SoC04 Elimu ni moja ya nguzo kubwa na muhimu katika safari ya kuyasaka mafanikio

SoC04 Elimu ni moja ya nguzo kubwa na muhimu katika safari ya kuyasaka mafanikio

Tanzania Tuitakayo competition threads

DUASMaka

Member
Joined
May 27, 2024
Posts
5
Reaction score
2
Elimu ni moja ya nguzo kubwa na muhimu katika safari ya kuyasaka mafanikio. Nchi ya Tanzania inatambua hilo na hadi kuweza kuwekeza katika elimu kwa wananchi wake. Tanzania imeweka kipaumbele kikubwa katika utoaji wa elimu kwa wananchi wake.

Tangu mwaka 2016 hadi sasa nchi yetu inaendelea kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi sekondari zote za umma. Hali hii imesaidia vijana wengi kufikia elimu ya juu yaani vyuo vikuu na vya kati.

Sekta ya elimu ni muhimu sana kuitazama kwa karibu kama sehemu nyeti inayoweza kutupatia taswira ya Tanzania tuitakayo. Kupitia sekta hii ya elimu sekta nyingine zote zinategemea kupata maendeleo yake kwa kuwaajili wataalamu waliotoka kusoma ambao ni wataalamu wa mambo mbalimbali kulingana na walivyo somea.

Kwahiyo, sekta ya elimu ni jiko la wataalamu wanaohitajika katika sekta nyingine zote nchini. Elimu yetu inaanza na mtoto akiwa mdogo hadi kuwa mtaalamu mkubwa, sasa basi sekta hii itazamwe kwa karibu na kuwekewa mifumo bora itakayoileta Tanzania tuitakayo.

Ili kupata mafanikio tunayoyahitaji kama nchi ni bora kuifanya sekta ya elimu kuwa sekta pacha ya kila sekta inayotegemewa kuleta mapinduzi ya kiuchumi nchini mfano sekta za nishati na madini, mifugo na uvuvi, kilimo, ulinzi na usalama, maji, mawasiliano na teknolojia na nyinginezo zote.

Sekta hizi zote zinaweza kushiriki kuzalisha wataalamu wao kwa namna bora kama ifuatavyo;
Shule nyingi huanza kugawa makundi ya wanafunzi kuanzia kidato cha tatu kwani wengine huchagua kusoma masomo ya sayansi wengine biashara na wengine masomo ya sanaa. Katika kipindi hiki sekta nyingine ziingie na kuanza kuchukua wanafunzi kwa idadi inayohitajika na nyongeza ya kadilio la watakaoshindwa au kufeli na kuanza kusomesha kwa kuwalipia ada ya masomo yao kama inavyofanya sekta ya elimu, Yaani sekta ya elimu isomeshe wanafunzi mwisho kidato cha pili na kuachia sekta nyingine ziwalipie wanafunzi zinaowahitaji kuja kuwa wataalamu wao kulingana na uhitaji wao.

Kitendo hiki kitapelekea yafuatayo;
1. Kupata wasomi bobevu na endelevu kwenye sekta husika.

2. Kuhakikisha wasomi wote watakaofika elimu za juu wanaajiliwa na kuepusha hasara ya kusomesha wataalamu tusiowatumia kwa sababu watakaochukuliwa ni idadi ya wale wanaohitajika na sekta husika na wengine kuendelea na mambo mengine ya kiuzalishaji.

3. Kuongeza ufanisi katika kutengeneza wataalamu wenye ubora na viwango vya juu zaidi kwani watakuwa wanatokana na sekta husika.

4. Kupunguza umri wa kusoma; wanavyuo wengi wanapoanza vyuo husoma pasipo kujua nini wanahitaji katika kusoma kwao na hatimaye kujikuta wanapoteza miaka mingi hadi kujua hatima yao ndio maana wengi wanaogopa kujiajili kwa sababu muda mwingi wameupoteza katika kusoma Mfano mwanafunzi anapofika chuo akiwa bado hajajua mengi hupata wakati mgumu katika uchaguzi wa kozi na baadae kujikuta anasoma kozi ambayo haikuwa ndoto yake.

5. Itasaidia kupata wasomi wavumbuzi kwenye sekta zao na kuondoa watu kufanya kazi ambazo si vipawa vyao.

Mwisho, Kwa kufanya hivi vijana wengi wakifika elimu za juu watakuwa tayali wanajua kwa kwenda kuisaidia nchi kupata mafanikio kuliko kumaliza na kuanza kujitafuta upya kama ilivyo sasa.

NB; Chapisho hili ni wazo kutoka kwa DUASMaka, huruhusiwi kukopi au kutumia bila idhini 🙏
 
Upvote 0
Back
Top Bottom