Lupembespeaking
New Member
- Jul 19, 2022
- 4
- 4
ELIMU YETU!
Hivi sasa elimu ni chombo chenye msaada mkubwa sana tofauti kabisa na ilivyochukuliwa hapo mwanzo wakati wa babu zetu kwani kwa baadhi ya watoto na jinsi ya kike ilionekana kuwapatia elimu ni suala la ajabu wakati Sasa tunaenda na kaulimbiu ukimwelimisha mwanamke umeelimisha jamii nzima pamoja na kusema urithi pekee kwa mtoto ni elimu.Elimu hasa kwa Nchi Kama Tanzania imebeba hatima za vijana wengi ambao wanatamani kufikia ndoto zao kupitia tasnia hii adhimu.
Wadau wa elimu mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha usajili wa watoto kuanza shule na hata kupiga vita suala la watoto kutopatiwa elimu Bora.Pamoja na jitihada zinazofanywa lakini bado zipo changamoto nyingi ambazo zinakwamisha ama kwa hakika kufanya elimu inayotolewa nchini mwetu kutokuwa na manufaa mapana hasa kwa wanufaika wa elimu hiyo. Serikari yoyote iliyoendelea ulifanya jitihada kubwa hasa katika elimu kwa vijana tena si elimu tu ni elimu endanifu kwa wakati husika (relevant education). Jamii yoyote inayotoa elimu ambayo si endanifu ni lazima ipate anguko kubwa hasa katika maendeleo yake pamoja na ukuaji wa kinyanja.
Suala la utoaji elimu bora na endanifu ni suala la msingi ambalo halihitaji kuwekewa siasa hata kidogo .Yapo mambo mengi ambayo elimu yetu kwa kiasi kikubwa haijazingatia kwa ufasaha hasa kutegemea mifumo ya kijamii pamoja na mabadiliko yake (Ulimwengu huu wa sayansi na tekinolojia).
Kutokana na changamoto wanazopata wahitimu/ wanufaika wa elimu hii ni vema utoaji wa elimu ukazingatia mambo makubwa matatu ;
Mfumo wa Nchi
Wakati (kipindi jamii inapitia na inachotarajia)
Mahitaji ya Nchi na mwenendo wa umataifa.
Pamoja na uzingativu wa mambo hayo matatu elimu inahitaji kujiambanua na kuzalisha wasomi ambao wataenda kutumika moja kwa moja kwenye taasisi zenye uhitaji. Pasipo na uzingativu wa mambo hayo matatu jamii ni lazima ikubaliane kupata anguko kubwa na kupata vilio vya watu wasio na ajira wengi kwani hawaendani na mahitaji ama vipindi ambavyo jamii inapitia kwa wakati husika.
Kama Taifa tunahitaji kufikiria kwa makini na kuona ni namna gani tunaweza kuzalisha wasomi kupitia elimu yetu hasa kwa kuzingatia Nchi inataka nini? mifumo ya ndani ya Nchi inataka nini? Vinginevyo tutaendelea kutoa elimu ambayo haimsaidii kijana anayeipata wala Nchi yenyewe.
Tunahitaji kupata mtaala mpya hasa kwenye elimu yetu. Ni dhahiri kuwa mitaala tuliyonayo hivi Sasa haikidhi mahitaji ya Nchi hivo basi ni vema mitaala yetu ikabadilishwa pasi na upepesaji wa macho juu ya nani wa kuanzisha vuguvugu hili. Siasa hazihitaji kuwekwa hasa katika suala hili la ubadilishaji was mitaala kwani ni suala ambalo limebeba hatima ya Nchi na wananchi wake. Wadau wa elimu wanapaswa kukaa pamoja na kuweka mada jadilifu mapema hasa juu ya nini kiondolewe na nini kipunguzwe kwenye mitaala yetu ya elimu inahitaji kufanyika mapema.
Ni vema mfumo wa elimu ukawekwa kwa namna ambayo inaendana na sayansi na tekinolojia.
Wakati taasisi nyingi za kielimu zikiwa zinaendela kutoa elimu kwa wanufaika hali ilikuwa tofauti hasa kwa mataifa Kama Tanzania kwani hakukuwa na mfumo wezeshi wa kuwafanya watu kupata elimu wakati wa janga kubwa la Corona (Covid-19). Hii yote ni kutokana na kuendekeza uzamani hasa katika utoaji wa elimu pasipo kuhusianisha elimu yetu na maendeleo ya sayansi na tekinolojia. Kujifunza pasipo na mgusano wa Moja kwa moja ni suala la kutiliwa mkazo kwani hivi sasa Ulimwengu ubadilika na watu wake wanapaswa kubadilika.
Uboreshwaji wa miundombinu ya kielimu ni suala ambalo linapaswa kuwekewa mkazo, ni dhambi kwa watoto kupata elimu chini ya mti kwa zama hizi, ni uonevu mkubwa kwa watoto wetu kukaa chini hasa katika zama hizi za utandawazi. Ni lazima kuweka mifumo shindani katika mazingira ya mijini na vijijini shule iwe ni mahali pa mapumziko pia kwa watoto wanaotoka kwenye mazingira magumu na si sehemu ya kuendelea kuwapa machungu hasa kwa kukaa kwao chini, kusafiri kwa umbali mrefu kwenda shule hii inahitaji kubadilishwa na kuweka miundombinu wezeshi katika elimu yetu.
Elimu yetu iondokane na ufundishaji kwa kutumia nadharia kwenye zama hizi zinazohitaji ufanisi katika utendaji zaidi (less theoretical and more practical). Tafiti nyingi zinaonesha kuwa vijana wengi wanamaarifa ambayo hawawezi kuyaweka kwenye vitendo na hii ni kutokana na athari za elimu nadharia wanayopata pindi wanapokuwa mashuleni. Ni dhahiri kuwa vijana wengi waliosoma wamejaza nadharia katika vichwa vyao ambazo hazina msaada wowote na kusababisha utengemezi kwa serikari ambayo haiwezi kuajiri watu wote waliopata elimu. Ni dhambi kubwa kuwafundisha watoto wetu namna ya kulina asali pasipo kuwapeleka kwenye maeneo ya utendaji na kujifunza kwa vitendo.
Elimu yetu, elimu yetu izalishe wasomi kwa kuzingatia mahitaji tu na so vinginevyo, ikiwa ni marubani wazalishwe kutegemea mahitaji, mapinduzi yoyote kwenye sekta ya viwanda, biashara, ubunifu yote haha yanategemea kwa kiasi kikubwa Ni aina gani ya elimu vijana wameipata kutoka kwa Nchi yao.
Taifa kwa kushirikiana na wadau wa elimu wanapaswa kukaa na kuumiza vichwa juu ya namna ya kuisaidia elimu yetu kwa mambo pendekezwa ili Taifa lisipate watu tegemezi kwa serikari. Ni lazima ifike wakati Taifa lihusike kwenye kujenga mazingira wezeshi ya ufanyiaji mazoezi ya vilivyopandikizwa kwa vijana wetu na si kujibu maombi ya ajira tu.
Mungu ibariki Nchi yangu!
Makala na,
Jobless Kaini

Upvote
2