ELIMU NA MAZINGIRA YETU.
Habari hii itajikita katika Elimu tunayowapatia vijana wetu na namna isivyoakisi kwa asilimia miamoja mazingira yetu.
Elimu, ni maarifa yatolewayo darasani au nje ya darasa, kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine au kundi la watu, pia kutoka kundi kwenda kwa mtu au kundi lingine, pia inasifa ya kurithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine. Elimu inaweza kutolewa katika njia iliyo rasmi na isiyo rasmi, na katika mazingira hayo Elimu inaweza kujikita katika nyanja za Kiuchumi, Kisiasa, Kitamaduni, na hata Kijamii. Hii yote inafanyika kwa kufundishwa au kukaririshwa katika mfumo Rasmi ama usiyo Rasmi.
Mazingira, Mazingira ni kitu chochote kinachomzunguka Mtu/Binadamu tunazungukwa na vitu kama Watu/ Binadamu wengine, misitu, mashamba, na vitu vingine kedekede.
Baada ya kuona Maana za kimandhari za haya Maneno Mawili (Elimu na Mazingira) sasa tujikite zaidi kwenye Mada, Ambapo tutaangalia Namna Elimu yetu Isivyoakisi kwa Asilimia Miamoja (100%) Mazingira Yetu, hii itaangaliwa Moja kwa moja katika nyanja tatu,
Tukianza na hili la kwanza;
Ratiba na namna Elimu yetu inavyotolewa kwa watoto na vijana wetu. Hapa tunaangalia namna mtoto anavyobanwa na Ratiba ya Elimu Rasmi ambayo inaupungufu mkubwa unaolenga zaidi ukariri wa mambo ambayo kwa asilimia kubwa katika mazingira aliyopo hayampi fursa ya kuyajua, kuyaelewa na kuweza kuyamudu zaidi ya kujifunza kwa kukariri.
Mfano, Mtoto anajifunza uchumi wa kikoloni darasani, mtoto anajifunza utawala wa kikoloni, lakini Je? Mtoto anayaelewa Mazingira ya nchi yetu au jamii zetu kiuchumi, kijamii, kisiasa na kitamaduni, Hivo utakuta Mtoto anajifunza vitu ambavyo ni nje na Mazingira yake, Akili yake haijiandai kuyakabili mazingira yake bali kukariri.
Mtoto anapelekwa Chekechea akiwa na miaka miwili na kidogo ama mitatu, huko ratiba yake kwa asilimia kubwa ni ya darasani na michezo, hamna somo la ziada la kufahamu hata Elimu ya mazingira au ujasiriamali na namna ya kukabiliana na Mazingira yanayomzunguka, Muda wote atakuwa na heka heka za kusoma vitu vingi visivyoendana na mazingira katika ratiba yake, atadumu humo mpaka Shule ya Msingi, baadae Sekondari na hatimae Chuo.
Sasa hii inapelekea lile Jambo la pili;
Aina ya Wahitimu tunaowapata kupitia Elimu yetu na namna ambavyo wanashindwa kuyamudu mazingira na kupelekea ugumu wa Maisha kutokana na Ukosefu wa Ajira, maana vijana wetu wanashindwa kujiajiri kutoka na mfumo wetu ambao unakuwa umewaandaa vijana Kuajiriwa. Kijana anahitimu chuo fikra ni ajira ya serikali Au taasisi binafsi na si vinginevyo, sababu kubwa, Elimu aliyopata haimpi fursa ya upanuzi wa mawazo ya kujiajiri ama kufanya kitu kingine nje ya kuajiriwa, Elimu haijamuandaa katika Mazingira ya kujiajiri.
Na hii inajidhihirisha pia kwenye Jambo la tatu;
Namna Serikali inavyoshindwa kutatua baadhi ya changamoto kutokana na uhafifu Wa Elimu yetu Kuendana Mazingira. Kwa sababu na wao, Viongozi wetu wa kiserikali wamepita katika mfumo huu huu hafifu ambayo hauendani na Mazingira yetu matokeo yake ni haya ya kuwa na changamoto za Ugumu wa Maisha ambao kwa asilimia kubwa unatokana ukosefu wa ajira, Ubunifu na namna ya kuyakabili Mazingira yetu.
Rai Yangu kwa Mamlaka husika.
1. Ziangalie namna ya kurudisha Somo la Elimu ya kujitegemea.
2. kutanua Wigo wa Somo la Elimu ya Maarifa/Ujuzi wa kimaisha badala ya kuwa Mada katika somo fulani.
3. Ni vyema sasa Elimu ya kimazingira ikawa inatolewa nchini kote inayohusu Mazingira ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kitamaduni, Ili vijana waelewe nikitoka eneo hili nikaenda eneo lile nitakutana na kitu gani, nini wanalima, nini wanafanya, wanaishije, nje ya kuajiriwa naweza kufanya nini au nijiajiri katika kitu gani. Hii pia itatusaidia kwa namna moja ama nyingine.
Pia kwa Jamii, ni vyema watoto wakaanza kujengwa kiakili wakijua ni namna gani mazingira yetu yalivyo kwa kushirikishwa katika shughuri mbali mbali zinazoingizia familia kipato au chakula, mfano ni mfugaji wa kuku, ni vyema mtoto akashiriki kufuga kuku na pengine ukamgawia kuku wa kufuga, Akiuzwa yule kuku au wale kuku, mweleze mtoto hii pesa ndio Ada yako ya shule, hii pesa ndio mahitaji yako ya shule au ya hapa nyumbani, mtoto ataelewa na kujua namna pesa inavyopatikana, huyu hata asipoajiriwa kuna kitu cha ziada anacho.
Pia kwa sasa yapo ya kukatisha tamaa kwa wasomi, Mfano kuna baadhi ya kazi huwezi kujumuika na wenzako ikijulikana unakiwango fulani cha elimu, hii inatokana na namna au usumbufu wa hao wasomi wenyewe wakipewa hizo kazi lakini pia fikra za watu wenyewe wanaotoa hizo kazi. Kwa sababu utaambiwa wasomi ni wasumbufu, hawakubali malipo kidogo, wanadharau baadhi ya kazi. Lakini sio wasomi wote wenye tabia ya kudharau kazi, tujue kama jamii pia ni wajibu wetu kuwafundisha na kuwarithisha kazi zingine nje ya taaluma ya Elimu kwa vijana wetu.
Hii itasaidia kuondokana au kupunguza tatizo la Ajira katika jamii zetu, ambapo itatusaidia pia kuondoa ugumu wa maisha au tatizo la Umaskini na utegemezi wa vijana kwa wazazi kwa muda mrefu zaidi.

1. Ratiba na namna Elimu yetu inavyotolewa kwa watoto na vijana wetu.
2. Aina ya Wahitimu tunaowapata kupitia Elimu yetu na namna ambavyo wanashindwa kuyamudu mazingira na kupelekea ugumu wa Maisha.
3. Namna Serikali inavyoshindwa kutatua baadhi ya changamoto kutokana na uhafifu Wa Elimu yetu na Mazingira yanayotuzunguka.

Upvote
4