
Mkate wa fani ni mkubwa tukiacha kila mtu achague bado hakuna fani itakosa watu.
Elisha Chuma.