Padone EPM
JF-Expert Member
- Jul 17, 2020
- 604
- 882
Habarii, Leo ningependa tujadili kuhusu Elimu itolewayo nchini Tanzania je? Inakizi viwango vya Dunia kulingana na utandawazi unavokuwa kwa Kasi na pia inawaandaa wahitimu kujiajiri au laa!.. Baada ya uhuru wa Tanganyika mnamo 1961 Chini ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilianzishwa Elimu maalumu ya kuwakwamua wananchi katika ujinga na kuwafanya kujitegemea.
Elimu hiyo ilitolewa kwa dhumuni la kuwaondoa katika ujinga na kuwafanya wajitegemee, hivyo basi ilihusisha mambo makuu matatu ambayo ni Kusoma kuandika na kuhesabu(KKK). Elimu hiyo ilijikita kuhakikisha Kila mwananchi ajue kusoma na kuandika kwaajili ya kushiriki katika maamuzi mbali mbali.
KUSOMA,KUANDIKA NA KUHESABU.(KKK)
1.Kusoma.
-Elimu hii ya kusoma ilijikita kuhakikisha wananchi wote wanajua lugha ya mazungumzo, Utambuzi wa sauti, Kusoma kwa ufasaha, Na pia matumizi ya misamiati mbalimbali.Wakufunzi walifanya kazi nzito sana kufanya watu kujua kusoma na hii ilikuwa njema sana.
2.Kuandika.
-Hii ilihusisha Uumbaji wa herufi,Matumizi ya Kanuni za uandishi na pia uandishi wa mwandiko hii mpaka sasa ina faida kubwa sana na inatumika na wanajamii wote.
3.Kuhesabu.
-Katika Hali ya kawaida kabisa mafunzo haya yamesaidia sana Taifa na wanajamii kwa ujumla hivyo kongole kwake Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kuhesabu kunahusisha Utambuzi wa namba mbalimbali na Utambuzi wa fedha.
Ukiangalia dhumuni kuu la kuanzishwa kwa hiyo Elimu maalumu ilikuwa sahihi na ilikizi mahitaji binafsi kwa kipindi hicho kutokana na uwepo wa Sayansi na Teknolojia Duni sana. Watu wengi kipindi hicho walijua kusoma kuandika na kuhesabu na iliwasaidia katika shughuli mbalimbali ikiwemo biashara, kusaini mikataba, kujua vipimo halisi vya ardhi,ujenzi, kutumiana ujumbe wa maandishi na mengineyo hivyo basi ilikizi mahitaji muhimu.
Mnamo mwaka 2015 Mtaala mpya wa Elimu ya msingi kwanzia darasa la kwanza adi darasa la Saba ulianzishwa na wizara husika Ili kuhakikisha utoaji wa Elimu inayokidhi mahitaji ya Mtanzania na yenye kutoa fursa sawa za kujifunza kwa wanafunzi wote. Mtaala huu ukiufuatilia kiundani zaidi haujatoa wazi wazi mtazamo wa wanafunzi wote kujiajili pindi wanapohitimu Elimu zao na wasifikilie suala la Ajira.
Yafuatayo ni sababu kuu zinazoelezea wazi wazi kuwa Elimu ya Tanzania haikidhi viwango vya soko la Dunia na pia haimuandai mhitimu kujiajili Moja kwa Moja bila kutegemea Ajira serikalini:-
i) Elimu itolewayo ni nadharia na sio Vitendo. Nchini Tanzania Elimu kuu itolewayo imesimamia asilimia kubwa kwenye nadharia na sio Vitendo mfano wa somo la Stadi za kazi unakuta wanafundisha masuala ya kutengeneza mikeka kwa maandishi tu pasipo kushiriki Moja kwa Moja kutengeneza kwa Vitendo kutokana na Mtaala mbovu na pia serikali haisapoti vipaji mbalimbali mashuleni kwa kuvipa vifaa maalumu kwaajili ya kufanya mazoezi zaidi.
ii) Ubaguzi. Elimu itolewayo vijijini na mijini ni tofauti kabisa kwa sababu mjini watafanya mazoezi ya Vitendo kwakuwa wamepewa vifaa ila vijijini wataishia kusoma kwa nadharia na ata pindi anapohitimu anakuwa hana uwezo wa kutumia kile alichojifunza kwa nadharia kukileta kwa njia ya Vitendo katika jamii.
iii) Elimu itolewayo haifundishi njia mbalimbali za kujiajili zimejikita katika kuajiliwa. Mfano Elimu mbalimbali zimejikita kufundisha jinsi ya kufanya kazi ukiwa chini ya Ajira na hifundishi ni mbinu zipi uzitumie katika kujisimamia mwenyewe.
iv) Kutokuwepo kwa shule za Sanaa na vipaji.kutokana na Dunia kuwa na mabadiliko makubwa Ajira nyingi zimejikita kwenye mambo ya Sanaa na vipaji katika Elimu ya Tanzania haijaweka mbele umuhimu wa kuvumbua vipaji na kukuza vipaji hivo hivyo basi haijakidhi vigezo na inafanya wahitimu wawaze kuajiriwa na sio kujiajiri kutokana na vipawa vyao.
v)Mitaala mibovu ambayo haimuandai muhitimu kujiajili Toka mapema. Mitaala Yetu nchini haikizi vigezo kabisa vya ushindani wa Dunia kwasababu haujiwekezi katika kuhakikisha wahitimu kujitegemea wao kwa wao kutokana na Elimu waliyopata.
