SoC02 Elimu kwa vitendo ni msaada kwa vijana wa Tanzania

SoC02 Elimu kwa vitendo ni msaada kwa vijana wa Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Kiepo

New Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Serikali inaweza kupunguza lawama za ajira.

Na Kiepo Benedicto.

Huzuni inatanda kadri siku zinavyozidi kwenda. Vijana wengi wanahitimu masomo yao ya elimu ya juu na hawajui hatima zao. Imekuwa ni kama utararibu wa maisha ya mfumo wa elimu yetu kuanza darasa la awali hadi chuo kikuu na kumuacha kijana huyu hawezi hata kujitegemea.

Ndio kijana hawezi kujitegemea, yeye ameandaliwa kwa namna ya kujua kuwa akimaliza masomo basi anaenda kuajiriwa moja kwa moja. Na kimsingi toka akiwa mdogo ameshaandaliwa ndoto ya kuifikia, kwa wale wanaotokea kanda ya kusini utamsikia mtoto anasema anataka kuwa mwalimu matokeoa yake anahitimu na hata hiyo taaluma anakosa kwa kuipeleka.

Ukikatisha vijiweni kila siku vijana wanaitupia lawama Serikali yetu, kwa mdai haitoi nafasi ya wao kupata ajira. Hapa panavutia sana. Je ni maelfu mangapi ya wanafunzi wanahitimu masomo ya ngazi ya juu kila mwaka? Je serikali inamudu kutoa nafasi ya kwa maelfu yote hayo ya vijana?

Jibu litakuja hapana. Sasa jiulize pia je ni haki kwa vijana hao kuendelea kuitupia lawama serikali? Jibu ndio kila sababu ya kuitupia lawama Serikalikwa sababu serikali ndio inayowajibika na mifumo iliyotumika kuwaandaa na kuwakuza vijana hao kielimu. Mfumo wa elimu wa Nchi yetu haumuandai kijana kujitegemea bali unamuandaa aje kutegemea kuajiriwa.

Hata kama Serikali yetu ingekuwa na wizara nyingi kiasi gani, ukweli ni kwamba kuna idadi kubwa sana ya vijana wanaohitimu masomo ya elimu ya juu kila mwaka, sidhani kama kwa namba hiyo ya vijana Serikali inaweza kuwafanya vijana wapate nafasi za ajira.

Hapa ndipo unapopata kumbukumbu kuwa tunaweza kuwa na njia mbadala za kusaidia wimbi hilo la vijana. Vinginevyo, tutaishia kuwasisitiza vijana hawa wajiajiri wakati hatujawawezesha wao kufanya hivyo.

Lile somo la stadi za kazi, walilolianzisha walifikiria sana lakini usimmamiaji wake haujatoa faida kwa wanafunzi wa Nchi yetu. Ni wazi wanafunzi wengi wanasoma kwa nadharia pekee bila kuwa na vitendo. Kijana alisoma kilimo ni nini, lakini hajui hata kuandaa eneo la kufanyia kilimo.

Ile miaka ya zamani elimu ilipokuwa ya vitendo, ilisaidia kumsaidia mwanafunzi ahitimu masomo yake akiwa hodari sana katika shughuli mbalimbali, zikiwemo kilimo na ufugaji. Elimu hii ya nadharia ilipoingia na kutawala iliwafanya vijana wengi kushindwa kuwa na uwezo wa kufikiria nje ya boksi badala yake wamekazania kuajriwa.

Wakati hayati Mwalimu, Julius Kambarage Nyerere anasisitiza ujamaa na kujitegemea, alilenga kuandaa kizazi bora, kizazi ambacho kitapambana kwa ajili ya kuijenga nchi baada ya Uhuru. Hebu fikiria katika hali ile ya ugumu wa maisha baada ya Uhuru bila ujamaa na kujitegemea hali ingekuwaje? Kipindi kile ndo kwanza nchi ilikuwa inapambana kujiimarisha zaidi.

