SoC02 Elimu kipofu

Stories of Change - 2022 Competition

EVANCIAN

Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
6
Reaction score
1
Na EVANCIAN.

Kwa miaka mingi sasa, tumekuwa tukiendelea kushuhudia uporomokaji wa viwango vya Thamani ya Elimu yetu ya Tanzania katika nyanja zote za Uchumi, Siasa, Jamii na Utamaduni ndani na nje ya Nchi. Licha ya jambo hili kuwa hatari sana, Juhudi za kulitatua zimekuwa chache sana na Serikali imezidi kukaa kimya ilhali Taifa linazidi kuteketea.

Jamii ya wasomi wa Elimu ya juu nchini imeongezeka na inaendelea kuongezeka mwaka Hadi mwaka lakini cha kusikitisha ongezeko hili badala ya kuisaidia jamii na Taifa kwa ujumla, wamebaki kuwa tegemezi kwa jamii zao na Taifa lao wakisubiri wapewe kazi/ajira za kufanya ndipo wainue Uchumi wao, Aibu gani hii!!!?

Muda wa kukaa kimya na kuacha mfumo wa nadhalia uliongoze Taifa umeisha, tuko huru kama Taifa na kama Nchi, tukae kama familia moja na tena wa historia moja, tubadili mfumo huu wa Elimu ambao hautufai tena,

Tuwatumie wataalamu wetu waliobobea katika tafiti, watafiti juu ya mazingira yetu, mahitaji yetu katika jamii, malighafi zetu tulizonazo na namna zinavyoweza kutatua mahitaji yetu na zaidi watafiti mbinu za kukuza sekta ya Kilimo ambayo ndiyo msingi wa kujitegemea kwetu, na baada ya kupata majibu sahihi ya tafiti hizi basi majibu hayo yawe dira ya kutuongoza kuandaa mitaala ya Elimu itakayotoa maarifa yenye kumuwezesha Mtanzania kuwekeza akili na maisha yake yote katika nyanja hizo ili kuibua ajira binafsi na kufanya dhana ya Elimu ya Kujitegemea na Kujiajiri iwe hai na ya kutekelezeka na hapo ndipo tutaweza kukata mzizi wa Utegemezi ndani ya Taifa letu ambao unasababishwa na Elimu hii Kipofu.

Naomba kuwasilisha ndugu zangu, Ahsanteni Sana!
 
Upvote 1
Ndugu zangu nawasalimu sana kwa Neema ya Amani tuliyonayo..,. Nawaomba ushirikiano wenu kwa kulipigia kura Andiko langu la ELIMU KIPOFU
Ndugu zangu nawasalimu sana kwa Neema ya Amani tuliyonayo.,. Naomba ushirikiano wenu kwa kulipigia kura Andiko langu la ELIMU KIPOFU hapo juu kwa kugusa mshale/alama ^ ili kwa pamoja tulijenge Taifa..... Ahsanteni Sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…