Kutokana na sababu tajwa hapo juu zinapelekea Elimu ya nchini kwetu Tanzania kutokizi mahitaji muhimu ya wananchi hivo basi kama Serikali pamoja na wadau wakubwa wa Elimu yawapasa kujadili kwa undani zaidi kujua ni jinsi gani ya kutatua tatizo Hilo na kuwakwamua wananchi katika kufikiri Ajira na mbadala wake wajikite katika kujiajiri wao kwa wao kwa sababu kujiajiri kuna tija na pia kunaepusha Taifa kuwa na watu wasiojiweza kimaisha pia itasaidia sana kupunguza vijana wasio na Ajira ambao wanaweza kujiunga na makundi ya kiharifu.
Je? Kipi kifanyike kuhakikisha tunatoka katika dhana ya Elimu kwaajiri ya kuajiriwa na twende katika Elimu inayojikita katika kujiajiri?
Yafuatayo ni mambo makuu yakufuatwa Ili kuepusha dhana ya Elimu ni Ajira, na kuleta dhana ya Elimu ni kujiajiri:-
i)Marekebisho ya Mtaala wa Elimu nchini. Hii itasaidia sana endapo katika Marekebisho hayo yatajikita katika kuendana na utandawazi unavotaka, mabadiliko katika dhana ya kuajiriwa na kuwa ya kujiajiri masomo mashuleni yafundishwe kwa lugha stahiki na Vitendo stahiki Ili kuhakikisha mambo hayo yanaweza kufanyika katika mazingira ya kawaida.
ii) Elimu kutolewa kwa Vitendo hasa kuliko kwa maneno na maandishi tu. Mfano katika ufundishaji wa somo la Sayansi ujikite katika Vitendo zaidi kwakuwa kuna wanafunzi wanaweza kuwa na vipaji kuhusu labda umeme na ufundi wakisoma kwa Vitendo zaidi vinaweza kuwasaidia katika maisha ya kawaida ya kujiajiri.
iii) Kuanzisha Shule nyingi za vipaji na sanaa mbalimbali nchini. Hii itasaidia sana watu kuondoa dhana za kuajiriwa kwasababu kutokana na vipaji vyao mbalimbali wanaweza kujiajiri Dunia kote mfano mziki,ufundi,ujenzi,uundaji wa vifaa mbalimbali.
iv) Serikali kuinua na kuwezesha wahitimu. Endapo serikali ikijitoa kuhakikisha inasaidia wahitimu mitaji mbali mbali wahitimu hao watatumia mitaji hiyo katika kujiajiri kutokana na Elimu waliyosomea na kupunguza mzigo mkubwa ya wasioajiriwa nchini.
v) Serikali kuwezesha vifaa vya mazoezi Kila shule bila kubagua vijijini. Kwasababu vifaa ndo nyenzo kuu ya Elimu ya Vitendo hivyo basi shule zote ziwe na vifaa husika kuhakikisha mazoezi yanafanyika na pia hii itasaidia kujiajiri wao kwa wao wakihitimu.
vi) Wazazi wa wahitimu waache kuwawekea dhana watoto wao kuwa wakisoma wataajiriwa Bali wawaambie kasome kwaajiri ya kupata maarifa ya kujitegemea. Wazazi wengi nchini wamejikita katika kushawishi watoto zao kuwa kusoma ndo kuajiriwa na kuwafanya watoto wawe tegemezi kwa Taifa kutokana wanapohitimu watakaa kusubiri Ajira na sio kujiajiri.
vii) Kuandaa matamasha mbalimbali ya kutoa Elimu ya kujiajiri pamoja na faida zake mashuleni. Moja kwa Moja itasaidia kuwatoa wanafunzi katika dhana ya kusoma ni Ajira.
Viii)Kufungua Madarasa maalumu ya Elimu ya ujasiliamali. Hakika ujasiliamali unasaidia kwa kiwango kikubwa sana katika kutatua tatizo la Ajira Nchi nyingi Dunia ivyo basi katika Mtaala wa Elimu wa Tanzania ingeweka somo la ujasiliamali mbele zaidi Ili wahitimu waweze kujitegemea wenyewe.
Hitimisho:- hayo juu ni mawazo yangu binafsi hivyo basi inahitajika mikakati mikubwa inayohusisha serikali,wananchi na wadau wakubwa wa Elimu kuhakikisha wanaangalia upya suala la Elimu yenye tija kwa Kila mtu Asanteni.

Upvote
3