Elimu ni cheti au ni ujuzi?

Ndio maana nikasema ni cheti cha kuthibitisha elimu kwenye mabano nikasema lakini sio ujuzi kwakuwa watu wanaweza kununua cheti cha elimu lakini sio ujuzi
 
Elimu ni ujuzi, cheti ni kama uthibitisho wa kinadharia kuwa tuna assume unao ujuzi hivyo ngoja upewe nafasi tuone kuwa kweli ujuzi upo?....Twende kibongo bongo sasa, bongo Elimu ni cheti Kwa asilimia kubwa, ndio maana kama huna cheti hupewi nafasi uoneshe ulichonacho maybe upitie chocho Kwa chocho ujikomboe mwenyewe bila kushikwa mkono na govt.

Hapa mm nimeongelea ujuzi wa kutatua changamoto Tu na siyo ujuzi kama wa mawasiliano na vinavyofanana na hivyo .
 
Kama changamoto hazitatuliwi inatafsiri, hakuna ujuzi?
 
Kwa huku kwa kina makonda ni cheti hata kama hujui chochote kilichopo kwenye chati chako
 
Ulisomea vitu gani hasa mkuu
 
Cheti ni kwa ajili ya kuajiriwa tu. Unaweza kuwa na ujuzi bila cheti hautaajiriwa. Ni rahisi kupata ujuzi kuliko kupata cheti. Ujuzi unaupata hata ukiwa mitaani kwa kuiga wenye ujuzi waliousomea shuleni/chuoni
 
Kuna watu ni wajuzi wa fani na taaluma mbalimbali za kimaisha ila hawana cheti, hawaajiriwi ingawa waajiri wanawatamani sana kuwapata ila mifumo ya ajira haiwatambui
 
Kwa mtazamo huu, ni sawa na kusema tunaenda shule ili tupate vyeti na si kupata ujuzi ili tuajiriwe?
 
Kuna watu ni wajuzi wa fani na taaluma mbalimbali za kimaisha ila hawana cheti, hawaajiriwi ingawa waajiri wanawatamani sana kuwapata ila mifumo ya ajira haiwatambui
Je, na sekta binafsi inaangalia ujuzi au vyeti?
 
Kuna watu wamefika mpaka vyuoni kusomea fani na taaluma fulani wakaishia kutokutunikiwa cheti. Watu hawa wakirudi mitaani tayari wana ujuzi na maarifa ila hawakupata cheti huko chuoni kutokana na sababu mbalimbali. Basi hubaki na maarifa na ujuzi wao bila kutumika sehemu mahsusi. Angalau fani kama za ufundi, biashara na kilimo/ufugaji hizo mtu huweza kujiajiri mwenyewe na akatumia maarifa/ujuzi alioupata chuoni hata bila kupata cheti
 
Kwa hiyo nikitumia njia za mkato nikapata cheti, nitakuwa tayari nina elimu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…