Kwa kawaida yale mawazo ya kujitegemea yaliyowasaidia ndugu zetu kipindi kile, zinafaa kurudishwa kwenye elimu yetu ya hivi sasa. Ili tuweze kupata vijana waliohitimu na sana uwezo wa kujitegemea tunaihitaji ile elimu kwa Mara nyingine tens.

Iko haja sasa ya kuanzisha masomo ambayo yatamfanya kijana huyo kuhitimu akiwa anajua anaenda mtaani kufanya nini, kwani yatakuwa amehitimu na ujuzi. Ingependeza zaidi masomo hayo mwanafunzi ayasome kila hatua yake ya elimu anayopitia. Kimsingi kama alianza kufundishwa ufungaji toka akiwa hatua ya awali, basi atakuwa anamaliza masomo hayo akiwa na ujuzi mkubwa.

Zama hizi tuna bahati kubwa sana, kwani watoto wanaanza kusoma wakiwa na umri mdogo sana. Sio siri ni rahisi kumuandaa mtoto huyo kwenye ujuzi fulani mpaka pale atakapokuwa mkubwa atakuwa tayari ameirika tayari na ujuzi Fulani. Pengine itatupa nafasi ya kupata wataalamu bora sana kwa sababu watakuwa waliandaliwa toka akili zikiwa changa.

Kama ikitokea siku taifa lina watu wengi wenye ujuzi wa kilimo na uvuvi wa kisasa, mafundi seremala, na ujuzi mwingineo, basi wimbi hilo la watu wenye ujuzi litaenda kufungua hali ya ushindani kwenye Nchi yetu kiasi cha kupelekea mazao bora kutoka ndani ya Nchi yetu. Hapa itakuwa imewasaidia vijana na taifa pia kiuchumi.

Nafahamu ya kwamba kuna vyuo vya ufundi (VETA) kuna watanzania wengi wanavitumia vyuo hivyo kupata ujuzi katika fani mbalimbali. Lakini kunahitajika maboresho kadhaa kuweza kufanyika ili kufanya VETA iwe na msaada mkubwa.

Fikiria kijana aliyemaliza kidato cha nne, toka akiwa darasa la awali alikuwa anapata ujuzi fualani, sasa anavyoenda VETA anaenda kuongeza ujuzi zaidi na kumfanya awe bora sana katika ujuzi ule anaousomea.

Kama vijana wengi watakuwa na ujuzi fulani, kuna nafasi kubwa ya kupata matokeo juu ya fani hizo. Ushindani utaongezeka na kufanya watu watumie ujuzi wao kuzalisha bidhaa bora sana. Uzalishwaji wa vitu hivyo bora utachagizwa na vijana kubwa wabunifu zaidi ili kupata kitu kitakachouza zaidi ujuzi wao. Hadi hapo kijana atailaumu vipi Serikali?

Nchi yetu imebarikiwa rasilimali nyingi sana ikiwemo miti. Ni aibu kubwa kusubiria au kununua samani za ndani nje ya Nchi ilihali tuna nchi yenye neema ya rasilimali. Vijana wenye ujuzi wataenda kutusaidia vizuri pia namna ya kuzitumia rasilimali hizo.

Mfumo wetu wa elimu bado unakosa kuwa msaada kwa vijana wetu. Vijana wanaandaliwa kwenda kuajiriwa badala ya kujiajiri ilihali nchi haina uwezo wa kumudu wimbi hilo la vijana.

Tusipowasaidia hawa vijana, tutaendelea kuwa na taifa la vijana wengi waliowekeza nguvu zao kwenye mitandao ya kijamii na sio kulijenga taifa.

Wanafunzi wa chuo cha VETA Chang'ombe wanaosoma kozi ya uchapishaji (printing) wakiwa katika mafunzo kwa vitendo. Picha na VETA Chang'ombe.
 

Attachments

Upvote 0
Back
Top Bottom