PrinceZuko
New Member
- Aug 26, 2022
- 2
- 1
“Elimu ni ufunguo wa maisha” nakumbuka huu msemo ndio ulikuwa motto na salamu tuliyotumia kusalimia walimu wetu kipindi niko shule ya msingi Diamond. Kwa kipindi hiko tulitamka maneno hayo kwa kuyaamini kabisa na yalitupa nguvu mno ya kusoma kwa bidii ili baadae tuje kuwa na maisha mazuri.
Sasa nina miaka 26, nina umri sawa au unaokaribiana na rafiki zangu wengi niliosoma nao kipindi kile ambao kwa pamoja tulikuwa tukitamka msemo wa elimu ni ufunguo wa maisha kwa sauti kubwa na yenye tumaini kubwa la siku za usoni, na kwa asilimia kubwa darasa letu liliendelea vizuri kwenye hatua za mbeleni yaani wengi wetu tulibarikiwa kuendelea na elimu ya sekondari mpaka chuo.
Wengi wetu tukiangalia nyuma na kukumbuka ule msemo tuliokaririshwa shuleni tunaona kama tulidanganywa, kwa kuwa msemo ule hauakisi hali zetu za maisha kwa sasa, kwa lugha nyepesi elimu haijatufungulia maisha! Ila tunashukuru imetutoa ujinga.
Muda mwingine tukizungumza kwenye makundi yetu ya mitandao hasa kwenye mtandao wa whatsapp huwa tunakumbushana huo msemo na kucheka sana, vicheko vinavyoonesha kukata tamaa, kuchoka, kuhisi kusalitiwa na elimu na muda mwingine tuna amini kuwa msemo wa elimu ni ufunguo wa maisha ni uwongo na tulidanganywa.
Hapana! Huu msemo uko sahihi kabisa na wala hatukudanganywa, elimu ni ufunguo wa maisha! Kwa sababu nina ushahidi wa watu wengi waliofanikiwa kutokana na elimu, na dunia ya leo inapiga hatua kwa sababu ya elimu, lakini Tanzania tuko nyuma hatuendani na kasi na mabadiliko ya elimu. Elimu yetu haitukomboi, haituimarishi, haitujengi, bali inatudumaza na kutufunga kwenye boksi moja la mfumo ambao kwa sasa umepitwa na wakati.
Wengi tunasoma ili tupate ajira, ama kwa kuajiriwa au kwa kujiajiri na ndipo hapo elimu inakuwa ufunguo sahihi wa maisha. Ila kwa bahati mbaya elimu yetu imetengeneza wasomi wengi ambao wameshindwa kuajiriwa ama kujiajiri na kusababisha kuona elimu ni uwongo na vyeti vyetu kuona kuwa tumepigwa. Nini kifanyike ili elimu kweli iwe ufunguo wa maisha?
Suala la ajira ni tatizo la nchi nyingi sio Tanzania pekee, tofauti ni kuwa mataifa mengine yalizinduka haraka na kuona mabadiliko ya uchumi, ajira, hayawezi kutatuliwa na mfumo mmoja tu wa elimu ambao mimi nauita mfumo wa makaratasi, nina maana gani?
Mfumo wa makaratasi nina maana kuwa hatua za ki elimu ziko wazi na zimeandikwa kwenye makaratasi either kwenye mihula yetu, katiba zetu, mamlaka zetu husika nikiwa na maana ya wizara na baraza la elimu. Mifumo hii imeelekeza ni kwa namna gani mtoto ataanza kusoma, na atasoma vitu gani, atajifunza nini, anahitaji alama ngapi kupanda hatua, na taifa litamchuja kwa kila hatua kupitia mitihani na litampa cheti ambacho kitamsaidia kumpelekea moja kwa moja kwenye soko la ajira.
Tayari mifumo imewekwa ambayo mpaka imetupangia umri wa kuanza kusoma. Ni kweli mfumo huo umefanya kazi kwa miaka mingi na kujenga taifa hili, lakini mfumo huo haukujiandaa na tatizo la ajira tunaloliona leo. Vijana tumekuwa tukijua yatupasa kusoma, tupate vyeti ili tuajiriwe.
Na wote tunasoma kwenye mfumo mmoja tukitofautiana kwenye ujuzi tunaosomea. Nini maoni yangu kwa serikali na wadau?!
Tuboreshe mfumo wetu wa elimu uweze kumuandaa kijana ambaye ana uwezo, ujuzi, akili, ubunifu na elimu ya kuweza kuajiriwa ama kujiajiri akiwa kwenye muda sahihi na umri sahihi.
1. Serikali kupitia wizara ione ni kwa namna gani itapunguza miaka ya kusoma kwa watoto na vijana hasa kwenye elimu ya msingi na sekondari kwa kujumuisha baadhi ya madarasa badala ya kusoma kwa miaka miwili tusome kwa mwaka mmoja. Mfano darasa la kwanza na la pili linaweza kusomwa kwa mwaka mmoja, darasa la sita na la saba linaweza pia kusomwa kwa wakati mmoja. Hapo tumekomboa miaka miwili tayari.
2. Michepuo O level ianze mapema, mtoto akiwa kidato cha kwanza anatambulishwa na masomo 13 yakiwemo ya sayansi na biashara. Akifika kidato cha pili basi watoto waanze kutofautishwa, watakaosoma sayansi, biashara na masomo ya arts.
Hii itawaandaa mapema wanafunzi kuchagua masomo wanayoyapenda na fani wanazozipenda na wanazoamini wana uwezo nazo ki akili na uelewa, hapa tunakuwa tunamkabidhi mwanafunzi uwezo wa kutumia nguvu zake nyingi kwenye masomo anayoyapenda kuliko asiyoyapenda na asiyokuwa na uwezo nayo. Kwenye upande wa A level na vyuoni pengine hakuhitaji mabadiliko sana.
3. Tufanye marekebisho kwenye mitaala na masomo yetu kwa kupunguza baadhi ya topic zisizokuwa na faida sana na kutambulisha elimu mpya kwenye masomo yetu ambayo inaendana na ulimwengu wa sasa. Mfano elimu ya digital currency au fedha ya kidijitali tukijikita kwenye forex, bitcoin, nft’s n.k kuhakikisha elimu hii inadumbukizwa kwenye masomo ya biashara kuanzia ngazi ya A level hadi vyuoni kumuandaa kijana kuona fursa nyingine ya kuji ajiri ama kuajiriwa huko.
Elimu ya coding inaweza dumbukizwa kwenye somo la kompyuta kuanzia ngazi ya o level mpaka vyuoni kuwaandaa wataalamu kwenye nyanja hizo.
Lazima tukubali elimu yetu imedumaa haiendani na kasi na mabadiliko ya kimaisha ya dunia, inapaswa kubadilika. Kwa hayo machache na mengine mengi ya kufanana nayo nina amini elimu itatukomboa na kuwa kweli ufunguo wa maisha yetu.

Upvote
0