Elimu na Maarifa kuhusu Ulinzi wa Kidigitali (Digital Security)

Elimu na Maarifa kuhusu Ulinzi wa Kidigitali (Digital Security)

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Ulinzi wa Kidigitali ni nini?

Ni Ulinzi na Usalama wa Vifaa na Mifumo ya Kidigitali. Somo hili ji kutokana uwepo wa matukio ya kila siku yanayohusisha mashambulizi na kuingiliwa kwa Vifaa vya Kidigitali na Mifumo yake

Maendeleo ya Teknolojia yamebadili namna ya uendeshaji wa mambo katika jamii na matumizi ya Vifaa vya Kidigitali na Mtandao wa Intaneti ‬yameongezeka kwa kasi.

Hata hivyo, ziko hatari kadha wa kadha zinazowanyemelea watumiaji wa mifumo ya kiditali‬Baadhi ya hatari hizo ni pamoja na shambulizi la Nywila, shambulizi la Barua Pepe, shambulizi la 'DDoS', shambulizi la Virusi, Udukuzi, Wizi wa Fedha n.k

Je, unazijua njia za kujilinda?

Baadhi ya njia kujikinda ni kuweka Nywila (Password) kwenye vifaa vyako, hakikisha vifaa vyako vyako pamoja na Mifumo yake na Programu Tumishi (Application) ziko Katika Sasa 'Updated'

Nyingine ni kuhakikisha unatumia Programu zilizothibishwa kuwa ni salama, hakikisha unatumia 'Anti-Virus' iliyoidhinishwa, epuka kufungua Kiunganishi (Link) usichokitambua. Fanya 'Setting' za Kiusalama kwenye Barua Pepe, Simu na Kompyuta yako

Nywila (Password) ni Nini?

Nywila ni mfano wa Ufunguo wa Kidigitali unaotumika kufungua milango ya akaunti na taarifa zilizohifadhiwa katika mifumo na programu za Kigitali

Nyila hupaswa kuwa siri ya mmliki au wamiliki kwasababu nywila ni ulinzi namba 1 wa taarifa na faragha za mtumiaji wa vifaa na mifumo ya kidigitali

Nywila ina umuhimu mkubwa lakini inapaswa kutengenezwa vizuri ili isiwe rahisi kudhaniwa, kuhisiwa na kukisiwa

Nywila bora huundwa kwa kutumia, herufi kubwa na ndogo, namba, na alama na ni lazima iwe ndefu (herufi 16) na ya kipekee
 
Upvote 1
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom