Kwa ufahamu wangu hizi shule zimekuwa na kamaati inayoitwa kamati ya wazazi, nasema inasemekana kwa kuwa sijui hata zinachaguliwaje. NImekuwa mteja wa hizi shule kwa kitambo sasa, kila siku utasikia kamati ya wazazi imeamua tupandishe kiasi fulani ili kufidia gharama za uendesahaji. Hizo gharama ni kiasi gani utajulishwa, na zimefikaje huko pia hutajulishwa. Kasoro kubwa ni wizara ya elimu, kuna kitengo maalum kinachoshughulika na hizi shule, kanafanya nini hata haijulikani. Maana hizi shule ziko huru sana kufanya zinazotaka, kana wakati moja ya shule hizi ilituahidi kama serikali ikiwapunguzia kodi nao watashusha bei. Cha kushangaza ndio ikapandisha hata baada ya serikali kushusha kodi, na hakuna aliyewauliza kulikoni.