Walker Water
JF-Expert Member
- Aug 23, 2022
- 842
- 3,357
Katika jamii na taifa lolote lile haipingiki kuwa elimu inasimama kama moyo au injili.Hili linajidhihirisha wazi kutokana na uwezo wa elimu kumtengeneza mtu kihaiba,kijamii,kihisia na kimaono.Lakini elimu hii pasipo kugeuka kuwa maarifa inakosa maana na kuwa mzigo mzito kwa mtu binafsi,jamii na hata taifa kwa ujumla.Ili elimu hii igeuke maarifa na kuwa faida,napendekeza mambo yafuatayo.
Moja;Elimu hii itolewe kwa lugha ya kiswahili kuanzia elimu msingi hadi chuo kikuu ili kuwapa wanafunzi uwanja mpana wa kubuni,kufikiri na kuvumbua mambo mbalimbali kwa urahisi kutoka kwenye mazingira yao. Lugha ya kiingereza napendekeza ifundishwe kama somo la kawaida,na ili somo hili lieleweke kwa urahisi na kwa haraka,tunaweza kununua mbinu za kufundisha somo hili toka kwa watu wenye uzoefu na kuziingiza kwenye mfumo rasmi,mfano mbinu za "Rasi Simba".
Mbili;Napendekeza elimu ya awali na msingi itolewe hadi darasa la sita.Elimu ya sekondari itolewe hadi kidato cha nne.Elimu ya kidato cha tano na sita iondolewe na badala mwanafunzi akimaliza kidato cha nne ajiunge moja kwa moja chuo cha kati kulingana na fani yake aipendayo. Elimu ya chuo kikuu itolewe kwa miaka minne na kwa vitendo ili kukazia uzoefu na umahiri mtu alioupata kwenye chuo cha kati. Tatu,napendekeza masomo na namna ya usomaji uwe kama ifuatavyo;
Awali,la kwanza na la pili wafundishwe masomo manne tu,ambayo ni kusoma,kuhesabu,kuandika na nyimbo.Hapa kwenye somo la nyimbo napendekeza ziwe nyimbo zote zinazohusu afya,mazingira,jamii,siasa ya nchi na uzalendo.Kuanzia darasa la tatu hadi la sita masomo haya yote ya hisabati, english, kiswahili, maarifa ya jamii,uraia na maadili,stadi za kazi na sayansi na teknolojia yaendelee kufundishwa hivihivi, isipokuwa liongezwe somo lingine la "Muda na fedha" ili kuwafundisha wanafunzi umuhimu wa kuzingatia muda na faida na hasara zinazotokana na matumizi ya fedha.
Baada ya mwanafunzi kufika darasa la sita nashauri apewe mtihani wa taifa wa kupimwa na baada ya matokeo kutoka,nashauri mzazi/mlezi wa mtoto wakae pamoja na mwalimu na mtoto na kumpa mwanafunzi uhuru wa kuchagua masomo ayatakayo kulingana na ndoto zake kwa kuzingatia matokeo yake na ushauri wa mwalimu na mzazi/mlezi.
Baada ya mwafunzi kuchagua masomo hayo yatumwe wizarani na wizara impangie mwanafunzi shule ya sekondari kulingana na masomo na ndoto zake.Mwanafunzi akimaliza kidato cha nne aruhusiwe kuendelea na chuo kati kwa miaka miwili kulingana na ndoto zake ili kuimarika zaidi.
Mwisho napendekeza baada ya mwanafunzi kumaliza chuo cha kati aruhusiwe kujiunga chuo kikuu kulingana na fani yake kwa ajili ya kwenda kufanya vitendo vya ndani zaidi kulingana na fani yake na hii kupelekea kuwa mbobezi na mahiri na aliyejaa maarifa katika fani yake.
Kumbuka hakuna binadamu yeyote asiyekuwa na akili sema tunatofautiana vipawa tu.

Upvote
3