mrlonely98
Member
- Nov 6, 2009
- 95
- 19
Asalaam jamani kuna swali nataka niulize tunasikia kwamba zipo shule nyingi za private ambazo zinapandisha bei ya elimu kila mwaka je nini kinafanyika kuzuiahili itafika wakati hatutaweza kubeleka watoto wetu kupata elimu bora
Kwa ufahamu wangu hizi shule zimekuwa na kamaati inayoitwa kamati ya wazazi, nasema inasemekana kwa kuwa sijui hata zinachaguliwaje. NImekuwa mteja wa hizi shule kwa kitambo sasa, kila siku utasikia kamati ya wazazi imeamua tupandishe kiasi fulani ili kufidia gharama za uendesahaji. Hizo gharama ni kiasi gani utajulishwa, na zimefikaje huko pia hutajulishwa. Kasoro kubwa ni wizara ya elimu, kuna kitengo maalum kinachoshughulika na hizi shule, kanafanya nini hata haijulikani. Maana hizi shule ziko huru sana kufanya zinazotaka, kana wakati moja ya shule hizi ilituahidi kama serikali ikiwapunguzia kodi nao watashusha bei. Cha kushangaza ndio ikapandisha hata baada ya serikali kushusha kodi, na hakuna aliyewauliza kulikoni.
Tatizo ni kwamba Wizara husika imelala usingizi mzito na kuacha mambo yakiendeshwa kienyeji bila hata kutathmini kwamba upandishaji wa fees unastahili kutokana na sababu zilizotolewa na kamati za wazazi kwa kushirikiana na uongozi wa shule.
Ingeweza kuwekwa hata percentage fulani kwamba fees zisipandishwe zaidi ya asilimia 3 au 5 kwa mwaka na wafanye hivyo baada ya kutoa sababu za kuridhisha zitakazokubalika na Wizara ya Elimu, lakini imekuwa ni bora liende tu kila mwaka mpya ukiingia wanapandisha fees wakati mishahara ya wazazi wengi haikuongezeka. Ndiyo nchi yetu hiyo mambo shakalabaghala!
Asalaam jamani kuna swali nataka niulize tunasikia kwamba zipo shule nyingi za private ambazo zinapandisha bei ya elimu kila mwaka je nini kinafanyika kuzuiahili itafika wakati hatutaweza kubeleka watoto wetu kupata elimu bora
Asalaam jamani kuna swali nataka niulize tunasikia kwamba zipo shule nyingi za private ambazo zinapandisha bei ya elimu kila mwaka je nini kinafanyika kuzuiahili itafika wakati hatutaweza kubeleka watoto wetu kupata elimu bora
sina uhakika kama una mtoto unaemsomesha kwa ada ya uhalali, vinginevyo ya kifisadi, au umetuma post hii ukiwa umechoka kutokana na kazi yako ya ukuliElimu bora na bei poa? Hivi vitu haviendi sambamba. Ili elimu izidi kuwa bora bei inabidi zipande kufidia vifaa, walimu na mazingira bora. Cha muhimu hapa ni kuwa na choice.
kwengine hapagusiki. 😛
International School of Tanganyika, IST
Fee Schedule 2009/2010
Early education USD 10300
Kindergarten USD 11900
Grade 6-8 USD 14600
Grade 9-10 USD 15700
Grade 11-12 USD 20000
http://www.istafrica.com/downloads/admission09-10/Fees Schedule & guidelines SY 2009-10.pdf