Shida Masuba
Member
- May 30, 2016
- 6
- 4
ELIMU NCHINI TANZANIA
Mwandishi: Shida Masuba
1.0. Fasili ya Elimu
Kwa mujibu wa sera ya Elimu na Mafunzo (2010:1) inafasili elimu kuwa ni “mjumuisho wa maarifa na stadi za kujitambua na kukabiliana na changamoto zilizopo katika mazingira na mabadiliko ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia. Elimu hupatikana kwa mchakato wa kufundisha na kujifunza. Mafunzo ni mchakato wa kupata maarifa, mwelekeo na stadi.
Fasili hii inatupa dira kuwa lengo kuu la elimu ni kutoa maarifa ya kutambua mazingira, changamoto za mazingira hayo na njia za kuzitatua changamoto hizo ama kupitia ubunifu au njia ambazo zimepatikana kupitia maarifa uliyoyapata darasani. Sanjari na hilo, fasili hii inatupeleka mbali zaidi kwamba elimu dhima yake kubwa ni kumfanya mtu ajifunze kinadharia kisha akatumie kwa vitendo katika maisha na ulimwengu halisi wa jamii inayomzunguka. Licha ya elimu kutolewa kwa nadharia na vitendo, basi lengo la mafunzo ya vitendo ni kuthibitisha juu ya kile ambacho amejifunza kinadharia akiwa darasani kisha azitatue changamoto zinazoikabili jamii yake pamoja na yeye mwenyewe.
1.1 Elimu ya Tanzania na Ajira
Ajira ni neno la Kiarabu lenye maana ya kazi yoyote ambayo mtu anafanya kwa malipo katika kampuni, ofisi za serikali, taasisi au kwa mtu mwingine binafsi, hii ni kwa mujibu wa Wikipedia. Ajira ya taasisi na mtu au kampuni na mtu au serikali na mtu, ni mahusiano na mapatano baina ya mwajiri na mwajiriwa ambao hawana budi kukubaliana kwa mujibu wa sheria ambayo huwekwa bayana katika mkataba ili kulinda haki za pande mbili yaani mwajiri na mwajiriwa.
1.1.1 Hali ya Ajira Tanzania
Kwa mujibu wa wa takwimu ya mwaka 2013 inaonesha kuwa idadi wa waajiriwa ni wachache zaidi kuliko mahitaji ya serikali na taasisi binafsi zenye uhitaji wa watumishi. Tukirudi nyumwa kawa 2004 Rais wa awamu ya nne Mh. Jakaya M.A. Kikwete aliamua kuanzisha programu ya muda mfupi kwa wahitimu wa kidato cha sita ili kukabiliana na tatizo la uhaba walimu shuleni. Mbali na hilo aliruhusu mpango wa walimu vyuo vikuu kusoma kozi ya Ualimu kwa miaka 3. Hili lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, mbali na hilo ajira zilitolewa wakiwa wanamaliza chuo. Baada ya kumaliza mitihani kulikuwa na fomu za ajira ambapo wahitimu walijaza mikoa na shule ambazo wangependelea kufundisha. Jambo hili lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kukata mzizi wa fitina kwa wanafunzi shuleni. Kwani waliwapata walimu kwa wakati muafaka kabisa.
Changamoto ya ajira ilianza kujitokeza katika mwaka wa 2015/2016 utawala wa nchi ulipobadilika, ajira hazikutolewa tangu mwaka huo hadi mwaka 2021/2022 kwa nini tunasema hazikutolewa, ni kwa sababu kumekuwa na mlundikano mkubwa wa wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu yaani Astashahada, Stashahada, Shahada, Umahiri na hata Uzamivu. Serikali haikutoa mwanya mkubwa wa ajira kwa wahimu, sanjari na hilo, mfumo wa uombaji ajira ulibadilika kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Mbali na changamoto ya kimtandao wahitimu wengi ambao kwa miaka 6 hawakupata ajira wakajiingiza kwenye ajira binafsi. Miongoni mwa ajira hizo ni pamoja na kilimo, biashara ndogondogo, uwakala, na wengine kuwa wajasiriamali ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto za ajira. Serikali ya awamu ya tano iliwapa hamasa kwa kuwapatia vitambulisho vya mjasiriamali.
