Elimu na Nidhamu

Elimu na Nidhamu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Sio lengo la elimu kuzalisha watu wenye tabia mbaya. Bali ni lengo la elimu kuzalisha watu wenye tabia njema ambao watasaidia kupeleka mbele taifa letu.

Elimu inapozalisha watu wenye tabia mbaya inakuwa haina matunda kwa taifa. Elimu ya namna hii huangamiza taifa badala ya kulijenga.

Elimu sio digrii peke yake. Bali pia tabia ya mtu ambayo lazima ijengwe na elimu hiyo ili kumfanya awe productive citizen.

Siku hizi tunawasomi kama wanavyojiita wanaoliangamiza taifa badala ya kulijenga. Usomi wao umekuwa hauna faida kwa taifa.

wasomi wa namna hii wako kila sehemu, kwenye siasa na kwenye taaluma mbali mbali. Maadili yameshuka kwa kiwango kikubwa.

Na kama wasomi wetu ambao tunawategemea na mfumo wetu wa elimu utaendelea kujenga wasomi wasio na maadili ya kutosha pamoja na nidhamu; tusahau kuhusu ufisadi na rushwa katika taasisi za umma.

Pamoja ya kwamba elimu inaweza kujenga maadili na nidhamu ya wetu. Kama tutakuwa makini kuijenga kuwa hivyo . Na kama itakuwa hivyo naamini itakuwa na manufaa kwetu. Kwasababu watu wetu watakuwa na uwezo wa kuchagua kilicho bora na sahihi kwa taifa lao.

Serikali inawajibu wa kusimamia maadili na nidhamu katika jamii. Kuzuia rushwa na ubadhirifu wa mali za umma na kujenga harmonius society. Ambayo haki ndio itakuwa mhimili mkuu.

Ni wajibu wetu kufahamu kuwa na elimu sio kuwa na skills tu za kazi lakini pia elimu lazima ijenge tabia ya mtu. Kuondoa ujinga ni kuondoa tabia zote mbovu ambazo humfanya binadamu kutenda katika njia ambayo sio sahihi hivyo kuleta madhara katika jamii yake na taifa.

Ni jukumu la elimu kutengeneza na kujenga raia ambao watakuwa wanawajibika kwa taifa lao, kwa familia zao na kwa jamii. Mtu mwenye elimu ni yule anayetenda katika usahihi. Elimu yetu ni muhimu kujenga na kukuza uwezo wa kufikiri
wa watu wetu badala ya kuwalisha maarifa.

Baadae yetu inategemea sana maamuzi sahihi tunayofanya sasa, mwelekeo wa taifa letu unategemea maamuzi yetu. Sio tu ya viongozi wa taifa hili , bali pia viongozi wa familia zinazounda taifa hili. Ufanisi wa familia zetu na maadili ya familia zetu, ndio yanayojenga taifa imara au bovu la watu wasio na nidhamu.

Taifa la watu wasio na nidhamu halina dira. Hakuna kuheshimiana wala kusikilizana. watu hupinga hata kilicho bora kwa taifa lao. Ni muhimu kujenga nidhamu katika taifa. Na kufuata kilicho bora kwaajili yetu.

Tukisema kwamba tutaendelea kama taifa pasipo nidhamu tutakuwa tunajidanganya. Malengo yetu kama taifa yanategemea sana umoja wetu na nidhamu yetu. Nasema kuendelea kwa taifa hili ni ngumu kama hatutabadilika.

Ni lazima tubadilishe mtazamo wetu ili taifa letu liendelee. Na kutenda yaliyosahihi kwa taifa letu. Lakini pia kutendeana sisi kwa sisi yaliyosahihi.
 
Back
Top Bottom