PAULMATOLI
Member
- May 28, 2024
- 11
- 14
ELIMU KIDIGITALI
Elimu huweza kumsaidia mtoto kuweza kujitambua na kutambua mambo mengi yanayomzunguka, pia huweza kumsaidia mwanadamu kuishi kwa kukabilia na mazingira yake.
Elimu kidigitali ni elimu ambayo inatumia vifaa vya kiteknolojia katika kufundisha na kujifunza, vifaa kama vile kompyuta, simu, Televisheni na projekta
Elimu yetu ya msingi na sekondari inachukua takribani miaka 13 mwanafunzi akiwa shuleni lakini anatoka hapo na elimu ambayo haimsaidii kuweza kupambana na mazingira yake wala haimsaidii kupata ajira, jambo ambalo silifurahii zaidi ni mtoto kutumia muda mwingi kujifunza jambo lile lile kwa nadharia na picha mficho ambazo haoni vitu kwa uhalisia wakati tupo kwenye tecknolonia ambayo itamsaidia kurahisisha ujifunzaji na kujenga kumbukumbu za kudumu.
Mawazo ambayo natamani yatumike ili kuweza kuboresha ufundishaji na ujifunzaji na kujenga kunbukumbu, ari ya kujifunza na zaidi kufanya wanafunzi wajue kwa uhalisia kitu anachojifunza kikoje na imsaidie zaidi kuchagua kitu anachokipenda na kuweza kujifunza kwa undani zaidi jambo ambalo ni talanta yake kwakuwa atapata fursa yakuona kwa uhalisia mambo mengi kwa undani na uhalisia.
Tupo kwenye kizazi cha kidigitali hivyo na shule zetu ni vyema vitumia vifaa vya kidigitali kufundishia na kujifunzia. Napendekeza kila shule iwe na kompyuta moja na projekta au skrini kwaajili ya watoto kuona kwa uhalisia vitu wanavyofundisha darasani.
Mfano mtoto aone kwa uhalisia jinsi mfumo wa damu unavyofanya kazi au aone kwa uhalisia jinsi mlipuko wa volkano unavyotokea.
Naamini kabisa vifaa vya kidigitali vikitumika kwenye ufundishaji na ujifunzaji wanafunzi wengi watapenda shule, wataongeza ufaulu na kuweza kujua vitu wanavyopenda kufanya kwenye maisha yao na mwisho kufaulu vizuri.

Upvote
2