Serikali ya awamu ya sita imeleta changamoto kwa sababu ya kodi za miamala (tozo), pembejeo kuwa juu mara dufu, tozo kwenye mabenki. Suala hili linaleta changamoto kubwa na kuona elimu tuliyopata haisaidii haswa kwa viongozi wetu. Kwani hawana mawazo mbadala ya kumwinua mwananchi anayepambana na mazingira kujikomboa anadidimizwa kutokana na mfumo wa kiutawala kumfanya chanzo kikubwa cha mapato ya taifa kwa njia shabihanifu.
1.2. Elimu na Lugha ya Kufundishia
Tanzania ni nchi yenye lugha nyingi zaidi ya mbili (Ulumbilugha). Katika mawasiliano ya kitaifa na mfumo wa elimu kuna uwililugha (lugha mbili) Kiswahili na Kiingereza. Sera ya lugha na utamaduni inabainisha kuwa lugha ya Kiswahili ni ya kufundishia ngazi ya shule za Awali na Msingi za serikali na Kiingereza ni somo, huku kuanzia sekondari ya kawaida hadi vyuo vikuu, Kiingereza ni lugha ya kufundishia na Kiswahili ni somo.
Changamoto zake ni kwamba
i. Mtoto hupata lugha katika umri wa mwaka 0-hadi umri wa balehe, hivyo kipindi hiki chote anakuwa shule ya awali hadi msingi kama anavyodai Stampe 1979. Anapata kanuni na kumudu lugha ya Kiswahili. Afikapo sekondari michakato ya kujifunza lugha inafikia ukomo, hivyo huanza kujifunza lugha ya Kiingereza kama lugha ya pili akitumia misingi ya lugha ya Kiswahili. Tatizo linalojitokeza anashindwa kuimudu lugha na maarifa yanayowasilishwa kwa lugha ya Kiingereza.
ii. kukosekana kwa weledi kwa wahitimu kwa sababu walikuwa na majukumu ya kujifunza lugha na maarifa. Hivyo anajikuta kila jukumu amelitimiza nusu si kwa ukamilifu. Amebaki vingi akiwa amevikariri na anashindwa kuvileta katika mfumo wa maisha halisi ya kila siku.
iii. Kiswahili kutokufanywa lugha ya kufundishia ni changamoto ya wazawa na si ulimwengu kama wataalamu na wasomi wengi wanavyodai. Ikumbukwe kuwa lugha inaishi, inakua na inakufa. Lugha ya Kiswahili inakua kupitia mabadiliko ya kijamii, tabianchi, sayansi na teknolojia, utabibu nk. Iwapo katika mataifa mengine kukabainika kuwa kuna uvumbuzi fulani ni lazima msamiati uundwe kwa njia zilizoanishwa za uundaji msamiati wa lugha. Hivyo basi madai ya kuwa Kiswahili hakijitoshelezi si kweli bali hatupendi vya kwetu na tuna ukata wa msamiati. Lakini pia ninaamini kuwa wasomi wanaozungumza hivyo, hawajui siri ya lugha ya Kiingereza na Kijerumani kuwa na msamiati mwingi wa Kigiriki na Kilatini na Kifaransa. Sababu kubwa ni kuhawilisha maarifa kutoka lugha hizo kuja katika Kiingereza na Kijerumani.
1.3. Elimu na Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia
Katika karne hii kizazi kimejikita na kujizatiti katika sayansi na teknolojia. Kuna masuala ya uvumbuzi na utumizi mkubwa wa teknolojia, katika tiba, elimu, biashara nakadhalika. Kutokana na mabadiliko hayo, elimu yetu katika mitaala na mifumo yake inapaswa kujielekeza katika sayansi na teknolojia. Somo la sayansi na teknolojia, liwe la lazima na si hitiari. Aidha, sayansi hii ijikite katika tiba, kwa kutumia teknolojia mpya, elimu kwa kutumia teknolojia mpya, ufundishaji uhusishe namna ya kuendesha biashara kiteknolojia, kutengeneza tovuti, aplikesheni za kampuni ama huduma mbalimbali, nk
1.4. Hitimisho
Fauka, elimu ni muhimu itolewe kwa kuzingatia lugha ambayo inamkuza mtoto kwani itamwezesha kupata maarifa faafu na kuyakabili mazingira yake ipasavyo. Lugha ni utambulisho wa mtu na jamii yake na hufumbata maarifa yake.

Upvote
1