SoC01 Elimu juu ya chanjo, kitaalamu 'vaccine'

SoC01 Elimu juu ya chanjo, kitaalamu 'vaccine'

Stories of Change - 2021 Competition

Asha Hincha

Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
15
Reaction score
18
Salamu wanajukwaa.

Elimu juu ya chanjo, kitaalamu 'vaccine'

MAANA YAKE
Kwa ufupi, hizi ni biomolekuli ambazo hupewa mtu kwa lengo la kuupa mwili kinga ya kupambana na ugonjwa fulani. hivyo basi, chanjo si tiba bali ni kinga dhidi ya ugonjwa husika (ikimaanisha chanjo ni maalumu kwa ugonjwa mmoja), na hakuna uwezekano wa chanjo moja kufaa kwa ugonjwa zaidi ya mmoja.

Ipo kasumba katika jamii zetu ikiwemo kampeni za kuwa hamasisha watu kuwa chanjo ni miongoni mwa njama za nchi zilizo endelea kutaka kutuua waafrika. natoa mfano wa hali ya sasa nchini juu ya wimbi la maambukizi ya virusi vya corona.

Miongoni mwa fikra zilizotawala ni "wanaipigia debe corona ili wapate mikopo kutoka mataifa makubwa", "chanjo ni njama za mabeberu za kutaka kutuua".

Tufahamu, chanjo ni kitu cha kawaida kama zilivyo dawa za kutibu maradhi mengine, pia mfano mzuri zipo chanjo nyingine nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa kwa miaka mingi mfano chanjo ya homa ya ini, kichaa cha mbwa, tetenus na kadhalika

Tufahamu, hakuna kitu kibaya kama kuchanganya siasa na taaluma ya afya, taaluma ya afya ni sehemu ya sayansi ambayo huwezi kuiongelea kwa siasa siasa na mitazamo binafsi bali ni kwa tafiti tu, ambazo ndiyo zinaweza kuthibitisha kipi sahihi kipi sicho, kipi salama kipi hatari.

Hivyo ni jambo jema kuachia masuala kama haya ya kiafya wataalamu wetu wa afya ambao wame aminiwa na mamlaka husika watusemee.

Jambo jingine linalo chochea hofu ni uwepo wa matukio ya watu kupata matatizo ya kiafya baada ya kuchoma chanjo, tufahamu kama ilivyo kawaida kwa dawa nyingine unaweza kupata maudhi ya hapa na pale pindi utumiapo dawa, mfano kichefuchefu, kizunguzungu, uchovu na mengine makubwa kama matatizo ya figo, ini na kupoteza ujauzito(kwa wanawake wajawazito) , je ilishawahi kutokea watu wakasema sasa basi hatu tumii tena dawa yoyote ile ya kizungu, (kama wanavyoita) ?, hapana.

Hivyo basi ni sawa sawa kwa upande wa chanjo, unaweza kupata maudhi mbalimbali ya kiafya mfano mzuri ni anaphylaxis (kitaalamu) ambayo inaweza kuwa hatari mpaka kupelekea kifo (anaphylactic shock) na pia maudhi haya sio lazima kila mtumiaji apate hutegemea na mtu na mtu.

Kwa maana hiyo basi hatuwezi kuacha kutumia chanjo kwa sababu hizo tajwa.

Ni jukumu la wataalamu wa afya kufanya tafiti baada ya kuipokea chanjo kutoka sehemu fulani au nchi fulani na kuifanyia uchambuzi/utafiti (quality assessment and assurance) kama ni salama au lah! jambo ambalo hufanywa kwa dawa yoyote ile inapoingia nchini kabla ya kumfikia mtumiaji.

Pia ni jukumu la wataalamu wa afya kutoa uangalifu unaostahiki wakati wa utoaji wa chanjo kama inavyo fanyika kwa matibabu mengine mbalimbali.

Hivyo si suala la jamii au watu kuhofia na kupotoshana kuhusu hili.

Mfano swali ambalo nimewahi kukutana nalo katika mitandao ni 'tangu waanze kutumia hizo chanjo je ugonjwa umeisha?',

tufahamu, chanjo si tiba bali ni kinga ya kuuandaa mwili kupambana na ugonjwa pale utakapo pata maambukizi hivyo kupunguza kasi ya vifo na kasi ya maambukizi, kwa maana kama unapata maambukizi kisha vimelea vinakufa baada ya muda mfupi, basi huwezi kuambukiza mtu mwingine na baada ya muda ugonjwa utapungua au kupotea kabisa.

Mfano mzuri ni ugonjwa wa ebola baada ya kupatikana chanjo yake.

SHUKRANI.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom