Elimu na siasa kama mapenzi na shule

bornsave

Member
Joined
Jan 22, 2013
Posts
45
Reaction score
5
wadau nchi yetu ya Tz imeshikiliwa na wanasiasa kiasi kwamba kila sehemu ni siasa tu. sasa imefikia hata kwenye swala la msingi kama ELIMU nalo limewekwa kwenye siasa. mambo mengi yamekuwa yakiahidiwa katika elimu lakini hayana utekelezaji. leo naongelea swala moja tu ambalo ni ajira kwa walimu wapya. mh alipokuwa sehemu aliongea kwamba tutaajiri walimu wapya mwanzoni mwa mwezi wa kwanza wananchi walipiga makofi mengi, lakini la kusikitisha hakuna kilichotekelezwa la zaidi watu wamebaki midomo wazi wakiwaza yale makofi waliyopiga. akaja naibu wazir akaongea kitu kama kile cha kusikitisha tena hatuwaoni tena wakiongelea hili swala (NO FEEDBACK), vilevile hawasemi kuna tatizo gani ili walimu hawa waendelee tu na majukumu mengine (kulima,biashara n.k). kwa swala kama hili inauma sana ndugu zetu walimu wamebaki tu wapowapo mtaani na kule mashuleni wanafunzi wanafeli ukiwauliza kwa nini wanasema hatuna walimu. viongozi wa siasa mtuachie elimu yetu.ELIMU ITABAKI KUWA ELIMU NA SIASA ITASIMAMA UPANDE WAKE.
 
Hakuna kitu kibaya kama kuchanganya siasa na mambo muhimu ya kijamii kama hayo, ni bora wangekaa kimya kuliko kusema mambo wasiyoyaweza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…