SoC03 Elimu na mapana yake

SoC03 Elimu na mapana yake

Stories of Change - 2023 Competition

Hyper_Think

New Member
Joined
Jan 1, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Nikisukumwa na uhalisia katika jamii za kitanzania. Imekuwa ni desturi kutazama ajira kama mkombozi pekee baada ya kuhitimu ngazi fulani ya elimu hususani katika fani mbalimbali. Hii inatengeneza malalamiko yasiyo na suluhisho kila kukicha ilihali mtu anaweza akafikiri na kuelekeza msukumo zaidi katika nyanja binafsi ili kujikwamua na changamoto hususani ya ajira.

Moja kati ya vitu vya msingi tunavyojifunza madarasani ni namna ya kutatua tatizo moja kwa namna tofauti tofauti ndo maana kama mtu anasoma masomo ya hesabu basi atajua kama unakuwa na kanuni elekezi moja ila njia tofauti na zinaleta jibu moja na hiyo ndo maana halisi ya maisha na changamoto zake. Ukitumia maarifa haya kujaribu kutafuta jawabu la swali linalokutatiza unaweza ukajikuta unamachaguo mengi juu ya swali moja na unashinda kwa kishindo.

Elimu hususani ya kiafrika inahitaji mtu afikirie mwenyewe nje ya boksi yaani kutumia maarifa ya darasani kutatua changamoto fulani katika jamii na hii ndo itakupa ujira wa kujiendesha na kujiendeleza zaid lakini wasomi wengi husubiri ajira. Hebu tukae chini na kujifikiria nchi bado changa na kwa kiwango kikubwa nchi za afrika bado changa ko haziwez kutuajiri na kutuhakikishia maisha bora kila mtu ilihali kuna vikwazo vingi vinatoka kwa mabeberu.

Hvyo basi kutambua hili iwe kama chachu ya kusukuma uvumbuzi na jitihada chanya zisizotafuta mkato rahisi zaidi kutuletea mafanikio. Vijana na watu wa rika la kati na watu wazima kila mmoja kwa namna yake afanye kazi kwa weledi, ajitoe kwa moyo na kutumia maarifa yake kutatua changamoto fulani katika jamii kwan kama ubunifu au jitihada zetu zitatatua changamoto ya kawaida na kipato ni cha kawaida au kama ni tatizo kubwa sana basi na kipato kitakuwa kikubwa ila uvumilivu ni muhimu. Huwezi ukapanda asubuhi uvune jioni.
Kwa sasa tumekuwa na uwanda mpana wa kujiendeleza na kutanua maarifa kwa njia rahisi na gharama nafuu zaid kidijitali hvyo basi tutumie rasilimali elimu vizuri ituletwe manufaa makubwa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom