SoC01 Elimu ndiyo Balozi namba moja wa mabadiliko

SoC01 Elimu ndiyo Balozi namba moja wa mabadiliko

Stories of Change - 2021 Competition

MaraVeteran

New Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
3
Reaction score
4
Elimu ni dhana inayoelezewa kwa namna nyingi na kufafanuliwa kulingana na mahala, wakati na shughuli.

Elimu ni uhamishaji wa maarifa, mbinu na ujuzi kutoka kwa mtu mmoja, jamii moja au kizazi kimoja kwenda mtu mwingine, jamii nyingine au kizazi mingine.

Moja kati ya viashiria vya elimu ni mabadiliko chanya, juu ya elimu uliyoipokea. Yaani hata kama ulikuwa ukijifunza uchawi au mauaji, basi utaelimika pale tu utakapoweza kuyatumia maalifa uliyopewa ipasavyo.
Hata hivyo elimu zimegawanyika katika Hali mbalimbali kama vile aina na mfumo.

Katika kipengere cha aina za elimu. Kuna aina tatu za elimu. Yaani elimu rasimi, elimu isiyo rasimi na elimu rasimi nyongeza.

Elimu rasimi ni ile inayotolewa katika eneo maalumu, ikiwa na walimu au wakufunzi rasmi, ikiambatana na mtaala (curriculum) na mkhitasari(syllabus) rasimi pia mwanafunzi hupimwa kwa mitihani na hutunikiwa cheti baada ya kuhitimisha masomo. Watu wengi hujua aina hii ya elimu (kisomo) kama elimu pekee.

Elimu rasimi nyongeza. Hii ni aina ya elimu ambayo inaambatana na shughuli mbalimbali zinazofanyika kwenye elimu rasimi, shughuli hizo si sehemu ya mkhitasari ila husindikiza mtaala. Mfano michezo mashuleni, Vikundi vya kijamii n.k.

Elimu isiyo rasimi. Hii ni aina ya elimu ambayo mtu huipata katika mazingura, hii haina mitihani wala vyeti. Aina hii ya elimu hupatikana mtaani kupitia uzoefu, changamoto, kuiga au kujisomea mwenyewe au nyumbani kutoka kwa wazazi au walezi.

Tukiachana na aina za elimu, pia kuna mfumo wa elimu ambao ni mfumo elimu shirikishi na elimu isiyo shirikishi.

Elimu shirikishi ni ile inayotolewa na Mkufunzi akishilikiana na wanafunzi katika kuchangia mawazo ili kufanya mada ieleweke zaidi. Mfano kwenye semina za kilimo, ufugaji, shule za misingi na sekondari. Yaani katika mfumo huu mwanafunzi huluhusia kuchangia mawazo na kuuliza maswali.

Elimu isiyo shirikishi ni ile inayotolewa na Mkufunzi bila kuwashilikisha wanafunzi katika kuchangia mawazo juu ya mada husika. Yaani hapa mwalimu au Mkufunzi ndiyo chanzo cha maalifa. Mfumo huu hutumia imla. Mfano wa elimu hii hupatikana Jeshini, kwenye nyumba za ibada yaani anachokisema kiongozi au mkuu ndo kinachofanywa hakuna maswali wala maoni.

Elimu ndiyo nguzo muhimu katika maisha na maendeleo. Napoongelea elimu simaanishi kisomo pekee, Bali dhana mzima ya elimu.

Wakoloni walipotaka kuitawala Africa walianza na elimu, wapigania Uhuru walipotafuta Uhuru elimu ilihusika pakubwa ndipo juhudi zingine zilifuata.

Tatizo la elimu ni moja, endapo elimu haitaendana na mfumo wa kijamii, kisiasa na kiuchumi basi elimu hiyo haitafaa. Maana elimu ni chombo na Mali ya jamii na si mali ya Serikali, Serikali ni mdau kama ilivyo wahisani japo nafasi yake ni usimamizi na siyo uamuzi.

Elimu ikiwa mbovu tutalajie kizazi kibovu, kizazi kikiwa kibovu tutalajie jamii mbovu, jamii ikiwa mbovu tutalajie siasa mbovu, Siasa ikiwa mbovu tutalajie uchumi mbovu. Hivyo vyote vikiwa vibovu tatarajie maisha magumu na mabaya.

Usukani wa elimu ni mtaala (curriculum), hapa ndo kuna muongozo wa nini kifanyike, mahala gani na wakati gani na kwasababu zipi. Mtaala katika elimu ni sawa na katiba katika Siasa japo katiba ni mawanda mapana maana hugusa mitazamo yote mitatu moja kwa moja ila mtaala hujikita saana kwenye elimu ambayo ni kipengere cha jamii japo husukumwa na mitazamo mingine kama Siasa na uchumi.

Mtaala hufuata mahitaji ya jamii. Tatizo la Serikali nyingi huwa zinalazimisha Mtaala kufuata matakwa yao badala ya matakwa ya jamii. Mfano mtawala atalazimisha mtaala kuandaliwa na wanasiasa ambao si wabobezi wa maswala ya elimu.

Pia mtaala huathiriwa na mfumo tegemezi. Mfano misaada ya wahisani kutoka nje ya nchi (jamii). maana hawa wahisani wataingiza matakwa yao ili kukidhi haja zao au kueneza elimu na kudumaza elimu ya jamii.

Katiba pia haiongelei saana maswala ya kijamii ila imejikita katika siasa yaani Serikali, utawala uongozi na mihimili na mamlaka, jambo ambalo linaathiri hadi mfumo wa elimu. Katiba isaidie mtaala katika kuhakiisha elimu inakuwa na nguvu.

Kwa mataifa yaliyopiga hatua, elimu ni silaha ya kivita katika maendeleo, ila kwa jamii za shikamoo marahaba elimu inafanywa kwa mazea. Mfano Walimu watambuliwi wala kuthaminiwa na nadharia huwa na nguvu kuliko masomo ya vitendo, bajeti ndogo.

Mtaala usiotambua kipaji cha mwanafunzi mtaala huo haufai. Na kwa elimu ya jamii zetu mtaala haufai maana watu wanasomea mitihani na siyo talanta aliyo nayo. Yaani mtu asiweza kingereza anaonekana ni mbumbumbu jambo ambalo siyo kweli. Huu ndiyo mwanzo engineere anaenda kuwa mwalimu, rubani anaenda kuwa mwalimu, mfanya biashara anaenda kuwa mwalimu mwisho wa siku wanafunzi hawaelewi waalimu maana walimu hawana vipaji hivyo na wenye vipaji wamekimbia kwa kuofia maslahi.

Katiba mpya itambue umuhimu wa elimu, itambue umuhimu wa elimu, waalimu watambuliwe, mtaala urekebishwe utambue vipaji, hiyo itakuwa chachu ya Wali ya mabadiko, vinginevyo tutaendelea kumsoma Napoleon Bonaparte huku tukishindwa kutengeneza hata jembe la mkono na tutaishia kunyosheana vidole.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom