SoC02 Elimu kwa wazazi/walezi juu ya malezi yenye ulinzi na usalama kwa watoto

SoC02 Elimu kwa wazazi/walezi juu ya malezi yenye ulinzi na usalama kwa watoto

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Jul 31, 2012
Posts
9
Reaction score
6
Ulinzi na usalama kwa watoto ni jambo ambalo jamii yetu ya sasa hailichukulii kwa uzito mkubwa licha ya kusikia katika vyombo vya habari, asasi za kutetea haki za watoto pamoja na kushuhudia wenyewe katika jamii zetu jinsi ulinzi na usalama kwa watoto ulivyo mdogo katika kizazi chetu cha sasa na madhara makubwa wanayoyapata watoto ikiwa ni pamoja na madhara ya kimwili na kisaikolojia.

Kwa kipindi cha hivi karibuni tumeshuhudia katika vyombo vya habari vinavyoripoti visa vya ukatili na unyanyasaji vinavyofanya kwa watoto ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kimwili (kupigwa, kusababishiwa ulemavu wa kudumu au kuuwawa), ukatili wa kingono (kubakwa na kulawitiwa) pamoja na kuumizwa kisaikolojia (kufetheheswa na kuaibiswa mbele za watu).

NI WAPI TUNAPOKOSEA?
1. Wazazi/walezi kutokuzingatia na kufuatilia kwa ukaribu usalama na ulinzi wa watoto
kutokana na kujikita zaidi katika shughuli za kupata kipato kwa ajili ya familia. kutokana na kubanwa na shughuli za kila siku mzazi/mlezi anashindwa kutenga muda wa kukaa na kuongea na watoto na kujua changamoto ambazo mtoto amekumbana nazo kwa siku hio.

2. Wazazi/walezi kuwa wakali sana kwa watoto hali inayomfanya mtoto kuogopa kumuelezea mzazi changamoto aliyokutana nayo siku hio. Mfano mtoto ataogopa kusema kama kuna alimshawishi kufanya ngono akihofia mzazi akisikia hio habari anaweza kumuadhibu.

3. Kukosekana kwa elimu kwa wazazi juu ya namna ya kuwalea na kuwalinda watoto. Elimu juu ya usalama kwa watoto haifundishwi shuleni kwa ajili ya kuandaa wazazi bora wa kizazi cha baadae. hii hupelekea kuandaa kizazi kisichojua namna bora ya kulea na kuwapatia watoto ulinzi hali ambayo hupelekea kuzalisha kizazi kilichoharibika kiafya, kimwili na kisaikolojia.

ATHARI ZITOKANAZO NA KUKOSEKANA KWA MALEZI YENYE ULIZI KWA WATOTO
1. Watoto kupata ulemavu wa kudumu kutokana na kupigwa kupitiliza. mtoto anaweza kupigwa hadi kupata ulemavu wa miguu mikono, makovu ya kudumu n.k. Pia wanaweza kufanyiwa ukatili wa kuchomwa na pasi, maji ya moto n.k
Aina za ukatili wanaofanyiwa watoto, wanawake – 4 - Mtanzania


2. watoto kupata madhara ya afya akili (psychological effects). Mtoto anapobakwa au kulawitiwa hupata tatizo la kisaikolojia kuhusu kitendo hicho ambapo tatizo hili ataendelea nalo hata atakapokuwa mtu mzima

3. watoto kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya ukimwi (VVU). watoto wanapokuwa wanacheza pamoja na watoto wa jirani ni rahisi kuambukizana magonjwa ya zinaa kwani kwa kizazi cha sasa watoto wamekuwa wakijifunza ngono wakiwa wagogo. hii hupelekea mtoto kuambukizwa magonjwa
4. watoto kushindwa kufanya vizuri kitaaluma pale wanaponyanyaswa. Mtoto anayenyanyaswa huwa wakati wote anakuwa na msongo wa mawazo hali ambayo humfanya ashindwe kufanya vizuri kitaaluma
5. Mimba za utotoni na watoto kukatisha masomo. mtoto kuanzia miaka 10 na kuendelea anaweza kubeba ujauzito. ikitokea mtoto akabakwa, anaweza kubeba mimba za utotoni.

NINI KIFANYIKE ILI KUIARISHA ULINZI NA USALAMA KWA WATOTO?
1. Kuwepo na programu za kutoa elimu ya malezi na usalama kwa watoto katika vituo vya redio, runinga na kuchapwa katika magazeti na katika mitandao ya kijamii ili kutoa elimu ya malezi na ulinzi kwa watoto kwa jamii nzima.

2. Wazazi na walezi kutenga muda na kukaa na watoto ili kusikiliza changamoto zinazoweza kuwaweka katika hatari ya ulinzi wao na kuwafundisha namna ya kuzitatua. hii ni pamoja na kuwasikiliza na kuwafundisha jinsi ya kuepuka mazingira hatarishi.

3. Jamii kutoa taarifa za ukatili kwa watoto katika dawati la jinsia na ustawi wa jamii ili watoto wapate msaada wa kisheria pale wanapofanyiwa unyanyasaji wa kimwili kama vile kubakwa, kulawitiwa, kupigwa kupita kiasi na kadhalika. Ili kuwesesha jambo hili kuwa rahisi, kila ofisi za dawati la jinsia na ustawi wa jamii linapaswa kutoa namba maalumu kwa ajili ya kuripoti matukio hayo.

IKUMBUKWE KUWA.
Watoto hawana mtu wa kuwasemea ili kupata haki zao pale wanapopata ukatili zaidi ya sisi jamii tunaowalea watoto hawa kutoa taarifa mara moja katika vyombo husika.

Kinachosikitisha zaidi ni kwamba watoto hawa hufanyiwa ukatili na watu wao wa karibu wanaowaamini kama vile mzazi, mjomba, binamu, ndugu au jirani. pale inapogundulika, taarifa za mhalifu hufichwa wakihofia huyo aliyetekeleza kitendo hicho ikigundulika itakuwa ni aibu kwa familia au itawaletea lawama kwa kuhukumiwa kifungo gerezani ikiwa ni ndugu.

Mimi kama mdau wa kutetea haki za watoto napenda kuwashauri jukwaa hili la jamiiforum kuanzisha mdahalo wa namna ya kuwalinda watoto na uwe wa mara kwa mara ili jamii tuweze kushauriana njia gani salama zaidi ya kulea na kuwapa ulinzi watoto wetu,

KAMA TUNAWEZA KUANDAA KURASA ZA KUJADILI MASUALA MBALIMBALI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII, INASHINDIKANAJE KUANDAA UKURASA KWA AJILI YA KUTOA ELIMU YA NAMNA BORA YA KUWAJENGEA WATOTO ULINZI NA USALAMA WAO?

TUTAFAKARI PAMOJA NA TUCHUKUE HATUA,

Imeandaliwa na , Amedeus Mathew
Contacts 0742280628/0625646050
 
Upvote 1
Back
Top Bottom